Mapishi ya Ugali Kwa Mchuzi Wa Kamba Wa Nazi, Kisamvu Na Kachumbari Ya Papa Mkavu

By, Melkisedeck Shine.

Vipimo - Ugali

Maji - 4 vikombe kiasi inategemea na unga wenyewe.

Unga wa sembe - 2 vikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Tia maji kiasi katika sufuria, weka motoni, yakipata moto korogea unga wa sembe kiasi na ufanye uji mzito uache uchemke vizuri huku ukikoroga.
Chota kibakuli kimoja cha uji huo weka pembeni kisha mimina unga wote uliobaki upigepige uchanganyike vizuri kwenye uji huo mpaka ushikamane
Punguza moto anza kuusonga taratibu huku ukiongeza ule uji ulioweka pembeni kidogo kidogo mpaka uone sasa umeshikamana vizuri.
Endelea kusonga mpaka ulainike kisha mimina kwenye bakuli au sahani iliyolowanishwa na maji kisha upete pete huku ukiugeuza geuza mpaka ukae shepu nzuri ya duara.Weka tayari kwa kuliwa.

Vipimo - Mchuzi wa kamba wa nazi

Kitunguu - 1

Nyanya - 2

Kamba waliomenywa - 1 Kilo

Pilipili mbichi iliyosagwa - ½ kijiko cha chai

Kitunguu saumu na tangawizi ilivyosagwa - 1 kijiko cha supu

Nazi nzito iliyochujwa - 1 kikombe

Bizari ya mchuzi - ½ kijiko cha chai

Chumvi - Kiasi

Ndimu - Nusu

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Safisha na osha kamba vizuri kisha mtie katika sufuria. Katia kitunguu, nyanya, tia chumvi, pilipili mbichi ya kusaga, thomu na tangawizi, bizari ya mchuzi na ndimu. Tia maji kidogo kiasi acha ichemke.
Watakapoiva na karibu kukauka, mimina tui la nazi taratibu koroga kiasi
Punguza moto aacha ichemke kidogo ukiwa mchuzi tayari.

Vipimo - Kisamvu

Kisamvu - 2 vikombe

Kunde mbichi zilizochemshwa - 1 kikombe

Kitunguu - 1

Nazi nzito iliyochujwa - 1 vikombe

Chumvi - Kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Weka kisamvu katika sufuria, katia kitunguu, tia chumvi, maji kidogo acha kichemke.
Huku ikichemka mimina kunde mbichi zilizochemshwa acha zipikikie kidogo mpaka kisamvu kikaribie kukauka na kunde kuiva.
Mimina nazi nzito punguza moto acha ichemke kidogo, mimina kwenye bakuli tayari kwa kuliwa.

Vipimo - Kachumbari Ya Papa

Papa mkavu (au nguru) - kipande

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Muoshe papa vizuri atoke mchanga kisha mchome kwenye jiko la mkaa au unaweza kumtia kwenye treya kisha kwenye oven kwa moto wa 350 kwa dakika 15 mpaka 20.
Akikauka mchambue chambue weka kando.
Tengeneza kachumbari, kwa kukata kitunguu, nyanya na pilipili mbichi, tia ndimu na chumvi.
Changanya na papa mkavu uliyemchambu ikiwa tayari.


UJUMBE-UNAVYOMMISI-NDUGU.JPG

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Mapishi ya Ugali Kwa Mchuzi Wa Kamba Wa Nazi, Kisamvu Na Kachumbari Ya Papa Mkavu;

a.gif Mapishi ya Muhogo Na Mbatata Za Nazi Kwa Nyama Ngombe

Nyama ya n’gombe ya mifupa - 3 lb.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Pilau Ya Nyama Ng'ombe Karoti Na Zabibu

Nyama ng’ombe ya mifupa ilokatwa vipande - 1 kilo.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Wali Wa Nazi Kwa Mchuzi Wa Samaki Na Rojo La Bilingani Na Viazi/Mbatata

Mpunga - 4 vikombe.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kutengeneza Pilau Ya Kuku

Mchele wa basmati - 3 vikombe.. endelea kusoma

[Kitendawili Kwako] 👉Sisi sate hapa tumeoza viuno

[Kichekesho Kwako] 👉Huyu mke ni shida!

kj.gif

a.gif Faida 6 za kula karoti kiafya

Asilimia kubwa tunapenda kutumia karoti katika kuunga katika mboga ya nyama na si kuila karoti kama karoti. wataalamu wanashauri ili uwe na afya bora unatakiwa ule karoti sita kwa wiki au moja kwa siku. Unaweza kula karoti ya kuchemshaa,juisi au mbichi… endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Wali Wa Zaafarani Na Kuku Wa Kupaka

Mchele - 3 Vikombe.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika Vileja Vya Tambi

Tambi (vermiceli Roasted) Mifuko 2.. endelea kusoma

a.gif Faida 10 za kula tende kiafya

Kila wakati unashauriwa na watalam wa afya ya kwamba unatakiwa kula tende kwa wingi ili kupata faida zifuatazo katika mwili wako:.. endelea kusoma

[Msemo wa Leo] 👉Matendo ya mtu

[Jarida la Bure] 👉Biblia ya Kiswahili- Agano Jipya

FURSA.PNG

Fursa Ya Kazi Na Ajira Yenye Malipo Mazuri

Au soma zaidi hapa

.

Marafiki-wa-enzi.GIF
ndugu.gif

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.