Mapishi ya Wali Mweupe Kwa Mchuzi Wa Kuku Wa Balti

By, Melkisedeck Shine.

afya-mapishi-na-lishe.png

Mapishi ya Wali Mweupe Kwa Mchuzi Wa Kuku Wa Balti

Vipimo

Kuku 1 mkate vipande vipande

Vitunguu 3 katakata (chopped)

Nyanya 5 zikatekate (chopped)

Tangawizi mbichi ilokunwa au ilosagwa 1 kijiko cha kulia

Thomu (kitunguu saumu) kilosagwa kijiko 1 cha kulia

Bizari mchanganyiko (garam masala) kijiko 1 cha chai

Jira/bizari ya pilau (cummin powder) kijiko 1 cha chai

Dania/gilgilani ilosagwa (coriander powder) kijiko 1 cha chai

Mtindi/maziwa lala (yoghurt) vijiko vya kulia 4 mjazo au paketi moja ndogo.

Malai ya kupikia (cooking cream) kikombe 1

Kasuri methi (majani makavu ya uwatu/dried fenugreek leaves) 1 kijiko cha kulia

Mafuta ya kupikia ½ kikombe

Chumvi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Osha kuku vizuri mwache achuje maji.
Weka mafuta katika sufuria kaanga vitunguu mpaka vianze kugeuka rangi ya brown hafifu. Kisha tia tangawizi na thomu ukaange.
Tia kuku ukaange mpaka ageuke mweupe kisha tia nyanya endelea kukaanga ziwive.
Piga mtindi vizuri katika kibakuli uwe nyororo.
Epua sufuria weka kando kisha tia mtindi uchanganye vizuri pamoja na kuku.
Rudisha katika moto acha uchanganyike na kuku kidogo kisha mwagia malai ya kupikia (cooking cream)
Tia kasuri methi/majani makavu ya uwatu yaliyovurugwa. Acha katika moto dakika 1 tu.
Epua umimine katika chombo na nyunyizia ikiwa tayari kuliwa na wali mweupe.


Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Mapishi ya Wali Mweupe Kwa Mchuzi Wa Kuku Wa Balti;

a.gif Jinsi ya kupika Magimbi Kwa Nyama Ya Ng’ombe

Majimbi (Eddoes) kiasi 6 au 7.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Boga La Nazi

Boga la kiasi - nusu yake.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Ugali Mchuzi Wa Samaki Nguru Wa Nazi Na Bamia Za Kukaanga

Unga wa mahindi/sembe - 4.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Biriani Nyepesi Kupika Ya Samaki

Mchele wa pishori (basmati) - 4.. endelea kusoma

a.gif Dondoo muhimu za afya

Tafadhali soma na uwapelekee wengine… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kutengeneza Pilau Ya Kuku

Mchele wa basmati - 3 vikombe.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika Pilau Ya Samaki WaTuna Na Mboga

Mchele 2 Mugs.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika Biskuti Za Tende Na Ufuta

Unga 3 Vikombe vya chai.. endelea kusoma

afya-mapishi-na-lishe.png

.

vichekesho-bomba-vya-siku.png
tafuta-ndugu.gif
familia-mapenzi-na-mahusiano.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.