Mapishi ya Pilau Ya Mchicha

By, Melkisedeck Shine.

VIPIMO

Mchele - 3 Vikombe

Mchicha

Mafuta - 1/2 kikombe

Vitunguu maji - 2 vikubwa

Nyanya - 1

Viazi - 3

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 3 vijiko vya supu

Vidonge vya supu (Stock cubes) - 3

Jiyrah (cummin powder) - 1 kijiko cha chai

Pilipili manga ya unga - 1 kijiko cha chai

Hiliki ya unga - 1/2 kijiko cha chai

Mdalasini - 1 kijiti

Maji (inategemea mchele) - 5 vikombe

Chumvi

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1. Osha na roweka mchele.

2. Osha mchicha, chuja maji na katakata.

3. Katakata vitunguu maji, nyanya.

4. Menya na kata viazi vipande ukaange pekee vitoe weka kando.

5. Katika sufuria tia mafuta na kaanga vitunguu hadi viwe rangi ya hudhurungi.

6. Tia thomu, bizari zote, kaanga kidogo kisha nyanya.

7. Tia mchicha kaanga kidogo kisha tia mchele, maji na vidonge vya supu, chumvi.

8. Koroga kidogo kisha tia viazi ulivyovikaanga, funika na acha uchemke kidogo katika moto mdogo mdogo.

9. Kabla ya kukauka maji, mimina katika chombo cha kupikia ndani ya oven (oven proof) au katika treya za foil, funika vizuri na upike ndani ya oven moto wa 400º kwa dakika 15-20 upikike hadi uive.

10. Ukishaiva epua na tayari kuliwa na kitoweo chochote upendacho.


Marafiki-wa-enzi.GIF

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Mapishi ya Pilau Ya Mchicha;

a.gif Mapishi ya Wali, Mchuzi Wa Nazi Wa Samaki Nguru

Mchele - 3 vikombe.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Wali Wa Mboga Na Mchuzi Wa Kuku wa Tanduri

Mchele basmati - 3 magi (kikombe kikubwa).. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya wali Wa Nazi Kwa Mchuzi Wa Nyama Ng’ombe Na Mchicha

Mchele wa mpunga - 4 Vikombe.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Wali Wa Mboga Na Samaki Wa Pink Salmon

Mchele 3 vikombe.. endelea kusoma

[Kitendawili Kwako] 👉Kinapanda 'chochoIi'

kj.gif

a.gif Faida za Korosho Kiafya

Korosho zina faida hizi zifuatazo;.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kuandaa Vileja Vya Tambi

Tambi (vermiceli Roasted) Mifuko 2.. endelea kusoma

a.gif Madhara ya kisukari kwa nguvu za kiume

Kulingana na baadhi ya chunguzi zilizofanywa na wanasayansi asilimia 60 – 70 ya wanaume hupoteza nguvu za kiume kutokana na ugonjwa wa kisukari… endelea kusoma

a.gif Faida 10 za kula tende kiafya

Kila wakati unashauriwa na watalam wa afya ya kwamba unatakiwa kula tende kwa wingi ili kupata faida zifuatazo katika mwili wako:.. endelea kusoma

FURSA..! Kuna nafasi za kazi 100.

Au soma zaidi hapa

.

KADI-MLO-MWEMA-MZAZI.JPG
PONGEZI-MPENZI-24498UA8.JPG

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.