Mapishi ya Pilau Ya Bilingani Na Kuku

By, Melkisedeck Shine.

Viambaupishi

Mchele wa basmati - 3 vikombe

Kuku - ½

Bilingani - 2 ya kiasi

Viazi - 4

Vitunguu - 2

Kitunguu (thomu/galic) iliyosagwa - 2 vijiko vya supu

Pilipili mbichi iliyosagwa - 2

Chumvi - kiasi

Garama masala (mchanganyiko wa bizari) - 1 kijiko cha chai

Hiliki ya unga - ¼ kijiko cha chai

Mafuta ya kupikia wali - ¼ kikombe

Mafuta ya kukaangia viazi na bilingani - kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:

Osha mchele na roweka kwa muda kutegemea na aina ya mchele.
Kata kuku vipande upendavyo safisha
Kisha mchemshe kwa chumvi, pilipili iliyosagwa, thomu, na bizari mchanganyiko (garama masala).
Akiwiva kuku, mtoe weka kando, bakisha supu katika sufuria.
Menya na kata viazi kaanga weka kando.
Kata kata bilingani slesi nene kaanga, chuja mafuta weka kando.
Katika sufuria, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangu ya hudhurungi. Tia vipande vya kuku, ukaange kidogo.
Tia supu ya kuku, mchele, tia hiliki, ufunike hadi karibu na kuwiva kabisa.
Tia viazi na bilingani uchanganye kidogo, kisha tia katika oven imalizike kupikika pilau humo au unaweza kuendelea kufunika juu ya jiko hadi pilau iwive.
Pakua katika sahani ikiwa tayari kuliwa kwa saladi ya mtindi.


UJUMBE-ZA-USIKU-KWA-NDUGU.JPG

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Mapishi ya Pilau Ya Bilingani Na Kuku;

a.gif Mapishi ya Wali Wa Kichina Wa Kamba Na Kuku

Mchele wa pishori (basmati) - 4.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika Biriyani Ya Nyama Ng'ombe

Nyama vipande - 3 LB.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya wali kuku wa Kisomali

Mchele - 3 vikombe.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Borhowa

Daal (lentils) nyekundu au/na kijani - 1 Kikombe kikubwa

Bizari ya manjano ya unga - 1/2 Kijiko cha chai

Pili pili ya unga - 1/2 kijiko cha chai

Chumvi - Kiasi

Maji ya ndimu - 3 Vijiko vya supu

Kitunguu - 1 kiasi

Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 Kijiko cha chai

Bizari ya unga (cummin powder) - 1 Kijiko cha chai

Mafuta ya kukaangia - Kiasi.. endelea kusoma

[Kitendawili Kwako] 👉Nilikwenda nikichoma nikarudi nikichoma

[Video Nzuri] 👉Angalia huyu mtu alichofanyiwa

[Chemsha Bongo Kwako] 👉Je, hii familia ina watoto wangapi?

mtu.gif

a.gif Madhara ya kutumia dawa za kuzuia mimba wakati wa hatari

Watu wengi hasa vijana watakuwa wanafahamu dawa ambazo hutumiwa sana kuzuia ujauzito pale ambapo wapenzi wamejamiiana ndani ya siku za hatari. Ninazungumzia dawa za kuzuia mimba sio dawa za kupanga uzazi. Dawa hizi zipo za aina nyingi ambazo zitozitaja hapa siku ya leo. Endapo wawili hawa wanakuwa hawapo tayari kupata mtoto, na wanaona kwamba siku walizojamiiana zitapelekea mwanamke huyo kutunga mimba, basi anaweza kutumia dawa hizi ambazo zinaharibu mazingira au uwezekano wa mimba kutungwa… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kutengeneza Wali Wa Dengu Kwa Samaki Wa Kukaanga

Mchele wa basmati - 3 Vikombe.. endelea kusoma

a.gif Vidokezo vya kukusaidia ule mboga za majani zaidi

Pika mboga mpya za majani au zilizogandishwa kwa barafu katika wimbi mikro kwa mlo wa haraka na rahisi kuongeza kwa mlo wowote. Pika maharagwe ya kijani, karoti, au brokoli kwa mvuke katika bakuli na kiwango kidogo cha maji katika wimbi mikro kwa mlo wa haraka… endelea kusoma

a.gif Tabia 10 zinazoweza kuharibu figo

1.Kubana mkojo kwa muda mrefu
2.Kutokunywa maji ya kutosha kila siku
3.Kutumia chumvi nyingi kuliko kawaida
4.Kula nyama mara kwa mara au mara nyingi
5.Kutokula chakula cha kutosha.. endelea kusoma

[Msemo wa Leo] 👉Umakini

[Hadithi Nzuri] 👉Kisa cha baba mzee na mwanae

Usipitwe na Nafasi za kazi kwa leo

<<Bofya HAPA kujua zaidi>>

.

UJUMBE-WA-ZA-JIONI-KWA-NDUGU.JPG
UJUMBE-WA-MCHANA-KWA-NDUGU.JPG

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.