Mapishi ya Pilau Ya Nyama Ya Ng'ombe Na Nyanya

By, Melkisedeck Shine.

uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png

Mapishi ya Pilau Ya Nyama Ya Ng'ombe Na Nyanya

Vipimo

Mchele (Basmati) - 3 vikombe

Nyama ya ngo’mbe - 1 kg

Pilipili boga - 1 kubwa

Nyanya - 2 kubwa

Vitunguu maji - 2 vikubwa

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 1 kijiko cha supu

Tangawizi - 1 kijiko cha chai

Ndimu - 1

Mafuta ya kupikia - ½ kikombe

Mdalasini - ½ kijiko cha chai

Binzari nyembamba - 1 kijiko cha chai

Pilipili manga - ½ Kijiko cha chai

Hiliki - ½ Kijiko cha chai

Namna ya kutayarisha na Kupika

Roweka mchele wako katika chombo

Chukuwa nyama na ioshe vizuri na itie thomu, tangawizi, ndimu, pilipili manga na chumvi kiasi

Iweke jikoni hadi ikauke maji na kuwa imewiva huku ukiikaanga kaanga kwa hayo hayo mafuta yake hadi kuwa rangi ya hudhurungi

Katakata Vitunguu na nyanya weka pembeni

Chukua pilipili boga, thomu, tangawizi na visage katika mashine ya kusagia

Weka sufuria pembeni na utie mafuta, subiri yapate moto

Kisha tia vitunguu na vikaange hadi kuwa hudhurungi na tia nyanya

Kisha mimina mchanganyiko wako ulio usaga wa pilipili boga, thomu na tangawizi

Koroga kwa dakika kadhaa Kisha mininia nyama uliyokuwa tayari, maji kiasi na chumvi wastani na subiri maji hayo yachemke

Weka mchele humo na koroga kiasi na onja chumvi kama ipo sawa au kama ndogo unaweza kuongeza

Funika na punguza moto na uache uive taratibu

Baada ya kukauka maji kabisa basi ugeuze na subiri tena kwa dakika kama mbili na tayari kuliwa.


Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Mapishi ya Pilau Ya Nyama Ya Ng'ombe Na Nyanya;

a.gif Mapishi ya Biriani Nyepesi Kupika Ya Samaki

Mchele wa pishori (basmati) - 4.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Ugali Mchuzi Wa Samaki Nguru Wa Nazi Na Bamia Za Kukaanga

Unga wa mahindi/sembe - 4.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Wali Wa Nyanya Wa Kukaanga

Mchele basmati, pishori - 3 vikombe.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Wali Wa Kichina Wa Kuku Na Mboga Mchanganyiko

Mchele wa basmati/pishori - 4 vikombe vikubwa (mugs).. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika Biskuti Za Kopa Za Kunyunyuziwa Sukari Za Rangi

Unga vikombe 2 ¼.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Viazi, samaki na asparagus

Viazi (potato 1/2 kilo)
Samaki (fish 2)
Asparagus 8
Kitunguu kilichokatwa (chopped onion 1)
Kitunguu swaum kilichosagwa (garlic 4 cloves)
Tangawizi iliyosagwa kiasi (ginger paste)
Limao (lemon 1)
Giligilani iliyokatwakatwa (chopped coriander)
Curry powder (kijiko 1 cha chai)
Chumvi (salt)
Mafuta (vegetable oil).. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Wali Wa Kichina Wa Kamba Na Kuku

Mchele wa pishori (basmati) - 4.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kutengeneza Visheti Vyeupe Na Vya Kaukau

VIAMBAUPISHI.. endelea kusoma

picha-kali.png

.

afya-mapishi-na-lishe.png
UJUMBE-MSAMAHA-35JHF32.JPG
elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.