Mambo ya Msingi kuyajua kuhusu Ugonjwa wa Kipindupindu

By, Melkisedeck Shine.

afya-mapishi-na-lishe.png

Mambo ya Msingi kuyajua kuhusu Ugonjwa wa Kipindupindu

Mojawapo kati ya magonjwa yanayohusishwa na umaskini na uchafu wa kupindukia ni ugonjwa wa Kipindupindu. Inaripotiwa kuwa Kipingupindu ni miongoni mwa magonjwa ambayo huathiri jamii maskini zaidi kwa kiasi kikubwa hasa hasa kwenye nchi zinazoendelea, kiasi kwamba Shirika la Afya Duniani (WHO) limeuweka ugonjwa huu kama mojawapo ya viashiria vya maendeleo ya jamii husika.

Kwanini nchi zinazoendelea ndizo zinazokumbwa na ugonjwa huu?

Moja wapo ya changamoto zinazokabili nchi zinazoendelea ni jamii kutokuwa na uhakika wa kupata Maji safi na salama, pamoja na kutokuwa na mazingira safi kwa ujumla. Ndio maana mpaka leo nchi zinazoendelea ndizo zinazokumbwa na mlipuko wa kipundupindu au huwa katika hatari ya mlipuko wa ugonjwa huo.

Kipindupindu husababishwa na nini?

Ugonjwa huu hutokana na maambukizi katika utumbo mdogo wa binadamu uletwao na vimelea vya bacteria vijulikanavyo kitaalamu kama Vibrio cholerae.

Jinsi unavyoweza kuambukizwa

Kwa kawaida vimelea hawa hupendelea kuishi katika kinyesi cha binadamu. Mtu anaweza kuambukizwa ugonjwa huu kwa kunywa maji ama chakula kilichochafuliwa na kinyesi chenye vimelea hivi vya kipindupindu.

Mara baada kula chakula au kunywa maji yaliyochafuliwa, baadhi ya vimelea hivi huuwawa kwa tindikali iliyopo kwenye tumbo (stomach) pindi chakula au maji haya yanapoingia tumboni. Hata hivyo baadhi ya vimelea hawa hufanikiwa kukwepa ukali wa hii tindikali na hivyo kuendelea kuishi.

Vimelea waliofanikiwa kuepukali tindikali ya tumbo la binadamu, hujongea kwenda kwenye ukuta wa utumbo mdogo kwa kutumia ‘maumbo’ maalum yaliyo kwenye miili ya ambayo huwawezesha kusafiri ama kwa kitaalamu huitwa flagella. Wawapo kwenye ukuta wa utumbo mdogo Vibrio cholerae hutoa sumu iitwayo CTX au CT (cholera Toxin) ambayo husababisha mtu kuharisha choo chenye majimaji, papo hapo kuendelea kutoa kizazi kingine cha vimelea hao nje kwa njia ya haja kubwa.

Iwapo choo hicho cha mtu aliyeambukizwa kipindupindu kitachanganyika na chanzo cha maji au chakula, watu wengine huambikzwa kirahisi. Hali kadhalika iwapo ni kwenye choo ambacho hakipo kwenye mazingira ya usafi kuna hatari ya choo cha mwambukizwa kuchanganyika na chanzo cha maji au chakula na hivyo kupelekea watu wengi zaidi kuambukizwa ugonjwa huu.

Dalili za kipindupindu ni zipi?

Dalili za mwanzo kabisa za kipindupindu ni

• Kuanza Kuharisha ghafla choo chenye majimaji (ambacho rangi yake ni kama maji ya mchele) na chenye harufu mbaya kama shombo ya samaki.
• Kutapika

Aidha mgonjwa wa kipindupindu huonesha dalili zakupungukiwa maji mwilini kama vile

• ngozi huwa kavu,
• midomo kukauka,
• mgonjwa kuhisi kiu kikali,
• machozi kutoweza kutoka,
• kupata mkojo kidogo sana,
• Kuishiwa nguvu na kujisikia mchovu sana.
• Macho kutumbukia ndani hasa kwa watoto.

