AckySHINE Afya na Mapishi Β» Mapishi ya wali mtamu Wa Nazi Kwa Maharage Na Samaki Nguru Wa Kukaanga

Tafuta

πŸ‘‰ Mapishi ya wali mtamu Wa Nazi Kwa Maharage Na Samaki Nguru Wa KukaangaπŸ‘‡βœ”

USIKOSE HIIπŸ‘‰ Tafuta ndugu zako msiojuana hapa

Vipimo

Wali:

Mchele mpunga - 4 Vikombe

Tui la nazi - 6 vikombe

Chumvi - kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Osha mchele weka kando.
Bandika tui jikoni likichemka tia mchele na chumvi.
Funika uchemke, tui likikauka wacha moto mdogomdogo hadi wali uive ukiwa tayari. Ikiwa unatumia mkaa unapalia juu yake.

Maharage Ya Nazi

Maharage - 3 vikombe

Tui la nazi zito - 1 kikombe

Tui la nazi jepesi - 1 kikombe

Kitunguu maji - 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa -1 kijiko cha chai

Chumvi - kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Chemsha maharage mpaka yaive.
Katiakatia kitunguu maji na tia thomu, tia na tui jepesi kikombe kimoja.
Tia tui zito endelea kuweka katika moto mdogomdogo hadi yakaribie kukauka yakiwa tayari.

Samaki Nguru Wa Kukaanga

Samaki Wa Nguru - 4 vipande

Kitunguu saumu(thomu/galic) & tangawizi ilosagwa - 1 kijiko cha supu

Pilipili mbichi - 4

Ndimu - 2 kamua

Bizari ya samaki -1 kijiko cha chai

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Mwoshe samaki kisha mtie kitunguu thomu, tangawizi ilosagwa, chumvi, pilipilimbichi ilosagwa, ndimu na bizari ya samaki.
Mwache akolee viungo kwa muda kidogo.
Makaange katika mafuta hadi aive akiwa tayari.

πŸ™‰πŸ™‰πŸ™‰Usisahau kushare posti hii kuhusu (Mapishi ya wali mtamu Wa Nazi Kwa Maharage Na Samaki Nguru Wa Kukaanga).πŸ‘ Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasomeπŸ’―βœ”


"Kama vile moto unavyozimwa na maji ndivyo vivyo hivyo hasira inamalizwa na maneno ya upole."

mtu.gif

Expert available for Hire

Kampeni ya Amani na Upendo Lengo ni kudumisha Amani na Upendo.
Soma%20Zaidi.gif