Mapishi ya Wali Wa Zaafarani Na Kuku Wa Kupaka

Mpendwa Msomaji, baada ya kukuandalia makala inayopendwa kuhusu; Mapishi ya visheti vitamu, sasa nimekuandalia makala hii kuhusu;

Mapishi ya Wali Wa Zaafarani Na Kuku Wa Kupaka.

Unaalikwa pia kusoma kuhusu; Mapishi ya Chapati za maji za vitunguu.

Mapishi ya Wali Wa Zaafarani Na Kuku Wa Kupaka

By, Melkisedeck Shine.

Vipimo

Wali:

Mchele - 3 Vikombe

Kitunguu kiichokatwa - 1

Pilipili boga nyekundu iliyokatwa vipande - 1

Mafuta - ¼ Kikombe

Zaafarani - 1 kijiko cha chai tia kwenye kikombe na maji robo roweka

Chumvi - 1 kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Katika sufuria, tia mafuta, kaanga kitunguu mpaka kiwe kidogo rangu ya udongo (brown)
Tia pili pili boga.
Tia mchele, kaanga kwa muda wa dakika 3, tia zaafarani na chumvi.
Tia supu uliyochemshia kuku iwe imoto.
Pika wali katika moto mdogo hadi uwive.

Kuku

Kuku Mzima -1

Mayai ya kuchemsha - 6

Namna Ya Kupika Kuku

Mchemshe kuku mzima na chumvi mpaka uhakikishe ameiva vizuri.
Mtowe na muweke pembeni. Supu yake tumia katika wali kama ilivyo hapo juuu.
Chemsha mayai, menya na kata vipande viwili kila yai moja weka kando

Vipimo Vya Sosi Ya Kuku Ya Nazi

Kitunguu - 1

Nyanya iliyokatwa vipande - 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi - 1 kijiko cha supu

Garam Masala - ½ kijiko cha supu

Bizari ya manjano - ½ kijiko cha chai

Chumvi - kiasi

Pilipili masala ya unga - ½ kijiko cha chai

Nyanya ya kopo - 1 kijiko cha supu

Nazi ya unga - 1 kikombe

Maji ya ukwaju - ¼ kikombe cha chai

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Tia Mafuta vijiko 2 vya supu katika sufuria
Kaanga kitunguu maji mpaka kiwe rangi ya udongo (brown).
Tia thomu na tangawizi.
Tia nyanya nzima iliyokatwa katwa.
Tia garam masala, manjano, pilipili ya unga, nyanya ya kopo, kaanga vizuri.
Changanya kwenye sufuria na ukwaju. Iache ichemke vizuri.
Changanya nazi ya unga na maji vikombe viwili.
Mtie kuku mpike vizuri na hilo tui.
Mtie kwenye oveni kidogo.

Kupakuwa katika Sinia

Pakuwa wali kwanza katika sinia
Muweke kuku juu ya wali.
Pambia mayai

Usisahau kushare makala hii uliyoisoma kuhusu; Mapishi ya Wali Wa Zaafarani Na Kuku Wa Kupaka. Share Facebook, Twitter bila kusahau WhatsApp.

Makala hii kuhusu, Mapishi ya Wali Wa Zaafarani Na Kuku Wa Kupaka, imeonekana kupendwa na wasomaji wengi. Makala nyingine zinazopendwa ni kama hizi zifuatazo;

• Utayarishaji bora wa chakula, endelea kusoma...

• Jinsi ya kutengeneza Biskuti Za Tende Na Ufuta, endelea kusoma...

• Njia bora za kumfanya mtu aache kuvuta sigara, endelea kusoma...

• Mapishi ya wali mtamu Wa Nazi Kwa Maharage Na Samaki Nguru Wa Kukaanga, endelea kusoma...

• Mapishi mazuri ya Wali Wa Kukaanga Kwa Kidari Cha Kuku, endelea kusoma...

• Jinsi ya kupika vizuri Wali Wa Karoti Na Nyama, endelea kusoma...

• Mapishi ya Pilau Ya Nafaka Na Nyama Ya Kusaga, endelea kusoma...

• Mapishi ya Pilau Ya Samaki Wa Tuna Na Mboga, endelea kusoma...

• Jinsi ya kupika wali wa Tuna (samaki/jodari), endelea kusoma...

• Jinsi ya kutengeneza Rock-cakes Za Njugu Na Matunda Makavu, endelea kusoma...

Unaweza kusoma makala mpya nzuri kila unapotembelea website hii wakati wowote. Baada ya kusoma makala hii kuhusu; Mapishi ya Wali Wa Zaafarani Na Kuku Wa Kupaka, sasa endelea kusoma makala hizi nyingine nzuri nilizokuandalia;

FURSA..! Kuna nafasi za kazi 100.

Au soma zaidi hapa

.

MLO-MWEMA-KWA-NDUGU-UJUMBE.JPG
UJUMBE-UNAVYOMMISI-NDUGU.JPG