Vipimo vya utambuzi wa Kipindupindu

Kwa kawaida kipindupindu huweza kugunduliwa na kutambuliwa kwa kutumia dalili. Hata hivyo ili kuthibitisha kuwa mlipuko uliotokea ni kweli kipindupindu, vipimo vifuatavyo huweza kufanyika;

Kupima damu kwa ajili ya kuotesha vimelea vya kipindupindu maabara.
Kuchunguza choo kwa kutumia darubini (dark field microscope) ambapo vimelea hivi vya V. cholerae huweza kuonekana. Vile vile choo hiki hutumika kuotesha vimelea vya v. cholerae kwa ajili ya utambuzi zaidi.

Tiba ya Kipindupindu

Lengo kuu katika kutibu kipindupindu ni kurejesha maji na madini ambayo mgonjwa wa kipindupindu hupoteza kwa wingi baada ya kuharisha na kutapika.

Njia kuu zitumikazo katika kumrejeshea mgonjwa wa kipindupindu maji na madini aliyopoteza ni kwa kumpatia maji maalum yenye madini hayo kwa njia ya mdomo, yaani kwa kumpa anywe au kwa njia ya mshipa wa damu ambayo kitaalamu huitwa intravenously (i.v).

ORS
Pamoja na ORS hiyo ambayo imetengenezwa na kuwekwa kwenye paketi tayari kwa matumizi, Shirika la afya duniani (WHO) limetoa pia mwongozo wa kutengeneza maji yenye madini yanayohitajika mwilini (oral rehydration fluid) ambao ni rahisi na usio na gharama.
ORS ya kutengeneza nyumbani kwa kadiri ya muongozo huo huitaji kuchanganya na
• Lita moja ya maji safi na salama,
• Changanya na vijiko vidogo vinane vya sukari, kisha
• Ongeza na kijiko kidogo kimoja cha chumvi
• Aidha, unaweza kuongeza nusu glasi ya juice ya machungwa au nusu ya ndizi (tunda) lilipondwapondwa kwa kila lita, ili kuongeza madini ya potassium na pia kuboresha ladha.

Kwa wagonjwa wenye hali mbaya na wale wasioweza kunywa wenyewe, hupewa maji yenye madini mbambali kwa njia ya mshipa wa damu. Maji haya huitwa kitaalamu kama Ringer’s Lactate.

Mwongozo wa kufuata katika kutibu kipindupindu

Baada wa mgonjwa kuwasili katika kituo cha afya, hupimwa kiwango cha upungufu wa maji kilichopo mwilini.

Kisha muhudumu wa afya husahihisha upungufu wowote wa maji utakaonekana kwa awamu mbili. Kwanza kwa kati ya masaa 4-6 ya kwanza tangu kuwasili kituoni na kuendelea mpaka hali ya kuishiwa kwa maji mwilini itakapoonekana imekwisha.

Mhudumu wa afya hutakiwa kurekodi kwenye cheti maalum kiasi cha maji anayokunywa mgonjwa na kiasi cha mojo anachokojoa.

Njia ya mshipa hutumika pale tu, hali ya mgonjwa inapokuwa mbaya sana au pale ambapo mgonjwa hawezi kunywa chochote mwenyewe. Aidha kiasi cha maji kitolewacho kwa njia hii ya mshipa wa damu hwa ni kati ya 50-100 mL kwa kilo za uzito wa mgonjwa kwa saa.

Baada ya hapo, mgonjwa huendelea kupewa ORS anywe kwa kiwango cha 800 mpaka lita moja kwa saa.

Matumizi ya dawa katika kutibu kipindupindu

Ieleweke kuwa tiba sahihi na makini ya ugonjwa huu wa kipindupindu ni kumrejeshea mgonjwa maji na madini aliyopoteza wakati wa kuharisha na kutapika kwa njia ambazo zimeelezwa hapo juu. Matumizi ya dawa (antibayotiki) husaidia tu kufupisha muda wa kuwatoa wadudu na wala yasitumike kama tiba kuu ya ugonjwa huu.

Baadhi ya dawa ambazo hutumika katika matibabu ya ugonjwa huu ni Azithromycin na Tetracycline.

