Mapishi ya wali Wa Nazi Kwa Mchuzi Wa Nyama Ng’ombe Na Mchicha

By, Melkisedeck Shine.

familia-mapenzi-na-mahusiano.png

Mapishi ya wali Wa Nazi Kwa Mchuzi Wa Nyama Ng’ombe Na Mchicha

Wali Wa Mpunga

Mchele wa mpunga - 4 Vikombe

Tui la nazi - 6 vikombe

Chumvi - kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Osha mchele kisha

Bandika tui jikoni likichemka tia mchele na chumvi.

Funika uchemke, tui likikauka wacha moto mdogomdogo hadi wali uive ukiwa tayari. Ikiwa unatumia mkaa unapalia juu yake.

Mchuzi wa nyama Ng’ombe

Nyama - 1 kilo

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi ilosagwa -2 viijiko vya supu

Viazi/mbatata - 2

Kitunguu maji kilokatwakawa (slice ndogo) - 2

Nyanya/tungule - 4

Nyanya kopo - 3 vijiko vya supu

Majani ya mchuzi/mvu - 3 msongo (bunches)

Bizari ya mchuzi (simba 2) - I kijiko cha chai

Ndimu - 1 kamua

Mafuta - ¼ kikombe

Chumvi - kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Weka nyama katika sufuri, tia kijiko kimoja cha kitunguu thomu na tangawizi, chumvi, ndimu na chemsha nyama hadi iwive na ibakie supu yake kidogo.
Weka mafuta katika sufuri nyingine, kaanga kitunguu. Vinapogeuka rangi tia majani ya mchuzi endelea kukaanga hadi vigeuke rangi ya hudhurungi (golden brown)
Tia nyanya/tungule, viazi/mbatata, endelea kukaanga mpaka nyanya ziive.
Tia nyama na supu yake kisha tia nyanya ya kopo, kotmiri, bizari ya mchuzi, chumvi uache mchuzi kidogo katika moto hadi viazi viive vikiwa tayari.

Mboga Mchicha

Mchicha - 4 michano/vifungu

Kitunguu - 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) - 3

Nyanya/tungule - 2

Tui la nazi zito - 1 kikombe cha chai

Chumvi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Osha mboga iache ichuje maji.
Ikatekate kisha weka katika sufuria.
Katika kitunguu maji, kitunguu thomu kisage au kikatekate kidogodogo (chopped), nyanya.
Weka jikoni ipikike kwa maji yake na mvuke.
Tia tui endelea kuweka katika moto mdogomdogo hadi ikaribie kukauka ikiwa tayari.


Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Mapishi ya wali Wa Nazi Kwa Mchuzi Wa Nyama Ng’ombe Na Mchicha;

a.gif Mapishi ya Pilau Ya Mchicha

Mchele - 3 Vikombe.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Wali, Mchuzi Wa Nazi Wa Samaki Nguru

Mchele - 3 vikombe.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Wali Wa Mboga Na Samaki Wa Pink Salmon

Mchele 3 vikombe.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Pilau Ya Nyama Na Mtindi

Nyama iliyokatwa vipande - 1 Ratili(LB).. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kutibu tatizo la kukosa choo bila kutumia dawa

Kukosa choo ni tatizo kubwa katika jamii zetu japo huwa halionekani kama ni tatizo. Hata hivyo kuna vyakula ambavyo vinapatikana kwa urahisi na vinasaidia kutibu tatizo la kukosa choo kwa njia rahisi kabisa… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia limau au limao

Dawa nyingine nzuri kwa ajili ya chunusi usoni na mwilini ni limau. Limau linajitokeza kwenye vyakula vingi tunavyokula kila siku mathalani limau halikosekani pakiwepo supu au mapishi yoyote ya samaki… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kufanya kupunguza mwili kwa kupanga ulaji wa chakula

Ulaji wa vyakula vingi vya wanga na mafuta ni chanzo kikubwa cha unene na uzito kuongezeka. Vyakula kama ugali,wali,mkate mweupe,bia na pombe za kienyeji zinazotokana na wanga (kimea) huchangia kuongezeka kwa uzito. Matumizi ya aina hii ya chakula ni muhimu kupunguzwa katika mlo wako… endelea kusoma

a.gif Hizi ndizo faida za kiafya za kuota jua

Kuna mambo ambayo huwa tunayachukulia ya kawaida na wala hatuko tayari kufahamu umuhimu wake. Jua ni kitu mojawapo ambacho huwa tunakiona kila siku, lakini ni mara chache tumelichunguza… endelea kusoma

vichekesho-bomba-vya-siku.png

.

picha-kali.png
KADI-PONGEZI-MZAZI.JPG
vichekesho-bomba-vya-siku.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.