Mapishi ya Samaki wa kupaka

Mpendwa Msomaji, baada ya kukuandalia makala inayopendwa kuhusu; Jinsi ya kupika Mboga Za Majani Makavu (Aina Yoyote), sasa nimekuandalia makala hii kuhusu;

Mapishi ya Samaki wa kupaka.

Unaalikwa pia kusoma kuhusu; Mapishi ya visheti vitamu.

Mapishi ya Samaki wa kupaka

By, Melkisedeck Shine.

Mahitaji

Samaki (Tilapia 2)
Nyanya ya kopo (Tomato tin 1)
Kitunguu (Onion 1)
Tangawizi (ginger kiasi)
Kitunguu swaum (garlic clove )
Mafuta (Vegetable oil)
Pilipili (scotch bonnet pepper 1)
Tui la nazi zito (coconut milk 2 vikombe vya chai)
Curry powder 1/2 cha kijiko cha chai
Binzari nyembamba ya unga (ground cumin 1/2 kijiko cha chai
Binzari manjano (turmaric 1/2 kijiko cha chai
Chumvi (salt)
Limao (lemon 1)
Giligilani (fresh coriander)

Matayarisho

Marinate samaki na chumvi, limao, kitunguu swaum, tangawizi kwa muda wa masaa 6 au zaidi. Baada ya hapo wakaange au waoke katika oven mpaka waive ila usiwakaushe sana. Baada ya hapo saga pamoja nyanya ya kopo, kitunguu maji, kitunguu swaum na tangawizi. Kisha bandika huo mchanganyiko jikoni na upike mpaka ukauke maji kisha tia mafuta, binzari zote, curry powder, chumvi na pilipili na upike kwa muda wa dakika 5. Baada ya hapo tia maji kidogo (kama 1/2 kikombe) pamoja na tui la nazi. Acha uchemke mpaka tui liive na mchuzi ubakie kiasi. Baada ya hapo waweke samaki kwenye sufuria ya kuokea na kisha umwagie huo mchuzi juu ya hao samaki na owaoke (bake) kwa muda wa dakika 20. Ukisha toa kwenye oven katakata giligilani na utie kwenye hao samaki na hapo watakuwa tayari kwa kuliwa. unaweza kuwala na wali, ugali au chapati

Usisahau kushare makala hii uliyoisoma kuhusu; Mapishi ya Samaki wa kupaka. Share Facebook, Twitter bila kusahau WhatsApp.

Makala hii kuhusu, Mapishi ya Samaki wa kupaka, imeonekana kupendwa na wasomaji wengi. Makala nyingine zinazopendwa ni kama hizi zifuatazo;

• Jinsi ya kupika Visheti, endelea kusoma...

• Mapishi ya Wali, Mchuzi Wa Nazi Wa Samaki Nguru, endelea kusoma...

• Mapishi ya Biriani Ya Kuku Wa Kuchoma Wa Tanduri, endelea kusoma...

• Mapishi ya Maharage, endelea kusoma...

• Mapishi ya Dagaa wa nazi, nyanya chungu na bamia, endelea kusoma...

• Mapishi ya Mlenda wa bamia na nyanya chungu, endelea kusoma...

• Mapishi ya Maini ya ng'ombe, endelea kusoma...

• Mapishi ya Firigisi za kuku, endelea kusoma...

• Mapishi ya Mchuzi wa kambale, endelea kusoma...

• Mapishi ya Maharage na spinach, endelea kusoma...

Unaweza kusoma makala mpya nzuri kila unapotembelea website hii wakati wowote. Baada ya kusoma makala hii kuhusu; Mapishi ya Samaki wa kupaka, sasa endelea kusoma makala hizi nyingine nzuri nilizokuandalia;

Usipitwe na Nafasi za kazi kwa leo

<<Bofya HAPA kujua zaidi>>

.