Mapishi ya Pilau Ya Adesi Za Brown Karoti Na Mchicha Kwa Samaki Wa Salmon

By, Melkisedeck Shine.

elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

Mapishi ya Pilau Ya Adesi Za Brown Karoti Na Mchicha Kwa Samaki Wa Salmon

Vipimo

Mchele vikombe 3

Karoti 1 ikune (grate)

Mchicha katakata kiasi

Adesi za brown

Kitunguu katakata (chopped)

Supu ya kitoweo chochote upendayo au vidonge vya supu 2

Garama masala (bizari mchanganyiko) kijiko 1 cha kulia

Samli ¼ kikombe

Chumvi kiasi

Vipimo Vya Samaki Wa Salmon

Samaki wa Salmon vipande 4 vikubwa

Tangawizi mbichi ilosagwa kijiko 1 cha kulia

Thomu (garlic/saumu) kijiko 1 cha kulia

Chumvi kiasi

Bizari ya mchuzi kijiko 1 cha kulia

Ndimu 1 kamua

Nyanya 2 kata slice kubwa kubwa

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Samaki wa Salmon

Changanya viungo vyote upake katika samaki.
Weka katika treya na panga slice za nyanya juu yake.
Oka (grill/choma) katika oven umgeuze samaki upande wa pili.
Akiwa tayari epua.

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Wali

Roweka mchele kiasi kutegemea aina ya mchele. Tumia basmati (pishori)
Roweka adesi kisha zichemshe katika maji ya kiasi. Chuja maji adesi na maji yatakayobakia tumia katika kupikia pilau hii.
Kaanga vitunguu katika samli iliyoshika moto kwenye sufuria ya kupikia.
Vikianza kugeuka rangi tia karoti, mchicha, adesi, bizari mchanganyiko kisha kaanga kidogo.
Tia mchele ukaange kidogo kisha tia supu au maji pamoja na kidonge cha supu.
Tia chumvi ukoroge funika upike kama pilau.
Epua upakue katika sahani utolee kwa samaki wa salmon


vichekesho-bomba-vya-siku.png

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Mapishi ya Pilau Ya Adesi Za Brown Karoti Na Mchicha Kwa Samaki Wa Salmon;

a.gif Jinsi ya kutengeneza Biriani Ya Nyama Ya Ng'ombe

Nyama - 2 Ratili (LB).. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Ugali Kwa Mchuzi Wa Nazi Wa Nyanya Chungu/Mshumaa/Ngogwe Na Bamia, Mboga Ya Matembele Na Samaki Wa Kukaanga

Unga wa mahindi - 4.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Boga La Nazi

Boga la kiasi - nusu yake.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika Magimbi Kwa Nyama Ya Ng’ombe

Majimbi (Eddoes) kiasi 6 au 7.. endelea kusoma

[Kitendawili Kwako] 👉Chapanda mti bila miguu

[Kichekesho Kwako] 👉Mkalimani alivyoharibu ibada ya leo

afya-mapishi-na-lishe.png

a.gif Njia za kuongeza wingi wa mbegu za kiume

Chakula unachokula kina mchango mkubwa katika kutibu tatizo hili. Vyakula vingi vya kisasa havina uwezo wa kuongeza uwingi wa mbegu… endelea kusoma

a.gif Lishe

• Lishe yahusu mafunzo ya chakula na jinsi miili yetu inavyotumia chakula kamakichocheo cha ukuaji, kuzaana na utunzaji wa afya.
• Lishe inajumuisha mchakato wa utoaji virutubishi vinavyohitajika kwa afya, ukuaji, kuendelea na kuishi… endelea kusoma

a.gif Ulaji mzuri hupunguza uwezekano wa kupata shinikizo la chini la damu

Ni mhimu kula mlo kamili kila siku. Kula lishe duni kunaweza kupelekea kuzalishwa kwa damu isiyo na afya inayoleta shinikizo la damu… endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Wali wakukaanga

Mchele (Basmati rice) 1 kilo
Vitunguu (chopped onion) 2 vikubwa
Garlic powder 1/2 kijiko cha chai
Njegere (peas) 1 kikombe
Turmaric 1/2 kijiko cha chai
Coriander powder 1/2 kijiko cha chai
Cumin seeds 1/2 kijiko cha chai
Mafuta ya kupikia 2 vijiko vya chakula
Chumvi kiasi.. endelea kusoma

[Msemo wa Leo] 👉Uzuri na ubora

familia-mapenzi-na-mahusiano.png

.

picha-kali.png
KADI-TUKUTANE-MZAZI.JPG
uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.