VIAMBAUPISHI

Unga - Vikombe 2

Samli au shortening ya mboga - 2 Vijiko vya supu

Maziwa ΒΎ Kikombe

Iliki - Kiasi

Mafuta ya kukarangia Kiasi

VIAMBAUPISHI :SHIRA

Sukari - 1 Kikombe

Maji ΒΎ Kikombe

Vanila Β½ Kijiko cha chai

Zafarani (ukipenda) - Kiasi

JINSI YA KUPIKA

Katika kisufuria pasha moto maziwa na wakati huo huo chemsha Samli katika kisufuria kengine.
Tia unga katika bakuli na iliki, kisha mimina samli iliyochemka na huku unachanganya.
Tia maziwa na uwendele kuchanganya vizuri isiwe na madonge, ikiwa maziwa haitoshi ongeza maji kidogo.
Kisha uwache unga ukae mahali pa joto kwa muda wa dakika 10 hivi.
Halafu fanya viduara vidogo vidogo, kisha finyiza kwenye greta yenye vishimo vidogo ili upate umbo lake.
Kisha karanga kwenye mafuta yaliyopata moto hadi vibadilike rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta.
Chemsha shira, ikiwa tayari mimina visheti na upepete na kuzichanganya zipate shira kote.
Weka kwenye sahani na zitakuwa tayari kwa kuliwa na kahawa.


Marafiki-wa-enzi.GIF

πŸ™‰πŸ™‰πŸ™‰Usisahau kushare posti hii kuhusu (Mapishi ya visheti vitamu).πŸ‘ Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasomeπŸ’―βœ”

🍴 Makala nyingine za Dondoo za Afya & MapishiπŸ‘‡

A.gif

mtu.gif