Mapishi ya Wali Wa Mboga Na Samaki Wa Pink Salmon

By, Melkisedeck Shine.

elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

Mapishi ya Wali Wa Mboga Na Samaki Wa Pink Salmon

Vipimo

Mchele 3 vikombe

Mboga mchanganyiko 1 kikombe

Samaki wa Pink Salmon 5 -6 vipande

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa 1 kijiko cha supu

Chumvi kiasi

Pilipili manga ya unga ½ kijiko cha chai

Pilipili nyekundu ya unga ½ kijiko cha chai

Ndimu zilokamuliwa 2

Parsley kavu (aina ya kotmiri) 2 vijiko vya supu

Bizari ya mchuzi 1 kijiko cha supu

Kidonge cha supu (stock) 2

Mafuta ¼ kikombe

Maji ½ kikombe

Namna ya Kutayarisha Na Kupika

Samaki:

Katika kibakuli kidogo, changanya; kitunguu thomu, tangawizi, chumvi, pilipili zote za unga, ndimu, parsely, bizari ya mchuzi na mafuta vijiko viwili vya supu.

Pakaza kwenye samaki.

Weka vipande vya samaki katika treya ya oveni kisha uchome (grill) huku ukigeuza hadi samaki awive. Epua weka kando.

Wali:

Osha mchele roweka kisha uchemshe uive nusu kiini

Mwaga maji uchuje mchele

Weka mafuta katika sufura, tia mboga mchanganyiko kakaanga kidogo

Weka vidonge vya supu, tia maji ½ kikombe, tia chumvi kiasi

Mimina mchele uchanganye vizuri, kisha funika hadi uive wali ukiwa tayari

Pakua katika sahani pamoja na samaki


Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Mapishi ya Wali Wa Mboga Na Samaki Wa Pink Salmon;

a.gif Mapishi ya wali Wa Nazi Kwa Mchuzi Wa Nyama Ng’ombe Na Mchicha

Mchele wa mpunga - 4 Vikombe.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Pilau Ya Mchicha

Mchele - 3 Vikombe.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Pilau Ya Nyama Na Mtindi

Nyama iliyokatwa vipande - 1 Ratili(LB).. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Ugali Kwa Mchuzi Wa Nyama, Mchicha, Maharage Na Chatini Ya Pilipili Mbichi

Nyama ya ng’ombe vipande vidogo - 2lb.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika Baklawa Za Pistachio Na Lozi

Philo (thin pastry) manda nyembamba - 1 paketi.. endelea kusoma

a.gif Kampeni ya usafi na Utunzaji wa mazingira

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.
Lengo la kampeni Hii ni kuhamasisha watu kusafisha na kutunza mazingira yao kwa manufaa yao ya sasa na kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Kampeni hii inaamini kuwa mazingira yakisafishwa na kutunzwa vizuri yanaweza kuwa msaada kijamii, kiuchumi na kiafya kwa kizazi hiki na kizazi kijacho… endelea kusoma

a.gif Madhara ya kunywa maji baridi na faida za kunywa maji moto na asali

UNYWAJI wa maji baridi, hasa katika joto kali kama la Dar es Salaam, ni kiburudisho kikubwa cha koo na huleta faraja kubwa mwilini. Ni jambo la kawaida pia kwa mtu kuhitaji kunywa maji hayo mara baada ya kula mlo, iwe mchana au usiku… endelea kusoma

a.gif Faida za Korosho Kiafya

Korosho zina faida hizi zifuatazo;.. endelea kusoma

elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

.

afya-mapishi-na-lishe.png
MPENZI-MLO-MWEMA-34NG.JPG
familia-mapenzi-na-mahusiano.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.