Mapishi ya Wali Wa Karoti Na Kuku Wa Kukaanga

By, Melkisedeck Shine.

uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png

Mapishi ya Wali Wa Karoti Na Kuku Wa Kukaanga

Vipimo Vya Wali

Mchele wa Basmati/Pishori - 1 kilo moja

Vitunguu maji - 3

Karoti - 2

Siagi - 3 vijiko vya supu

Kidonge cha supu (stock) - 1 kimoja

Chumvi - kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Ósha mchele uroweke kama saa moja au mbili
Katakata vitunguu vipande vidogodogo (chopped) weka kando.
Kwaruza karoti (grate) weka kando.
Tia siagi katika sufuria ya kupikia wali, weka katika moto iyayuke
Kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi kiasi tu.
Tia maji kiasi ya kupikia wali, changanya na kidonge cha supu.
Yakichemka tia mchele, koroga, funika uweke moto mdogo mdogo.
Kabla ya maji kukauka tia karoti changanya wali kisha funika uive kama unavyopika pilau.

Vipimo Vya Kuku Wa Kukaanga

Kuku alokatwakatwa - 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi ilosagwa - 2 vijiko vya supu

Bizari ya mchanganyiko/garam masala - kijiko cha supu

Mtindi/Yoghurt - 1 kijiko cha supu

Ndimu - 1

Chumvi - kiasi

Mafuta ya kukaangia - kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Ukishamuosha kuku, mchuje atoke maji yote.
Changanya viungo vyote katika kibakuli kidogo.
Changanya pamoja na kuku kisha acha akolee viungo (marinate) kwa muda wa masaa mawili takriban.
Weka mafuta katika karai na kaanga kuku, akiwiva yu tayari kuliwa na wali.


Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Mapishi ya Wali Wa Karoti Na Kuku Wa Kukaanga;

a.gif Mapishi ya Ndizi Za Supu Ya Nyama Ya Ng’ombe

Ndizi - 15 takriiban.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Wali Wa Kukaanga Kwa Nyama Mbuzi Ilichomwa Ya Sosi Ya Ukwaju

Mchele Basmati - 4 vikombe.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Wali Wa Nazi Wa Adesi, Bamia Na Mchuzi Wa Kamba

Mchele - 2 vikombe.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika Pilau ya Mpunga Na Nyama Ya Ng’ombe

Mpunga - 4 vikombe.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Pilau Ya Nyama ya Kusaga, Adesi Za Brauni Na Zabibu

Mchele wa Par boiled au basmati - 5 vikombe.. endelea kusoma

a.gif Aina ya vyakula vinavyotakiwa kwa wajawazito

Kwa ajili afya ya mama na mtoto ni muhimu sana, mwanamke anatakiwa apate chakula bora kilicho na madini yote kama vitamini na protini. Mama mjamzito anatakiwa apate gramu 100 za protini kila siku. Ifuatayo ni mlo kamili anaotakiwa apate mama mjamzito kila siku ya ujauzito wake kwa afya bora… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya Dengu (Dengue fever)

Ugonjwa wa dengue ni tishio la ugonjwa hatari linaongezeka siku hadi siku. Dengue ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyoenezwa na mbu aitwae aedes… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kutibu chunusi kwa Chumvi na mafuta ya zeituni

Mchanganyiko wa chumvi na mafuta ya zeituni (olive oil) ni dawa nyingine inayotibu chunusi. Mafuta ya zeituni yandhibiti bakteria na huondoa sumu vitu ambavyo vinafanya kuwa dawa nzuri kutibu chunusi na matokeo ya chunusi… endelea kusoma

uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png

.

afya-mapishi-na-lishe.png
rafiki.gif
uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.