Sababu, dalili, matibabu na kinga ya fangasi sehemu za siri kwa mwanamke

By, Melkisedeck Shine.

uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png

Sababu, dalili, matibabu na kinga ya fangasi sehemu za siri kwa mwanamke

Fangasi ya ukeni husababishwa na fangasi aina ya Candida albicans. Ugonjwa huu huitwa vaginal candidiasis kwa kiingereza na ni kati ya magonjwa ambayo husumbua wanawake mara kwa mara.

Maambukizi

Fangasi ya ukeni huambukizwa kwa njia ya;
Vyoo vichafu.
Kuchangia nguo za ndani na taulo.

Sababu

Uwezekano wa kupata fangasi ya uke au fangasi ya uke kujirudia rudia unaongezeka pale ambapo mwanamke ana;
Kisukari.
Ujauzito.
Anatumia antibiotics kwa muda mrefu
Ukimwi.
Joto, unyevu mwingi na nguo za kubana huchangia pia kutokea kwa fangasi ukeni. Ugonjwa huu haumbukizwi kwa njia ya ngono.

Dalili

Fangasi ya ukeni inaweza kuleta dalili zifuatazo kwa wagonjwa wenye maambukizi;
Kuwashwa sehemu za siri hasa wenye uke na mashavu ya uke.

Kutokwa na maji maji meupe mfano wa maziwa kutoka kwenye uke ambayo hayana harufu mbaya.
Maumivu wakati wa kukojoa kwa baadhi ya wagonjwa. Mara chache hali hii hutokea, ikisabaishwa nakuchubuka wakati wa kujiwasha.

Matibabu

Matibabu ya fangasi ya uke hutumia dawa za kuua fangasi (antifungals). Mara nyingi dawa za kuingiza kwenye uke (vaginal pessaries) hutumika kwa muda wa siku 3 mpaka 6. Wakati mwingine dawa za kunywa zinaweza kutumika kutibu fangasi hii.

Muone daktari kwa ajili ya uchunguzi, dawa na dozi sahihi.Cotrimazole na ketoconazole ni kati ya dawa zinazotumika mara kwa mara.

Kinga

Pamoja na matibabu kuna hatari ya maambukizi ya fangasi hawa kujirudia, hivyo ni muhimu kupata tiba hospitali na kurudi unapoona inajirudia. Vitu vingine muhimu kuzingatia ni;
Usafi wa nguo za ndani; kuvaa safi iliyofuliwa kila siku na kuanikwa juani (au kupigwa pasi).

Vaa nguo za ndani zilizokauka vizuri. Epuka zenye unyevunyevu au mbichi.

Vaa nguo za ndani zilizotengezwa kwa pamba (hupunguza joto na hivyo hatari ya fangasi kuzaliana)

Usafi wa sehemu za siri na kujikausha viruzi baada ya kuoga.

Usafi wa choo ni muhimu sana.


uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Sababu, dalili, matibabu na kinga ya fangasi sehemu za siri kwa mwanamke;

a.gif Faida za kula karanga mbichi

Karanga ni muhimu sana katika afya ya mwili wa binadamu. Kiukweli karanga siyo chakula cha kupuuziwa iwapo utajua faida zake kama nitakavyokujuza leo katika makala haya… endelea kusoma

a.gif Matumizi ya tunda la shelisheli kama dawa ya ngozi

Shelisheli lililokomaa huwa na uzito wa hadi kilo 6, ambapo mshelisheli unaweza kukua kwa urefu wa kati mita 9 hadi 18 na huanza kuzaa matunda ukiwa na miaka 6 na kuendelea kwa miaka zaidi ya 50… endelea kusoma

a.gif Sababu na tiba ya tatizo la kukoroma usiku

Kukoroma ni tatizo linalowapata watu wengi wakati wanapolala ambalo linaweza kuwatokea watu wa kila umri ingawa hutokea mara nyingi kwa wanaume au watu wanene. Kukoroma huzidi kwa kadri umri unavyoongezeka na asilimia 54 ya watu wazima hukoroma baadhi ya wakati huku asilimia 25 ya wengine wakiwa na tabia ya kukoroma kila wakati. Kukoroma baadhi ya wakati kwa kawaida sio tatizo kubwa na mara nyingi huleta tu karaha kwa mtu anayelala karibu na mkoromaji… endelea kusoma

a.gif Faida za kunywa juisi ya ubuyu

Mungu ameumba miti na mimea kwa ajili ya binadamu. Kila mti au mmea una makusudio yake. Mbuyu ni miongoni mwa miti yenye faida nyingi na maajabu mengi. Vitu vyote vilivyomo kwenye mbuyu vinatumika kama chakula au dawa kwa faida ya binadamu… endelea kusoma

[Fumbo Kwako] 👉Je, glass ina Maji kiasi gani?

afya-mapishi-na-lishe.png

a.gif Mapishi – Kisamvu cha Karanga

Mapishi yetu leo ni kisamvu cha kuchanganya na karanga. Karibu… endelea kusoma

a.gif Chanzo, dalili, aina na matibabu ya ugonjwa wa kifafa

Huu ni ugonjwa ambao unasabababishwa na seli zilizopo katika mishipa ya fahamu zilizopo kwenye ubongo kutoa umeme[impulses] mwingi kuliko kawaida kwenda kwenye misuli na sehemu zingine za mwili, na kusababisha mtu kupata dalili kama vile kuishiwa nguvu, kichwa kuuma, kuchanganyikiwa, mwili kukakamaa na hata kupoteza fahamu. Hali hii hujirudia mara kwa mara… endelea kusoma

a.gif Faida za ulaji wa Peasi

Peasi ni tunda ambalo limekuwa halithaminiwi licha ya kuwa na faida lukuki katika mwili wa binadamu. Tunda hilo ambalo kwa umbo linafanana na tufaa (apple), lina faida nyingi kwa binadamu iwapo atalitumia mara kwa mara… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia tango

Tango ni tunda na ni mboga pia na ni chanzo kizuri cha potasiamu na vitamini nyingi ambazo zina kazi mhimu katika ngozi yako na huifanya ngozi ngozi ionekane laini na yenye kupendeza… endelea kusoma

[Jarida la Bure] 👉Jarida la kilimo bora cha matikiti

[Hadithi Nzuri] 👉Stori inayogusa!!

picha-kali.png

.

picha-kali.png
UJUMBE-WA-ASUBUHI-KWA-NDUGU.JPG
uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.