MAPISHI YA LADU

Mpendwa Msomaji, baada ya kukuandalia makala inayopendwa kuhusu; Mapishi – Fish Finger, sasa nimekuandalia makala hii kuhusu;

MAPISHI YA LADU.

Unaalikwa pia kusoma kuhusu; MADHARA YA SHISHA.

MAPISHI YA LADU

By, Melkisedeck Shine.

VIAMBAUPISHI

Unga - 6 vikombe

Samli - ½kikombe

Baking Powder - ½kijiko cha chai

Maziwa- 1 kikombe

Maji -Kisia kiasi kama unga bado mzito

VIAMBAUPISHI VYA SHIRA

Sukari - 5 vikombe

Maji - 2 1/2 vikombe

Vanilla - 2 vijiko vya chai

Rangi ya orange - 1 kijiko cha chai

Iliki ya unga - 1 Kijiko cha chai

MAANDALIZI

Changanya unga wa dengu, samli, baking powder pamoja na maziwa katika mashine ya keki (cake mixer).
Ukisha changanya angalia kama mchanganyiko wako umekua mwepesi kidogo kuliko wa keki, kama bado mzito basi ongeza maji kiasi.
Kisha weka mafuta kiasi kwenye karai,weka na samli kikombe kimoja, weka kwenye moto wa kiasi.
Mafuta yakisha pata moto, chukua kijiko kikubwa cha matundu chota mchanganyiko wako na kijiko cha kawaida tia kwenye kijiko cha matundu. Hakikisha kijiko cha matundu kiwe juu ya karai ili mchanganyiko wako uchuruzike ndani ya mafuta yalio pata moto.
Pika ndani ya mafuta mpaka iwive, ila usiache ikawa brown.
Toa mchanganyiko ulowiva tia ndani ya shira uliyo pika. Hakikisha shira iwe imepoa kabla ya kutia mchanganyiko huo.
Endelea kupika mchanganyiko wako mpaka uishe, kila ukitoa katika mafuta hakikisha unatia ndani ya shira.
Ukishamaliza wote kanda huo mchanganyiko ulokua ndani ya shira mpaka uone shira yote imekauka (yaani iwe imeingia ndani ya mchanganyiko).
Tupia zabibu kavu na lozi zilizo katwa, changanya na mkono.
Wacha mchanganyiko katika bakuli, funika na foil mpaka siku ya pili.
Siku ya pili chukua mchanganyiko kiasi katika mkono tengeneza mviringo (round).

MAANDALIZI YA SHIRA

Katika sufuria, tia sukari, maji, iliki, vanilla na rangi.
weka kwenye moto wacha ichemke mpaka itowe povu (bubbles) juu.
Kisha toa povu, wacha shira kwenye moto kama dakika 3.
Hakikisha shira yako iwe inanata kiasi kwenye vidole, lakini iwe nyepesi kidogo kuliko shira ya kaimati.

Usisahau kushare makala hii uliyoisoma kuhusu; MAPISHI YA LADU. Share Facebook, Twitter bila kusahau WhatsApp.

Makala hii kuhusu, MAPISHI YA LADU, imeonekana kupendwa na wasomaji wengi. Makala nyingine zinazopendwa ni kama hizi zifuatazo;

• Jinsi ya kupika Mboga Za Majani Makavu (Aina Yoyote), endelea kusoma...

• Mapishi ya Wali Wa Nyanya Wa Kukaanga, endelea kusoma...

• Jinsi ya kupika Biskuti Za Ufuta Na Jam, endelea kusoma...

• Jinsi ya kutengeneza Biskuti Za Cornflakes, endelea kusoma...

• JINSI YA KUANDAA VILEJA, endelea kusoma...

• Namna ya kutengeneza Visheti Vya Nazi Na Njugu (Sudani), endelea kusoma...

• Jinsi ya kupika Baklawa Za Pistachio Na Lozi, endelea kusoma...

• Jinsi ya kupika Biskuti Nyembamba (Wafer Bar) Za Chokoleti Na Njugu, endelea kusoma...

• Jinsi ya kutengeneza biskuti za Matunda Makavu Na Cornflakes, endelea kusoma...

• Mapishi ya Biskuti Za Jam, endelea kusoma...

Unaweza kusoma makala mpya nzuri kila unapotembelea website hii wakati wowote. Baada ya kusoma makala hii kuhusu; MAPISHI YA LADU, sasa endelea kusoma makala hizi nyingine nzuri nilizokuandalia;

Usipitwe na Nafasi za kazi kwa leo

<<Bofya HAPA kujua zaidi>>

.

KADI-POLE-MZAZI.JPG
UJUMBE-WA-MCHANA-KWA-NDUGU.JPG