Mapishi ya Biriani Ya Kuku Wa Kuchoma Wa Tanduri

By, Melkisedeck Shine.

uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png

Mapishi ya Biriani Ya Kuku Wa Kuchoma Wa Tanduri

Mahitaji

Mchele - 4 vikombe

Kuku - 1

Vitunguu - 3

Nyanya/tungule - 4

Zabibu kavu - ½ kikombe

Tangawizi na kitunguu (thomu/galic) - 2 vijiko cha supu

Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 kijiko cha supu

Mtindi (yoghurt) - 2 kijiko cha supu

Masala ya tanduri - 2 vijiko vya supu

Pilipili manga - 1 kijiko cha chai

Hiliki - ½ kijiko cha chai

Mdalasini - kijiti kimoja

Ndimu - 3 vijiko vya supu

Chumvi - kiasi

Zaafarani (saffron) - 1 kijiko cha chai

Mafuta - ½ kikombe

Namna Ya Kutayarisha Kuku:

Baada ya kumsafisha kuku, mkate vipande vikubwa vikubwa kiasi upendavyo, muoshe mchuje atoke maji.
Katika bakuli, tia tangawizi, kitunguu thomu ilosagawa, pilipili mbichi ilosagwa, chumvi, ndimu, mtindi, masala ya tanduri na uchanganye vizuri, kisha mtie kuku na uchanganye tena na acha arowanike kwa muda wa kiasi saa au zaidi.
Panga kuku katika sinia ya kuchoma ndani ya oveni. Kisha mchome (grill) hadi awive, mtoe acha kando. Mwagia juu yake masala yatakayobakia katika sinia baada ya kumchoma.

Namna Ya Kutayarisha Masala Ya Nyanya:

Weka mafuta katika karai, tia vitunguu ulivyokatakata, kaanga hadi vianze kugeuka rangi.
Tia nyanya ulizokatakata, tia pilipili manga, hiliki, mdalasini, chumvi, na zabibu. Kaanga kidogo tu yakiwa tayari.

Namna Ya Kutayarisha Wali:

Osha na roweka mchele wa basmati.
Roweka zaafarani kwa maji ya moto kiasi robo kikombe weka kando.
Chemsha maji, tia chumvi, kisha tia mchele uive nusu kiini.
Mwaga maji uchuje mchele kisha rudisha katika sufuria au sinia ya foil. Nyunyizia zaafarini, na rudisha katika moto upike hadi uive kamili.
Epua, kisha pakua wali katika sahani au chombo upendacho, mwagia juu yake masala ya nyanya. Kisha weka vipande vya kuku ulivyochoma, biriani ikiwa tayari.


Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Mapishi ya Biriani Ya Kuku Wa Kuchoma Wa Tanduri;

a.gif Jinsi ya kutengeneza Wali Wa Dengu Kwa Samaki Wa Kukaanga

Mchele wa basmati - 3 Vikombe.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika Wali Wa Samaki Na Mboga

Samaki wa sea bass vipande - 1 1/2 LB (Ratili)
Kitunguu saumu(thomu/galic) -1 Kijiko cha supu
pilipili mbichi iliyosagwa - 1 Kijiko cha chai
Bizari ya manjano au ya pilau - 1/2 Kijiko cha chai
Paprika ya unga au pilipili ya unga - 1 kijiko cha chai
Chumvi - Kiasi
Ndimu
Mafuta - 3 Vijiko vya supu.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Ugali Kwa Mchuzi Wa Samaki Wa Kuchoma

Unga wa mahindi - 4 vikombe.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Pilau Ya Nyama Ng'ombe Karoti Na Zabibu

Nyama ng’ombe ya mifupa ilokatwa vipande - 1 kilo.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika Biskuti Za Ufuta Na Jam

Unga 2 Viwili.. endelea kusoma

a.gif Madhara ya soda

Soda ni kiburudisho ambacho si muhimu sana kwa afya… endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Viazi vya nyama

Viazi (potato) 1 kilo
Nyama ya ng'ombe 1/2 kilo
Nyanya ya kopo iliyosagwa 1/2 tin
Vitunguu maji 2
Tangawizi/ swaum 1 kijiko cha chai
Hoho 1
Curry powder 1 kijiko cha chai
Pilipili ya unga 1/2 kijiko cha chai
Limao 1/2
Chumvi
Coriander
Mafuta ya kupikia.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya wali kuku wa Kisomali

Mchele - 3 vikombe.. endelea kusoma

uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png

.

picha-kali.png
UJUMBE-WA-MCHANA-KWA-NDUGU.JPG
vichekesho-bomba-vya-siku.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.