Lifahamu tatizo la maumivu chini ya kitovu

By, Melkisedeck Shine.

picha-kali.png

Lifahamu tatizo la maumivu chini ya kitovu

Tatizo hili huwakumba watu wengi sana kwenye jamii yetu lakini kwa bahati mbaya watu wengi huchukulia ni jambo la kawaida kitu ambacho baadae hupelekea watu wengi kuingia kwenye matatizo makubwa ya kiafya hasa kwenye mfumo wa uzazi na mfumo wa chakula.

Maumivu Chini Ya Kitovu Hutokea Kama Ifuatavyo:

Yapo yale ya chini ya kitovu katikati, kushoto na kulia. Kwa wanawake maumivu ya kushoto na kulia yapo ya aina mbili. Kuna yale ambayo yanakuwa upande mmoja lakini husambaa kwa urefu wa sentimita mpaka nne na inaweza ikawa upande mmoja au pande zote mbili lakini yapo mengine chini ya kitovu ambayo yanaweza yakawa upande mmoja au pande zote mbili bila kusambaa kwa marefu.

Kuna maumivu mengine chini ya kitovu huwapata wanawake wakati tu wanaposhiriki tendo la ndoa kwa ndani ya uke au chini ya kitovu. Pia yapo ambayo huwapata wanawake wakati wameinama, wakati wa kunyanyua vitu vizito, wakati wa kucheka au kuimba na wakati mwingine wakiwa wamelala kifudifudi.

Maumivu chini ya Kitovu Yanaashiria Matatizo Gani Kwa Wanawake?

Mirija ya uzazi kujaa maji mazito na machafu ambayo huzuia yai kutembea kwenye mirija ya uzazi. Mwanamke ambaye amewahi kuambiwa na daktari kwamba anatakiwa asafishwe kizazi chake/mirija ya uzazi na wakati huo huo anasikia maumivu chini ya kitovu kushoto na kulia au upande mmoja kuna uwezekano akawa na tatizo la mirija ya uzazi kuziba kutokana na kujaa maji machafu.

Kutokukomaa kwa mayai ya uzazi. Hii husababisha vifuko vya mayai ya uzazi kuvimba(ovaritis) na kumletea mwanamke maumivu chini ya kitovu mithili ya kichomi. Mwanamke ambaye anamaumivu chini ya kitovu na wakati huo huo ana matatizo ya hedhi mfano hedhi kukoma au kutokuwa na mpangilio maalum kunauwezekano mkubwa akawa na tatizo la vifuko vyake vya mayai ya uzazi kutokomaza mayai na hivyo mayai kutotoka kwenye vifuko hivyo na kusababisha kuvimba na hatimaye kumsababishia mwanamke maumivu makali mithili ya kichomi.

Kuvimba kwa kuta za mji wa mimba na kuta za mirija ya uzazi (PID/Pelvic Inflamatory Disease). Mwanamke anayesikia maumivu chini ya kitovu katikati na pembeni kwa wakati mmoja na wakati huo huo akawa anatokwa na uchafu mzito mithili ya maziwa mtindi kunauwezekano akawa na PID hasa hasa kama amewahi kukumbwa na tatizo la kuharibika kwa mimba kabla haijafikisha miezi mitano.

Afya mbovu ya kibofu cha mkojo ikiambatana na matatizo ya maambukizi kwenye mfumo mzima wa mkojo (UTI). Maumivu chini ya kitovu yanayohusisha afya mbovu ya kibofu cha mkojo huambatana na mgonjwa kutoa haja ndogo kidogo sana ila mara kwa mara.

Maumivu chini ya kitovu kwa wanaume huashiria nini?

Maumivu chini ya kitovu kwa wanaume huashiria pia tatizo la tezi dume liitwalo Prostatitis yaani kuvimba kwa tezi dume. Maumivu haya hujikita kwenye shina la uume na huashiria tatizo hili hasa kama mwanaume anakwenda haja ndogo mara kwa mara nyakati za usiku na umri ukiwa unaelekea miaka 50 au zaidi.

Dalili nyingine ambatano ni kutoa haja ndogo ambayo ina kasi ndogo sana tofauti na kawaida, ikiambatana na maumivu ya kiuno na mgongo, kuvimba kwa korodani, haja ndogo inayoambatana na usaha na damu, maumivu ya uume wakati wa kufika kileleni, na damu katika maji ya uzazi (semen)
Kwa wanaume, maumivu haya ya chini ya kitovu huashiria pia tatizo ambalo kitaalamu hujulikana kwa jina la Hernia ambapo waswahili tunaita ngiri.

