.

πŸ‘‰ LISHE BORA KWA WATU WENYE AFYA NZURIπŸ‘‡βœ”

images-13.jpeg

Imehaririwa na; Melkisedeck Leon Shine. Tarehe 27 Mar 2015 17:59. [Legal & Authority]


LISHE BORA KWA WATU WENYE AFYA NZURI

β€’ Kula chakula bora kunamaanisha kula vyakula aina tofauti ya vyakula kila siku kama vile matunda, mboga, maziwa na aina ya vyakula vyenye asili ya nyama wa kufuga kama kuku, mbuzi, ngombe, samaki na na vyakula vya nafaka.

β€’ Lishe bora linamaanisha pia kula chakula ambacho hakina mafuta mengi, sukari au chumvi nyingi

β€’ Zingatia angalau vyakula vya nafaka kama vile mtama, mahindi, mchele, ngano, wimbi, ndegu, njegere. n.k

β€’ Ni bora kula matunda mengi kama β€˜maembe, ndizimbivu, papai, pera, chungwa, ubuyu, nanasi, pesheni, zambarau” na mbogamboga kama vile β€œmchicha, majani ya mboga, karoti, nyanya chungu, nyanya, mkunde, biringanya” mara tano kwa siku.

β€’ Kama mboga na matunda hazipatikani ni bora kununua zile ambazo zimehifadhiwa tayari kwenye mikebe au zile ziko kwenye jokofu (friji).

β€’ Punguza kula vyakula ambavyo vinapikwa kwa mafuta mengi na chumvi nyingi

β€’ Lishe bora hukusaidia wewe na jamii yako kuishi vyema, kuwa na afya bora, kufanya kazi vizuri na kwa bidii, shuleni na hata kucheza.

πŸ™‰πŸ™‰πŸ™‰Usisahau kushare posti hii kuhusu (LISHE BORA KWA WATU WENYE AFYA NZURI).πŸ‘ Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasomeπŸ’―βœ”


kj.gif

.

.

b.gif

Mimi ni Melkisedeck Shine Mmiliki, Mwandishi /Mhariri. Karibu tena kila siku.

Blog nyingine maarufu ndani ya AckySHINE.com

| Vichekesho | Videos | Picha | Ujasiriamali | Mahusiano | Kilimo & Mifugo | Katoliki | Afya & Mapishi | Hadithi | Misemo | SMS