Mapishi ya Wali Wa Mboga Na Mchuzi Wa Kuku wa Tanduri

By, Melkisedeck Shine.

Vipimo vya Wali:

Mchele basmati - 3 magi (kikombe kikubwa)

Mchanganyiko wa mboga za barafu

(Frozen vegetables) - 1 ½ mug

Chumvi - kiasi

Mafuta - 3 vijiko vya chakula

Kitungu maji (kilichokatwa) - 1

Bizari ya pilau (nzima) - 1 kijiko cha chakula

Namna Ya kutayarisha na kupika:

Osha mchele uroweke kwenye maji muda wa dakika 20.
Chemsha maji kwenye sufuria kama magi 6.
Tia chumvi.
Yakisha kuchemka unatia mchele, chemsha usiive sana, uive nusu kiini. Mwaga maji na kuchuja wali.
Unamimina Yale mafuta kwenye sufuria unakaanga bizari ya pilau kidogo na kitunguu kabla ya kugeuka rangi ya hudhurungi (brown).
Tia mchanganyiko wa mboga za barafu.,
Mimina wali, changanya vizuri, ufunike na uweke katika moto mdogo kwa dakika 20.
Pakua tayari kwa kuliwa.

Vipimo Vya Mchuzi

Kuku - 2 Ratili (LB)

Chumvi - Kiasi

Mafuta - ¼ Kikombe

Nyanya Kata vipande - 4

Nyanya kopo - 2 vijiko wa chakula

Tangawizi - 1 kijiko ya chakula

Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 kijiko ya chakula

Tanduri masala - 1 kijiko cha chakula

Kotmiri liliyokatwa - 3 vijiko vya chakula

Pilipili mbichi - 2

Pili masala - 1 kijiko cha chakula

Garam masala - ½ kijiko cha chakula

Bizari manjano - ½ kijiko cha chakula

Mtindi - 3 vijiko vya chakula

Pilipili boga (kata vipande virefu) - 1

Ndimu - 2 vijiko vya chakula

Namna ya kutayarisha na kupika:

Kwenye bakuli tia kuku na changanya vitu vyote pamoja isipokua mafuta.
Tia mafuta kwenye sufuria yakisha kupata moto mimina kuku umpike kwa muda ½ saa kwa moto kiasi.
Pakua kuku kwenye bakuli au sahani na ukate vitunguu maji duara na umpambie. Tayari kwa kuliwa.


kj.gif

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Mapishi ya Wali Wa Mboga Na Mchuzi Wa Kuku wa Tanduri;

a.gif Jinsi ya kutengeneza Pilau Ya Kuku

Mchele wa basmati - 3 vikombe.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Wali Wa Nazi Kwa Mchuzi Wa Samaki Na Rojo La Bilingani Na Viazi/Mbatata

Mpunga - 4 vikombe.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Wali, Mchuzi Wa Nazi Wa Samaki Nguru

Mchele - 3 vikombe.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Pilau Ya Mchicha

Mchele - 3 Vikombe.. endelea kusoma

[Kitendawili Kwako] 👉Huenda nimepanda hurudi nimepanda

[Video Nzuri] 👉Utaalamu wa kufunga tai

MPENZI-MLO-MWEMA-34NG.JPG

a.gif Mapishi ya Ugali Mchuzi Wa Samaki Nguru Wa Nazi Na Bamia Za Kukaanga

Unga wa mahindi/sembe - 4.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Pasta za cream na uyoga

Pasta (2 na 1/2 vikombe vya chai)
Uyoga (mashroom 2 vikombe vya chai)
Cream (1 kikombe cha chai)
Mafuta (vegetable oil)
Kitunguu (onion 1)
Chumvi
Majani ya basil (dried basil leaves 1/2 kijiko cha chai).. endelea kusoma

a.gif MAANA YA MANENO YANAYOTUMIKA KATIKA MASUALA YA LISHE

ni kitu chochote kinacholiwa au kunywewa na kuupatia mwili virutubishi mbalimbali Chakula huupatia mwili nguvu, kuulinda na kuukinga dhidi ya maradhi mbalimbali .Mfano wa chakula ni ugali, wali, maharagwe, ndizi, viazi, mchicha, nyama, samaki… endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Half cake (Keki)

Unga wa ngano (self risen flour) kikombe 1na 1/2
Sukari (sugar) 1/4 kikombe
Barking powder 1/2 kijiko cha chai
Magadi soda (bicarbonate soda) 1 kijiko cha chai
Mafuta 2 vijiko vya chai
Mafuta ya kukaangia
Maji ya uvuguvugu kiasi.. endelea kusoma

[Msemo wa Leo] 👉Chema na kizuri

[Jarida la Bure] 👉Jinsi ya kupika Biskuti za tende

[Hadithi Nzuri] 👉Stori inayogusa!!

[SMS kwa Umpendaye] 👉Ujumbe wa kimahaba kwa mpenzi wako

FURSA..! Kuna nafasi za kazi 100.

Au soma zaidi hapa

.

UJUMBE-POLE-NDUGU.JPG
tafuta-rafiki.gif

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.