Mapishi ya Viazi, samaki na asparagus

By, Melkisedeck Shine.

Mahitaji

Viazi (potato 1/2 kilo)
Samaki (fish 2)
Asparagus 8
Kitunguu kilichokatwa (chopped onion 1)
Kitunguu swaum kilichosagwa (garlic 4 cloves)
Tangawizi iliyosagwa kiasi (ginger paste)
Limao (lemon 1)
Giligilani iliyokatwakatwa (chopped coriander)
Curry powder (kijiko 1 cha chai)
Chumvi (salt)
Mafuta (vegetable oil)

Matayarisho

Safisha samaki na kisha uwamarinate na kitunguu swaum, tangawizi, limao na chumvi kwa muda wa nusu saa. Baada ya hapo wakaange na usiwakaushe sana kisha waweke pembeni. Chukua fry-pan kisha tia mafuta kidogo sana (kama 1/2 kijiko cha chai) kisha tia vitunguu maji na uvikaange kwa muda wa dakika 2 (kwani havitakiwi kuiva kabisa) kisha waweke samaki na uwachanganye na hivyo vitunguu. Kisha baada ya hapo tia giligilani iliyokatwa, kamulia limao na tia chumvi kidogo kisha geuzageuza ili kuchanganya vitu vyote na kisha ipua. Baada ya hapo menya na ukate viazi katika vipande vya wastani, na kisha uvichemshe kidogo na visiive kabisa. Baada ya hapo weka sufuria jikoni kwenye moto wa wastani na utie mafuta kidogo (kama vijiko 2 vya chakula) na kisha tia viazi na uanze kuvipika kwa kuvigeuzageuza mpaka viive na kuwa rangi ya brown kisha tia chumvi kidogo, curry powder na giligilani iliyokatwa.Vipike kwa muda wa dakika mbili kisha viipue. Na baada ya hapo malizia kwa kupika asparagus. Kwanza zioshe kisha zikate kati. Baada ya hapo weka mafuta kidogo kama 1/2 kijiko katika fry-pan yakisha pata moto tia kitunguu swaum, asparagus na chumvi.Zipike kwa kuzigeuzageuza kwa muda wa dakika 5 na hapo zitakuwa zimeshaiva na tayari kwa kuliwa pamoja na samaki na viazi. Unaweza kuvisevu kwa ketchup.


MPENZI-MLO-MWEMA-34NG.JPG

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Mapishi ya Viazi, samaki na asparagus;

a.gif Mapishi ya Wali maharage,mchuzi wa samaki na spinach

Mchele (rice 1/2 kilo)
Maharage yaliyochemshwa (boiled red kidney beans 1 kikombe cha chai)
Samaki waliokaangwa ( 2 fried fish)
Nyanya ya kopo (tin tomato 1/2 ya tin)
Vitunguu vilivyokatwa (onion 2)
Kitunguu swaum (garlic 3 cloves)
Tangawizi (ginger kiasi)
Limao (lemon 1/2)
Chumvi (salt)
Pilipili (scotch bonnet pepper 2)
Mafuta (vegetable oil)
Spinach
Tui la nazi (coconut milk 1 kikombe cha chai).. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Wali, mchicha wa nazi na nyama ya kukaanga

Mchele (rice 1/2 kilo)
Mchicha uliokatwakatwa (spinach mafungu 2)
Nyama (beef 1/2 ya kilo)
Nyanya (tin tomato 1/2 ya tin)
Nyanya chungu ( garden egg 3)
Kitunguu swaum (garlic cloves 3)
Tangawizi (ginger)
Curry powder
Vitunguu (onion 2)
Limao (lemon 1)
Chumvi
Pilipili (scotch bonnet pepper )
Tui la nazi (coconut milk 1 kikombe cha chai).. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Pilau ya nyama ya ng'ombe na kachumbari

Mchele (rice vikombe 3)
Nyama ya ng'ombe (beef 1/2 kilo)
Viazi mbatata (potato 3)
Vitunguu maji (onions 3)
Kitunguu swaum (garlic cloves 4)
Tangawizi iliyosagwa (ginger kiasi)
Hiliki nzima (cardamon 4)
Karafuu (clove 4)
Pilipili mtama (blackpepper 4)
Amdalasini (cirnamon stick 1)
Binzari nyembamba nzima(cumin seeds 1/2 ya kijiko cha chai)
Binzari nyembamba ya kusaga (ground cumin 1 kijiko cha chai)
Chumvi (salt)
Mafuta (vegetable oil)
Nyanya (fresh tomato 3)
Limao (lemon 1)
Pilipili (chilli 1)
Hoho (green pepper).. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Ndizi na samaki

Ndizi laini (Matoke 6)
Viazi mbatata (potato 3)
Samaki wabichi wa wastani ( Fresh tilapia 2)
Kitunguu swaum (garlic 6 cloves)
Tangawizi (fresh ground ginger vijiko 2 vya chai)
Nyanya ya kopo (tin tomato 1/2 kopo)
Vitunguu (onion 1)
Pilipili (chilli 1 nzima)
Chumvi (salt to your taste)
Mafuta (vegetable oil)
Limao (lemon 1/2)
Curry powder (1/2 kijiko cha chai).. endelea kusoma

[Kitendawili Kwako] 👉Ng'ombe wa miguu minane

ml.gif

a.gif Bisikuti Za Kokoa (Cocoa Biscuits)

Siagi 100gm.. endelea kusoma

a.gif Faida za kula Karoti kiafya

Asilimia kubwa tunapenda kutumia karoti katika kuunga katika mboga ya nyama na si kuila karoti kama karoti. wataalamu wanashauri ili uwe na afya bora unatakiwa ule karoti sita kwa wiki au moja kwa siku. Unaweza kula karoti ya kuchemshaa,juisi au mbichi… endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Pilau Ya Kuku Kwa Mchele Mpya

Mchele - 1 kilo.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Biriani Ya Kuku Wa Kuchoma Wa Tanduri

Mchele - 4 vikombe.. endelea kusoma

[Msemo wa Leo] 👉Mke Na Mme Kusaidiana

[Jarida la Bure] 👉Jinsi ya kupika Biskuti za tende

FURSA..! Kuna nafasi za kazi 100.

Au soma zaidi hapa

.

KADI-SHUKRANI-MZAZI.JPG
Marafiki-wa-enzi.GIF

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.