Jinsi ya kuzuia kipindupindu

Mara kwa mara serikali na taasisi zake zimekuwa zikihimiza watu jinsi ya kujikinga na ugonjwa huu wa kupindupindu. Miongoni mwa njia zinazofaa katika kuzuia milipuko ya ugonjwa huu ni
Upatikanaji wa maji safi na salama, watu hawana budi kuhakikisha kuwa maji ya kunywa yanachemshwa vyema kabla ya kuyanywa. Vile vile wanaweza kutumia chlorine katika maji ambayo huua vimelea hawa wa V. cholerae.

Ni muhimu kunawa mikono baada ya kutoka chooni na kabla ya kula

Tunashauriwa kufunika chakula kikiwa mezani ili nzi wasitue juu yake

Inashauriwa kujenga choo umbali wa angalau mita 30 kutoka chanzo cha maji
Inashauriwa kwa wasafiri watokao nchi zilizoendelea kupata chanjo iitwayo Dukoral, pindi wanaposafiri kwenda nchi zinazoendelea.


Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Mambo ya Msingi kuyajua kuhusu Ugonjwa wa Kipindupindu;

a.gif Hizi ndizo faida za kiafya za kuota jua

Kuna mambo ambayo huwa tunayachukulia ya kawaida na wala hatuko tayari kufahamu umuhimu wake. Jua ni kitu mojawapo ambacho huwa tunakiona kila siku, lakini ni mara chache tumelichunguza… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kujisaidia unapotokwa na damu Puani

Unapotokwa na damu puani fanya yafuatayo;
1. Simama wima na inamisha kichwa kwa mbele, kusimama itakusaidi kupunguza kasi na presha katika mishipa ya damu puani wakati unapoinamisha kichwa kwa mbele huzuia kumeza damu ambayo italeta shida tumboni… endelea kusoma

a.gif Madhara ya kutumia dawa za kuzuia mimba wakati wa hatari

Watu wengi hasa vijana watakuwa wanafahamu dawa ambazo hutumiwa sana kuzuia ujauzito pale ambapo wapenzi wamejamiiana ndani ya siku za hatari. Ninazungumzia dawa za kuzuia mimba sio dawa za kupanga uzazi. Dawa hizi zipo za aina nyingi ambazo zitozitaja hapa siku ya leo. Endapo wawili hawa wanakuwa hawapo tayari kupata mtoto, na wanaona kwamba siku walizojamiiana zitapelekea mwanamke huyo kutunga mimba, basi anaweza kutumia dawa hizi ambazo zinaharibu mazingira au uwezekano wa mimba kutungwa… endelea kusoma

a.gif Suluhisho rahisi la nguvu za kiume hili hapa

NI muujiza! Pengine hivyo ndivyo yeyote anaweza kusema pindi akisikia kwa mara ya kwanza juu ya namna mihogo mibichi na nazi kavu maarufu kama mbata vinavyoweza kuwasaidia watu kiafya, na hasa wanaume… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kujisaidia unapopatwa shambulio la moyo ukiwa pekeyako

Tafadhali chukua walau dk 2 kusoma hii:.. endelea kusoma

a.gif Matumizi ya Tangawizi kutibu shinikizo la chini la damu

Hatua za kufuata.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika Mkate wa sinia

Unga wa mchele (rice flour 2 vikombe vya chai)
Sukari (sugar 3/4 ya kikombe cha chai)
Hamira (dried yeast 3/4 kijiko cha chakula)
Hiliki (cardamon powder 1/2 kijiko cha chai)
Ute wa yai 1(egg white)
Tui la nazi (coconut milk kikombe 1 na 1/2 cha chai)
Mafuta (vegetable oil).. endelea kusoma

a.gif Faida za kiafya za Kula Matunda

Matunda yote yana faida mwilini kiafya lakini matunda yanatofautiana kifaida. Zifuatazo ni faida za kula matunda ya aina Mbalimbali;.. endelea kusoma

elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

.

uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png
UJUMBE-WA-SHUKRANI-KWA-NDUGU.JPG
elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.