AckySHINE Afya na Mapishi Β» Mapishi ya Pilau Ya Samaki Wa Tuna Na Mboga

Tafuta

πŸ‘‰ Mapishi ya Pilau Ya Samaki Wa Tuna Na MbogaπŸ‘‡βœ”

Mahitaji

Mchele - 2 Mugs

Mboga mchanganyiko za barafu (Frozen veg) - Mug

Tuna (samaki/jodari) - 2 kopo

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi -2 vijiko vya supu

Garam masala - 1 kijiko cha supu

Nyanya - 2

Kitungu maji - 1

Mdalasini nzima - 2 vijiti

Karafuu - 6 chembe

Pilipili mbichi - 1

Chumvi - kiasi

Viazi - 3

Maji - 2 Β½ Mugs

Mafuta - 3 vijiko vya supu

Maandalizi

Osha mchele na uroweke kwa muda wa dakika 20
Tia mafuta katika sufuria, kaanga kitunguu maji mpaka kigeuke rangi ya hudhurungi (brown).
Mimina viazi, thomu na tangawizi, bizari zote na kaanga.
Tia nyanya uliyokatakata ikaange mpaka iwive.
Tia tuna endelea kukaanga kidogo tu.
Tia maji, yatakapochemka tia mchele.
Punguza moto uwe mdogo funika kwa muda wa Β½ saa hadi wali ukauke na uwive. Utakuwa tayari kuliwa.

πŸ™‰πŸ™‰πŸ™‰Usisahau kushare posti hii kuhusu (Mapishi ya Pilau Ya Samaki Wa Tuna Na Mboga).πŸ‘ Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasomeπŸ’―βœ”

Tafuta ndugu zako hapa Utawapata kirahisi zaidi

πŸ‘‰Jua Zaidi...

rafiki.gif

Expert available for Hire

Je, unatoa misaada kwa jamii? Tangaza kituo chako bure hapa.
Soma%20Zaidi.gif