Mapishi ya Pilau Ya Nyama Na Mtindi

By, Melkisedeck Shine.

elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

Mapishi ya Pilau Ya Nyama Na Mtindi

MAHITAJI

Nyama iliyokatwa vipande - 1 Ratili(LB)

Mchele Basmati - 2 Magi

Chumvi ya wali - kiasi

Kitungu kilichokatwa katwa - 1 kikubwa

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi - 1 kijiko cha supu

Mtindi (yogurt) - ½ kikombe

Mchanganyiko wa bizari ya pilau ya tayari - 2 vijiko vya supu

Mafuta kidogo yakukaangia

Rangi ya manjano (ukipenda)

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

Osha mchele na roweka nusu saa .

Weka mafuta katika sufuria na kaanga vitungu mpaka viwe rangi ya hudhurungi (brown).

Tia thomu na tangawizi na ukaange kidogo.

Kisha weka bizari ya pilau halafu nyama huku unakaanga hadi nyama isiwe nyekundu tena.

Tia maji gilasi 1½- 2 ichemke mpaka nyama iwive na karibu kukauka.

Mimina mtindi na iachie moto mdogo ikauke kidogo.

Kwenye sufuria nyingine chemsha mchele pamoja na chumvi na mafuta kidogo mpaka uive.

Mimina wali juu ya nyama, kisha nyunyiza rangi (ukipenda) kama vile wali wa biriani na ufunike kwa dakika kumi hivi.

Changanya wali na nyama pamoja ikiwa tayari kuliwa.


Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Mapishi ya Pilau Ya Nyama Na Mtindi;

a.gif Mapishi ya Wali Wa Mboga Na Samaki Wa Pink Salmon

Mchele 3 vikombe.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya wali Wa Nazi Kwa Mchuzi Wa Nyama Ng’ombe Na Mchicha

Mchele wa mpunga - 4 Vikombe.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Ugali Kwa Mchuzi Wa Nyama, Mchicha, Maharage Na Chatini Ya Pilipili Mbichi

Nyama ya ng’ombe vipande vidogo - 2lb.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Biriyani Ya Kuku

Mrowanishe kuku na viungo hivi kwa muda mdogo tu.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kutengeneza Biriani Ya Nyama Ya Ng'ombe

Nyama - 2 Ratili (LB).. endelea kusoma

a.gif Madhara ya kubana mkojo muda mrefu

Utakubaliana na mimi kwamba, kitendo cha mtu kubanwa na haja ndogo siyo kitu cha hiyari kwamba sasa mtu anaamua ngoja nibanwe na mkojo, hili ni jambo la asili na ni matokeo ya vyakula, matunda au vinywaji tunavyotumia. Kwa lugha nyingine tumekuwa tukiita kuwa ni wito wa asili au nature’s call… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kujua kama una Mimba: Dalili za kwanza kabisa za Ujauzito

Mwanamke anapopata ujauzito kwa kawaida huwa anaanza kuona dalili ambazo si za kawaida. Na ni wakati huo ambao ni muafaka kwake kuanza kuuchunguza mwili wake… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika kisamvu bila nazi

Kisamvu ni aina ya mboga ya majani inayopatikana kwa wingi na kwa urahisi katika mikoa takriban yote nchini Tanzania.
Pia aina hii ya mboga hupikwa katika mapishi ya aina mbalimbali kulingana na mahitaji ya mpishi… endelea kusoma

uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png

.

afya-mapishi-na-lishe.png
MPENZI-MLO-MWEMA-34NG.JPG
vichekesho-bomba-vya-siku.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.