Mapishi ya Wali Wa Tambi Na Kuku Wa Sosi Ya Mtindi

By, Melkisedeck Shine.

familia-mapenzi-na-mahusiano.png

Mapishi ya Wali Wa Tambi Na Kuku Wa Sosi Ya Mtindi

Vipimo Vya Wali

Mchele - 3 vikombe

Tambi - 2 vikombe

Mafuta - ¼ kikombe

Chumvi

Vipimo Vya Kuku

Kuku kidari (boneless) aliyekatwa katwa vipande - 1 Kilo

Kitunguu maji kilichokatwa katwa - 2

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa - 1 kijiko cha supu

Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 kijiko cha chai

Chumvi - kiasi

Paprika - 1 kijiko cha supu

Masala ya kuku (tanduri au yoyote) - 1 kijiko cha supu

Ndimu - 2 vijiko vya supu

Mtindi (yoghurt) au malai (cream) - 1 kikombe

Mafuta - ¼ kikombe

Majani ya kotmiri (coriander) - ½ kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Wali:

Osha Mchele, uroweke.
Tia mafuta katika sufuria, kaanga tambi zilizokatwakatwa hadi zigeuke rangi kuwa nyekundu.
Tia mchele endelea kukaanga kidogo.
Tia maji kiasi cha wali kupikika kama unavyopika pilau. Kiasi cha maji kinategemea aina ya mchele
Funika katika moto mdogo mdogo hadi uive ukiwa tayari.

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Kuku

Katika bakuli, changanya vitu vyote isipokuwa mtindi na kitunguu.
Tia mafuta katika karai, kisha tia kitunguu ukaange muda mdogo tu, usikiache kugeuka rangi.
Tia kuku na masala yake, endelea kukaanga, kisha tia mtindi au malai ufunike apikike na kuiva vizuri.
Nyunyuzia kotmiri iliyokatwakatwa ikiwa tayari kuliwa na wali wa tambi.


uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Mapishi ya Wali Wa Tambi Na Kuku Wa Sosi Ya Mtindi;

a.gif Jinsi ya kupika Pilau ya Nyama ya Kusaga Na Mboga Mchanganyiko

Mchele - 2 Mugs.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Biriani Ya Samaki Nguru, Njegere Na Snuwbar (UAE)

Mchele wa basmati - 4 cups.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Biriani Ya Kuku Wa Kuchoma (Grilled)

Mchele wa Basmati /Pishori - 4 vikombe.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kuandaa Wali Wa Hudhurungi Na Kabeji

Mchele wa hudhurungi (brown rice).. endelea kusoma

[Kitendawili Kwako] 👉'Kitanga' amefunika watoto wake

afya-mapishi-na-lishe.png

a.gif Mapishi ya Kuku wa kukaanga

Miguu ya kuku (chicken legs) 10
Kitunguu swaum na tangawizi (ginger & garlic paste) 1 kijiko cha chakula
Limao (lemon) 1
Pilipili iliyosagwa (ground scotch bonnet) 1/2
Giligilani iliyokatwakatwa (chopped coriander) kiasi
Chumvi (salt) kiasi
Mafuta ya kukaangia (veg oil).. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya viazi mbatata Vya Nazi Kwa Nyama Ya Ng'ombe

Mbatata / viazi - 2 kilo.. endelea kusoma

a.gif Lifahamu tatizo la maumivu chini ya kitovu

Tatizo hili huwakumba watu wengi sana kwenye jamii yetu lakini kwa bahati mbaya watu wengi huchukulia ni jambo la kawaida kitu ambacho baadae hupelekea watu wengi kuingia kwenye matatizo makubwa ya kiafya hasa kwenye mfumo wa uzazi na mfumo wa chakula… endelea kusoma

a.gif Faida za matumizi ya Ukwaju kiafya

Faida kuu za ukwaju ni kama ifuatavyo:.. endelea kusoma

[Hadithi Nzuri] 👉Stori inayogusa!!

[SMS kwa Umpendaye] 👉SMS nzuri sana ya kutakia usiku mwema

vichekesho-bomba-vya-siku.png

.

uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png
UJUMBE-HONGERA-NDUGUU.JPG
familia-mapenzi-na-mahusiano.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.