Mapishi ya Pilau Ya Nyama Ng'ombe Karoti Na Zabibu

Mpendwa Msomaji, baada ya kukuandalia makala inayopendwa kuhusu; Mapishi ya visheti vitamu, sasa nimekuandalia makala hii kuhusu;

Mapishi ya Pilau Ya Nyama Ng'ombe Karoti Na Zabibu.

Unaalikwa pia kusoma kuhusu; Mapishi ya Chapati za maji za vitunguu.

Mapishi ya Pilau Ya Nyama Ng'ombe Karoti Na Zabibu

By, Melkisedeck Shine.

Vipimo - Nyama

Nyama ng’ombe ya mifupa ilokatwa vipande - 1 kilo

Tangawizi na thomu (somu/garlic) ilosagwa - 2 vijiko vya supu

Bizari mchanganyiko/garama masala - 1 kijiko cha chai

Chumvi - Kiasi

Vipimo - Wali

Mchele - 4 glass

Mbatata/viazi menya katakata - 3 kubwa

Vitunguu katakata - 5

Kitunguu thomu kilosagwa (garlic/somu) - 1 kijiko cha supu

Hiliki ya unga - 1 kijiko cha chai

Bizari nzima ya pilau/cumin - 1 mti

Samli au mafuta - 2 Vijiko vya supu

Karoti zilokatwakatwa nyembamba - 6-7

Zabibu - Kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Katika sufuria weka mafuta kijiko kimoja cha supu tia nyama na viungo vyake.
kaushe katika moto hadi ikaribie kukauka kisha tia maji kiasi cha kuivisha na kubakisha supu ya mchele.
Katika sufuria ya kupikia weka samli au mafuta ishike moto.
Tia mbatata/viazi kaanga, tia vitunguu kaanga kidogo.
Tia kitunguu thomu, hiliki, bizari ya pilau endelea kukaanga hadi viwe rangi ya brown kidogo.
Tia mchele kaanga kidogo, kisha mimina nyama na supu yake. Funika wali uwive.
Weka kikaangio katika moto, tia samli kijiko kimoja kisha tia karoti na zabibu, kaanga kwa sekunde chache tu kwa ajili ya kulainisha karoti na zabibu.
Utakapopakuwa wali, pambia juu karoti na zabibu.

Usisahau kushare makala hii uliyoisoma kuhusu; Mapishi ya Pilau Ya Nyama Ng'ombe Karoti Na Zabibu. Share Facebook, Twitter bila kusahau WhatsApp.

Makala hii kuhusu, Mapishi ya Pilau Ya Nyama Ng'ombe Karoti Na Zabibu, imeonekana kupendwa na wasomaji wengi. Makala nyingine zinazopendwa ni kama hizi zifuatazo;

• MAPISHI YA LADU, endelea kusoma...

• Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia baking soda, endelea kusoma...

• Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia papai, endelea kusoma...

• Mapishi ya Ugali Kwa Mchuzi Wa Samaki Wa Kuchoma, endelea kusoma...

• Mapishi ya Biriani Ya Kuku Wa Kuchoma Wa Tanduri, endelea kusoma...

• Jinsi ya kutengeneza Wali Wa Dengu Kwa Samaki Wa Kukaanga, endelea kusoma...

• Jinsi ya kupika Wali Wa Samaki Na Mboga, endelea kusoma...

• Mapishi ya Pilau Ya Nyama ya Kusaga, Adesi Za Brauni Na Zabibu, endelea kusoma...

• Mapishi ya viazi mbatata Vya Nazi Kwa Nyama Ya Ng'ombe, endelea kusoma...

• Mapishi ya Ndizi Mbichi Za Nyama Ng'ombe, endelea kusoma...

Unaweza kusoma makala mpya nzuri kila unapotembelea website hii wakati wowote. Baada ya kusoma makala hii kuhusu; Mapishi ya Pilau Ya Nyama Ng'ombe Karoti Na Zabibu, sasa endelea kusoma makala hizi nyingine nzuri nilizokuandalia;

FURSA..! Kuna nafasi za kazi 100.

Au soma zaidi hapa

.

MLO-MWEMA-KWA-NDUGU-UJUMBE.JPG
UJUMBE-UNAVYOMMISI-NDUGU.JPG