Njia za kuongeza wingi wa mbegu za kiume

Mpendwa Msomaji, baada ya kukuandalia makala inayopendwa kuhusu; Namna ya kutengeneza Visheti Vya Nazi Na Njugu (Sudani), sasa nimekuandalia makala hii kuhusu;

Njia za kuongeza wingi wa mbegu za kiume.

Unaalikwa pia kusoma kuhusu; Dondoo kuhusu tezi dume.

Njia za kuongeza wingi wa mbegu za kiume

By, Melkisedeck Shine.

Kula lishe bora

Chakula unachokula kina mchango mkubwa katika kutibu tatizo hili. Vyakula vingi vya kisasa havina uwezo wa kuongeza uwingi wa mbegu.

Punguza matumizi ya sukari na vyakula vya ngano. Ongeza zaidi matunda, mboga za majani na mafuta yenye afya.

Acha kutumia kahawa, vinywaji na vyakula vyenye kaffeina

Kama una tatizo la kuwa na mbegu chache ni vizuri ukaacha kutumia vinywaji au vyakula vyote vyenye kaffeina kwanza.

Matumizi ya kitunguu swaumu

Kitunguu swaumu kina Selenium na pia kinaondoa sumu mwilini vitu hivi viwili ni mhimu kwa ajili ya kuongeza spidi ya mbegu.

Vile vile Kitunguu swaumu kina ‘Allicin’ ambayo huongeza msukumo wa damu kwenda kwenye uume.

Kujitibu unaweza kuongeza kitunguu swaumu kwenye chakula unachopika. Pia unaweza kutafuna punje 2 au 3 kila unapoenda kulala au unaweza kukatakata hizo punje 3 vipande vidogo vido (chop) kisha unywe na maji.

Usile zaidi ya punje 3 kwa siku.

Matumizi ya Mayai

Mayai yanachukuliwa kama mbadala wa uhakika zaidi katika kuongeza uwingi wa mbegu pamoja na kuongeza spidi au kasi yake. Yana vitamini E nyingi na protini ya kutosha vitu viwili mhimu katika kuongeza mbegu. Tumia mayai ya kienyeji zaidi na sio ya kisasa.

Matumizi ya Spinach

Mboga hii ina Folic asidi ambayo ni mhimu katika kuongezeka kwa mbegu za kiume.

Kula ndizi

Ndizi zina Magnesiamu, Vitamini B1 na Vitamini C, vitu ambavyo ni mhimu sana kwa ajili ya kutengeneza mbegu za kiume. Vile vile Ndizi zina kimeng’enya kimoja adimu sana kijulikanacho kama ‘Bromeliad’ ambacho husaidia kuziweka sawa homoni zinazohusiana na tendo la ndoa.

Matumizi mbegu za maboga

Mbegu za maboga zina kiasi kingi cha madini ya Zinki ambayo ni mhimu katika kuundwa au kutengenezwa kwa mbegu za kiume na homoni ya testosterone.

Vile vile mbegu hizi zina vitamini B, C, D, E, na K ambazo zote ni vitamini mhimu katika kuongeza hamu ya kushiriki tendo la ndoa na nguvu kwa ujumla.

Kula zaidi mboga za majani

Mboga za majani zinapunguza homoni ya ‘estrogen’ na hivyo kufanya homoni ya ‘testosterone’ ipatikane kwa wingi na kiurahisi zaidi na hivyo mbegu zako ziweze kuongezeka bila vipangamizi vyovyote. Homoni hii ndiyo inayohusika na kuzalishwa kwa mbegu

Kunywa maji mengi kila siku

Kutokunywa maji ya kutosha kila siku kuna uhusiano wa moja kwa moja na kupungua kwa uwingi wa mbegu. Mbegu zako zimetengenezwa kwa maji, zipo kwenye hali ya kimiminika.

Kunywa maji ya kutosha kunasaidia kutengenezwa kwa mbegu nyingi.

Kutegemea na uzito wako unaweza kuhitaji maji lita 2 mpaka 3 kila siku.

Tumia vyakula vyenye folic asidi kwa wingi

Vyakula hivi ni pamoja na tunda la parachichi na karoti, mbegu za maboga, ufuta, alizeti, maharage, chungwa, papai, bamia nk

Usisahau kushare makala hii uliyoisoma kuhusu; Njia za kuongeza wingi wa mbegu za kiume. Share Facebook, Twitter bila kusahau WhatsApp.

Makala hii kuhusu, Njia za kuongeza wingi wa mbegu za kiume, imeonekana kupendwa na wasomaji wengi. Makala nyingine zinazopendwa ni kama hizi zifuatazo;

• Mapishi – Mayai Mchanganyiko, Tosti na Soseji, endelea kusoma...

• Mapishi ya Ugali, dagaa (wabichi) na matembele, endelea kusoma...

• Jinsi ya kupika Pilau Ya Samaki WaTuna Na Mboga, endelea kusoma...

• Vitu vinavyoweza kusababisha tatizo la mbegu chache na ugumba kwa ujumla kwa wanaume, endelea kusoma...

• Mambo ya kuzingatia kujikinga na chunusi | Jinsi ya kuzuia, endelea kusoma...

• Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia Mtindi na asali, endelea kusoma...

• Jinsi ya kutibu chunusi za usoni kwa kutumia Parachichi na asali, endelea kusoma...

• Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia maganda ya ndizi, endelea kusoma...

• Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia Uwatu (Fenugreek), endelea kusoma...

• Namna ya kutibu chunusi kwa kutumia Binzari, maziwa na asali, endelea kusoma...

Unaweza kusoma makala mpya nzuri kila unapotembelea website hii wakati wowote. Baada ya kusoma makala hii kuhusu; Njia za kuongeza wingi wa mbegu za kiume, sasa endelea kusoma makala hizi nyingine nzuri nilizokuandalia;

FURSA..! Kuna nafasi za kazi 100.

Au soma zaidi hapa

.

UJUMBE-MSAMAHA-35JHF32.JPG
KADI-TUKUTANE-MZAZI.JPG