Mapishi ya Haliym Ya Nyama Mbuzi -Bokoboko La Pakistan

By, Melkisedeck Shine.

familia-mapenzi-na-mahusiano.png

Mapishi ya Haliym Ya Nyama Mbuzi -Bokoboko La Pakistan

Mahitaji

Nyama ya mbuzi au ng’ombe ya mafupa - 2 LB

Mchanganyiko wa dengu (hadesi, mchele, chooko, ngano, dengu n.k au nunua ya tayari iliyokwisha changanywa - 2 Vikombe

Kitungu maji (vikate vidogo) - 1

Mafuta - ¼ Kikombe

Nyana kata ndogo ndogo - 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawazi iliyosagwa - 1 Kijiko cha supu

Bizari ya haliym - 2 vijiko vya supu

Nyanya ya kopo - 2 vijiko vya supu

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Chemsha nyama na chumvi ½ kijiko mpaka iive, toa mafupa.
Chemsha mchanganyiko wa dengu mpaka ziive.
Katika sufuria weka mafuta, kaanga vitunguu vilainike, tia thomu na tangawizi, bizari ya haliym, nyanya ya kopo. Kaanga mpaka iwive.
Tia nyama iliyowiva na supu yake kidogo.
Tia mchanganyiko wa dengu tia kwenye mashine ya kusaga (blender), saga na ile supu ya nyama isagike vizuri
Mimina kwenye sufuria changanya, tia ndimu kidogo, acha moto mdogo mdogo kwa muda wa dakika 15.
Tia katika bakuli, pambia kwa vitunguu vilivyokaangwa vya rangi ya hudhurungi vikavu, pilipili mbichi (ukipenda) na kotmiri, ikiwa kuliwa.


Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Mapishi ya Haliym Ya Nyama Mbuzi -Bokoboko La Pakistan;

a.gif Jinsi ya kuandaa Muhogo, Samaki Wa Kuchoma Na Bamia

Mihongo 3 - 4.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kuandaa Biriani Na Sosi Ya Nyama Ya Mbuzi

Nyama Ya Mbuzi - 1 Kilo.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kuandaa Pilau ya sosi ya soya, nyama na mboga

Nyama isiyokuwa na mifupa - 1 ½ Lb(ratili)
Mchele wa Basmati (rowanisha) - 3 Magi
Vitunguu maji - 2
Mchanganyiko wa mboga za barafu - 1 Magi
(karoti, mahindi, njegere)
Pilipili Mbichi - 3
Pilipili mboga kijani na nyekundu - 1
Pilipili manga - ½ kijiko cha chai
Chumvi - Kiasi
Sosi ya soya (soy sauce) - 5 Vijiko vya supu
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa - 1 Kijiko cha supu
Mchanganyiko wa bizari (garam masala) - 1 Kijiko cha supu
Kotmiri iliyokatwa - ½ Kikombe
Mafuta ya kukaangia - Kiasi.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika Viazi Vya Nazi Kwa Nyama

Viazi - 3lb.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika kisamvu bila nazi

Kisamvu ni aina ya mboga ya majani inayopatikana kwa wingi na kwa urahisi katika mikoa takriban yote nchini Tanzania.
Pia aina hii ya mboga hupikwa katika mapishi ya aina mbalimbali kulingana na mahitaji ya mpishi… endelea kusoma

a.gif Namna ya kuondokana na tatizo la kunuka Kikwapa

Harafu ya jasho inakera, kibaya zaidi ni kuwa wewe mwenyewe husikii harufu hiyo ila wale walio karibu yako. Kwa upande mwingine kujaribu kuzuia kutoka jasho ni hatari kwa afya yako na kujaribu kuondoa harufu kwa kutumia pafyumu husababisha madhara mengine ya kiafya na kwa bahati mbaya perfume zina jaribu poteza harufu kwa mda mfupi tu na sio kutokomeza tatizo hilo… endelea kusoma

a.gif Sababu na tiba ya tatizo la kukoroma usiku

Kukoroma ni tatizo linalowapata watu wengi wakati wanapolala ambalo linaweza kuwatokea watu wa kila umri ingawa hutokea mara nyingi kwa wanaume au watu wanene. Kukoroma huzidi kwa kadri umri unavyoongezeka na asilimia 54 ya watu wazima hukoroma baadhi ya wakati huku asilimia 25 ya wengine wakiwa na tabia ya kukoroma kila wakati. Kukoroma baadhi ya wakati kwa kawaida sio tatizo kubwa na mara nyingi huleta tu karaha kwa mtu anayelala karibu na mkoromaji… endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Ugali na dagaa

Dagaa (dried anchovies packet 1)
Unga wa ugali (corn meal flour 1/4 kilo) (unaweza kutumia unga wa choice uipendayo)
Nyanya ya kopo (tin tomato 1/2)
Kitunguu maji (onion 1)
Limao (lemon 1/4)
Pilipili mbuzi nzima bila kukata (scotch bonnet pepper1, do not chop)
Chumvi (salt 1/4 ya kijiko cha chai)
Mafuta (vegetable oil)
Hoho (green pepper).. endelea kusoma

uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png

.

uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png
KUKUTANA-MPENZI-FG94T.JPG
uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.