Mwanaume anaposikia maumivu haya ya chini ya kitovu ikiambatana na maumivu ya korodani, korodani moja kupungua na nyingine kukua zaidi au zote mbili kukua au kupotea, ni dalili ya ugonjwa huu ambao huharibu ubora wa uzalishwaji wa mbegu za kiume ambazo zaweza kuzalishwa chache au ambazo hazina kasi ya kutosha kusafiri kwenye via vya uzazi vywa mwanamke na hivyo mwanaume kupoteza uwezo wake wa kutungisha mimba.

Maumivu chini ya kitovu kwa wanaume kama ilivyo kwa wanawake huashiria tatizo la maambukizi katika mfumo wa haja ndogo yaani (Urinary Track Infection/UTI) ambapo dalili zake ni kama zile za mwanamke hapo juu.

Vipimo na tiba vyahitajika mapema bila kuchelewa ili kuepuka madhara makubwa katika mfumo wa uzazi, mkojo na hata wa chakula


Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Lifahamu tatizo la maumivu chini ya kitovu;

a.gif Hizi ndizo sababu kwa nini ule Tende kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Kitaalamu chakula unachokula leo ndio kinaamua hali ya afya yako kwa siku za usoni. Na ni muhimu sana kuzingatia ulaji bora wa chakula na si kula ilimradi umekula. Wataalamu wa lishe wanatuambia kuwa ulaji unaofaa hutokana na kula chakula mchanganyiko kulingana na wakati… endelea kusoma

a.gif Vyakula vinavyofaa kuliwa katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Vyakula vinavyofaa kuliwa wakati huu wa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni vingi, leo tutaanza kuchambua kimoja baada ya kingine, Mbali na Waislamu, uchambuzi huu unawafaa pia wale ambao siyo Waislamu. Chakula kilichozoeleka zaidi kwa futari ni tende. Baada ya kushinda kutwa nzima na Swaumu, kiwango cha sukari ya mwili hupungua na hivyo, kuhitaji kujazilizwa tena. Aina ya kwanza ya sukari itumikayo mwilini na hasahasa ubongoni ni glukosi… endelea kusoma

a.gif Mambo ya Muhimu kufahamu kuhusu tatizo la mgongo wazi

Uti wa mgongo ulio wazi( Spinal bifida) ni hali ambayo mtoto anazaliwa nayo huku uti wa mgongo (mishipa ya fahamu mkubwa unaotoka kwenye ubongo) ukiwa wazi kutokana na mifupa (vipingili vya uti wa mgongo) kutokufunga vizuri… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya Dengu (Dengue fever)

Ugonjwa wa dengue ni tishio la ugonjwa hatari linaongezeka siku hadi siku. Dengue ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyoenezwa na mbu aitwae aedes… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika Pilau Ya Nafaka Na Nyama Ya Kusaga

+Viambaupishi.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Wali Wa Kichina Wa Kuku Na Mboga Mchanganyiko

Mchele wa basmati/pishori - 4 vikombe vikubwa (mugs).. endelea kusoma

a.gif Vyakula vinavyosaidia kuongeza kinga ya mwili

Watu wengi tumekuwa tukijali kazi zetu za kila siku bila kujali hali ya afya zetu matokeo yake kumekuwa na ongezeko kubwa la vifo vya ghafla. Suala la kula pengine ndilo nguzo ya kwanza ya afya ya binadamu. Mwili ukiwa sawia bila shaka utaweza kufanya mambo yako yote, na usipokuwa sawa basi hutaweza kutimiza lengo lako lolote! Hivi ni vyakula kadhaa vinavyoweza kukusaidia kuongeza kinga ya mwili wako.. endelea kusoma

a.gif Kampeni ya utunzaji wa vyanzo vya maji

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.
Lengo la kampeni Hii ni kuhamasisha watu kutunza vyanzo vya maji kwa manufaa yao ya sasa na kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Kampeni hii inaamini kuwa vyanzo vya maji vikitunzwa vizuri vinaweza kuwa msaada kijamii, kiuchumi na kimazingira kwa kizazi hiki na kizazi kijacho… endelea kusoma

uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png

.

picha-kali.png
KUKUTANA-MPENZI-FG94T.JPG
elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.