Mapishi ya Ugali Kwa Mchuzi Wa Nazi Wa Nyanya Chungu/Mshumaa/Ngogwe Na Bamia, Mboga Ya Matembele Na Samaki Wa Kukaanga

By, Melkisedeck Shine.

vichekesho-bomba-vya-siku.png

Mapishi ya Ugali Kwa Mchuzi Wa Nazi Wa Nyanya Chungu/Mshumaa/Ngogwe Na Bamia, Mboga Ya Matembele Na Samaki Wa Kukaanga

Vipimo Vya Ugali

Unga wa mahindi - 4

Maji - 6 kiasi kutegemea na aina ya unga

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Weka maji katika moto.

Tia unga kidogo katika kibakuli, koroga ufanye uji.

Maji yakichemka tia kwenye maji uwe uji.

Ujii ikiiva punguza kidogo tia unga kidogokidogo na usonge ugali. Ikiwa unga ni mgumu utaongeza maji ya ule uji ulopunguza usonge hadi uive ukiwa tayari.

Vipimo Vya Mchuzi Wa Nazi Kwa Nyanya Chungu/Mshumaa/Ngogwe Na Bamia

Nyanya chungu/mshumaa/Ngogwe - 7

Bamia - 10

Kitunguu maji - 2

Nyanya/tungule - 2

Tui la nazi jepesi - 2 viwili

Tui la nazi zito - 2

Chumvi - kiasi

Ndimu - 2 mbili kamua

Bizari manjano/haldi/turmeric - ½ kijiko cha chai

Pilipili mbuzi - 3

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Katakata kitunguu maji na nyanya vipande vidogodogo sana kisha weka katika sufuria.

Iache ichemke kwa maji yake ya nyanya, ikishachemka tia maji kidogo kama robo kikombe.

Tia nyanya chungu, bamia na koleza ndimu, chumvi.

Iache ichemke. Inapokuwa tayari imeiva tia tui jepesi endelea kuacha katika moto huku unakoroga kidogo kidogo.

Tui jepesi likipungua kiasi chake, tia tui zito, kisha usiachie mkono koroga ikichemka kidog kiasi cha kuiva tui mchuzi tayari.

Vipimo Vya Mboga Ya Matembele

Matembele - 5 mafungu

Mafuta - ¼ kikombe

Kitunguu maji kilokatwakatwa - 1

Nyanya/tungule - 4

Chumvi - 1

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Punguza miche ya matembele kwa kuikata ncha kisha osha majani yake. Acha yachuje maji .
Weka mafuta katika sufuria, kaanga kitunguu maji na nyanya hadi viivie.
Tia mboga, Iache ichemke kwa maji yake hadi iive. Ukiona bado haikuiva tia maji kidogo tu.
Ukipenda unatia ndimu kiasi cha kipande kimoja ukamue .

Samaki Wa Nguru Wa Kukaanga

Samaki Wa Nguru - 4 vipande

Kitunguu saumu(thom/galic) na tangawizi ilosagwa - 1 kijiko cha supu

Pilipili mbichi - 4

Ndimu - 2 kamua

Bizari ya samaki - 1 kijiko cha chai

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Mwoshe samaki kisha mtie kitunguu thomu, tangawizi ilosagwa, chumvi, pilipilimbichi ilosagwa, ndimu na bizari ya samaki.
Mwache akolee viungo kwa muda kidogo.
Makaange katika mafuta hadi aive akiwa tayari.


Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Mapishi ya Ugali Kwa Mchuzi Wa Nazi Wa Nyanya Chungu/Mshumaa/Ngogwe Na Bamia, Mboga Ya Matembele Na Samaki Wa Kukaanga;

a.gif Mapishi ya Biriani Ya Tuna

Mchele Basmati - Mugs 2 ½.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Biriyani Ya Kuku

Mrowanishe kuku na viungo hivi kwa muda mdogo tu.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kutengeneza Biriani Ya Nyama Ya Ng'ombe

Nyama - 2 Ratili (LB).. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Pilau Ya Adesi Za Brown Karoti Na Mchicha Kwa Samaki Wa Salmon

Mchele vikombe 3.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kuandaa Ndizi Mbichi Za Supu Ya Nyama Ng’ombe

Ndizi mbichi - Kisia.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika Pilau Ya Nyama Ya Ng'ombe Na Nyanya

Mchele (Basmati) 3 vikombe

Nyama ya ngo’mbe 1 kg

Pilipili boga 1 kubwa

Nyanya 2 kubwa

Vitunguu maji 2 vikubwa

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa 1 kijiko cha supu

Tangawizi 1 kijiko cha chai

Ndimu 1

Mafuta ya kupikia ½ kikombe

Mdalasini ½ kijiko cha chai

Binzari nyembamba 1 kijiko cha chai

Pilipili manga ½ Kijiko cha chai

Hiliki ½ Kijiko cha chai.. endelea kusoma

a.gif Mapishi – Saladi ya Matunda

Matunda ni mojawapo wa kundi la vyakula, ni muhimu sana kwa afya bora. Matunda yakitengenezwa vizuri yanavutia sana na yanakuwa ni chakula kizuri sana… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika Biskuti Za Tende Na Ufuta

Unga 3 Vikombe vya chai.. endelea kusoma

elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

.

afya-mapishi-na-lishe.png
tafuta-ndugu.gif
vichekesho-bomba-vya-siku.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.