VIAMBAUPISHI

Unga - 3 mug za chai

Samli - Β½ mug ya chai

Maziwa - 1ΒΌ mug ya chai

Baking powder - 2 vijiko vya chai

VIAMBAUPISHI VYA MJAZO

Njugu zilizomenywa vipande vipande - 2 vikombe cha chai

Sukari - Β½ kikombe cha chai

Iliki - 1 kijiko cha chai

Nazi iliyokunwa - 2 vikombe vya chai

VIAMBAUPISHI VYA SHIRA

Sukari - 2 vikombe vya chai

Maji - 1 kikombe cha chai

Ndimu - 1

JINSI YA KUVIANDAA

1-Changanya unga na samli kisha tia baking powder na maziwa. Ukande ulainike kisha

uwache kama dakika 5 uumuke.

2-Kwenye bakuli nyingine changanya njugu, sukari na iliki.

3-Kata madonge madogo dogo sukuma kila donge duara jembamba, kisha tia kijiko cha mchanganyiko wa njugu juu yake ifunikie juu yake na ibane pembeni.

4-Panga kwenye treya isiyoganda (non stick) kisha choma kwenye oven kwa moto wa chini

(bake) 350Β° C kwa dakika kama 15-20.

5-Chemsha maji na sukari katika sufuria ndogo kisha tia ndimu acha ichemke mpaka inatenate unapoigusa.

6-Kwenye sahani ya chali mimina nazi iliyokunwa.

7-Vibiskuti vikiwa tayari vya motomoto chovea kwenye shira kisha zungushia katika nazi iliyokunwa,

panga kwenye sahani tayari kwa kuliwa.


ndugu.gif

πŸ™‰πŸ™‰πŸ™‰Usisahau kushare posti hii kuhusu (Namna ya kutengeneza Visheti Vya Nazi Na Njugu (Sudani)).πŸ‘ Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasomeπŸ’―βœ”

🍴 Makala nyingine za Dondoo za Afya & MapishiπŸ‘‡

A.gif

SALAMU-USIKU-23ND.JPG