Mapishi ya Koshari Na Sosi Ya Kuku

Mpendwa Msomaji, baada ya kukuandalia makala inayopendwa kuhusu; Jinsi ya kupika vizuri Wali Wa Karoti Na Nyama, sasa nimekuandalia makala hii kuhusu;

Mapishi ya Koshari Na Sosi Ya Kuku.

Unaalikwa pia kusoma kuhusu; Jinsi ya kutengeneza Biskuti Za Tende.

Mapishi ya Koshari Na Sosi Ya Kuku

By, Melkisedeck Shine.

Vipimo Vya Koshari

Mchele - 2 vikombe

Makaroni - 1 kikombe

Dengu za brown - 1 kikombe

Vitunguu vilokatwakatwa (chopped) - 2

Nyanya ziilokatwakatwa (chopped) - 4

Nyanya ya kopo - 1 kijiko cha supu

Kitunguu saumu(thomu/galic) ilosagwa - 1 kijiko cha supu

Pilipili mbichi ilosagwa - 1 kijiko cha chai

Pilipili manga ya unga - 1 kijiko cha chai

Mdalisini kijiti - 1

Bizari ya pilau (cumin seeds) - 1 kijiko cha supu

Hiliki - 2 chembe

Mafuta - 3 vijiko vya supu

Chumvi - kiasi

Vipimo Vya Kuku

Kuku - 3 LB

Kitunguu saumu(thomugalic) na tangawizi - 1 kijiko cha supu

Mtindi (yoghurt) - 1 kijiko cha supu

Pilipili ya masala nyekundu - 1 kijiko cha chai

Bizari upendazo - 1 kijiko cha chai

Ndimu - 1

Vitunguu slesi vilokaangwa - 3

Namna Kutayarisha Kuku

Kata kuku vipande vikubwa kiasi, osha, weka kando achuje maji.
Changanya vipimo vya kuku pamoja katika kibakuli.
Changanya pamoja na kuku, roweka muda wa kiasi nusu saa au zaidi.
Mchome (grill) kuku hadi aive weka kando.

Namna ya Kutayarisha Koshari

Tia mafuta katika sufuria, kaanga vitunguu hadi viive kuwa rangi hudhurungi.
Tia thomu ,mdalisini, bizari ya pilau na hiliki kaanga tena kidogo.
Tia nyanya, pilipili zote, nyanya kopo, chumvi changanya vizuri ukaange kidogo.
Epua sosi acha kando.
Chemsha dengu pamoja na kidonge cha supu ziive nusu kiini na ibakie supu yake. Muda wa kuchemsha dengu inategemea aina yake.
Tia mchele uchanganyike, funika, pika hadi uive vizuri pamoja na dengu
Chemsha makaroni hadi yaive , epua chuja maji.
Changanya pamoja wali wa dengu na macaroni.
Pakua katika sahani, kisha weka juu yake kuku aliyechomwa, mwagia vitunguu vilokaangwa, kisha mwagia sosi.

Usisahau kushare makala hii uliyoisoma kuhusu; Mapishi ya Koshari Na Sosi Ya Kuku. Share Facebook, Twitter bila kusahau WhatsApp.

Makala hii kuhusu, Mapishi ya Koshari Na Sosi Ya Kuku, imeonekana kupendwa na wasomaji wengi. Makala nyingine zinazopendwa ni kama hizi zifuatazo;

β€’ Mapishi ya Wali wakukaanga, endelea kusoma...

β€’ Mapishi ya Chapati za Kusukuma kitaalamu, endelea kusoma...

β€’ Jinsi ya kupika Biskuti Nyembamba (Wafer Bar) Za Chokoleti Na Njugu, endelea kusoma...

β€’ Mapishi ya Kidheri - Makande, endelea kusoma...

β€’ Mapishi ya Bokoboko La Kuku, endelea kusoma...

β€’ Jinsi ya kutengeneza Muhogo Wa Nazi Na Samaki Wa Kukaanga, endelea kusoma...

β€’ Jinsi ya kupika Viazi Vya Nazi Kwa Nyama, endelea kusoma...

β€’ Jinsi ya kuandaa Pilau ya sosi ya soya, nyama na mboga, endelea kusoma...

β€’ Mapishi ya Haliym Ya Nyama Mbuzi -Bokoboko La Pakistan, endelea kusoma...

β€’ Jinsi ya kuandaa Muhogo, Samaki Wa Kuchoma Na Bamia, endelea kusoma...

Unaweza kusoma makala mpya nzuri kila unapotembelea website hii wakati wowote. Baada ya kusoma makala hii kuhusu; Mapishi ya Koshari Na Sosi Ya Kuku, sasa endelea kusoma makala hizi nyingine nzuri nilizokuandalia;

Usipitwe na Nafasi za kazi kwa leo

<<Bofya HAPA kujua zaidi>>

.

KADI-TUKUTANE-MZAZI.JPG
NIMEKUMISI-MPENZI086H.JPG