Jinsi ya kutibu tatizo la kukosa choo bila kutumia dawa

By, Melkisedeck Shine.

Kukosa choo ni tatizo kubwa katika jamii zetu japo huwa halionekani kama ni tatizo. Hata hivyo kuna vyakula ambavyo vinapatikana kwa urahisi na vinasaidia kutibu tatizo la kukosa choo kwa njia rahisi kabisa.

Kwa kawaida mtu mwenye afya njema anatakiwa kwenda chooni angalau mara tatu kwa siku, lakini si ajabu kusikia mtu hajaenda chooni siku tatu na tunaona ni kawaida sana kwenda chooni mara moja kwa siku.

Tatizo la kukosa choo (Constipation) linatokana na chakula tunachokula kuchelewa kuunguzwa tumboni hivyo kuchukua muda mrefu katika mfumo wa usagaji.

Tatizo hili linasababishwa na mfumo wa chakula kukosa baadhi ya mahitaji ili kufanya kazi yake ya usagaji. Vitu hivi ni maji na vyakula vya fiba(Vyakula vyenye nyuzinyuzi) ambavyo ni muhimu sana kuharakisha zoezi la usagaji wa chakula tumboni.

Vifutavyo ndivyo vyakula ambavyo husaidia kutibu tatizo la kukosa choo.

Tende

Tende zikiwa kavu au kama juisi inasaidia kuondoa tatizo la kukosa choo. Tende zina fiba kwa wingi hivyo kusaidia zoezi la usagaji chakula tumboni. Pia Tende zina kemikali ya sorbitol–aina ya sukari ambayo inatajwa kusaidia usagaji chakula.

Maji

Kunywa maji kwa wing kunasaidia kutibu tatizo la kukosa choo kwa kuwa maji yanahochea usagaji wa chakula na kufanya choo kuwa laini. Fiba zinahitaji maji ili kufanya kazi ya kufagia uchafu tumboni na maji yanapokosekana hunyonya toka katika uchafu tumboni na kufanya choo kuwa kikavu na kusababisha ugumu wa kutoka.

Wataalamu wa afya wanashauri kunywa glasi 6 mpaka 8 za maji kila siku( Lita 1-2 kwa siku)

Kama kunywa maji ni ngumu kwako basi jaribu kuweka vipande vya matunda kama ndimu ,limao,tikiti maji na aina nyingine ya matunda.

Kahawa na Vinywaji Vingine vya Moto

Kahawa na vinywaji vingine vya moto husaidia kusukumwa kwa chakula tumboni na kupata choo.

Matumizi ya muda mrefu ya kahawa yanaweza pia yakaongezea tatizo. Kama unatumia kahawa kwa wingi unashauriwa kunywa maji mengi pia,vinginevyo itaongezea tatizo la kukosa choo

Ulaji wa Matunda au Saladi

Matunda yanasaidia kutibu tatizo la kukosa choo kwa vile yana fiba kwa wingi. Lakini matunda yanasaidia kuongeza maji maji hasa matunda kama matikiti.

Pia ulaji wa matunda ni muhimu kuzingatia muda wa kula, ni vyema kula matunda saa moja au dakika 30 kabla au baada ya chakula. Kula matunda mara baada ya kula kama wengi wanavyofanya ni makosa na kunakukosesha faida zinazotarajiwa.

Ulaji wa Mboga za Majani

Mboga za majani kama ilivyo matunda ni chanzo kizuri cha faiba ambazo ni muhimu sana katika usagazi na usukumaji wa chakula.

Mchicha, Spinachi,karoti na mboga mboga nyingine ni muhimu kuwepo katika chakula cha kila siku.

Maharage na aina nyingine za kunde kunde pia zina fiba kwa wingi na zinasaidia kupunguza tatizo.

Mazoezi Husaidia Kutibu Tatizo la Kukosa Choo Pia:

Ukiachia vyakula,ufanyaji mazoezi au kazi zinazoshughulisha mwili zinazaidia kuzuia na kutibu tatizo la kukosa choo.

Kufanya mazoezi kila siku angalau kwa dakika 30 ni jambo linalowezekana kama utalipa muda na kuweka katika ratiba zako. Mazoezi rahisi kabisa ni kukimbia (jogging) na pia hushughulisha mwili mzima(Total Body Exercise).

Ukiachia kutibu tatizo la kukosa choo pia mazoezi yanasaidia kuzuia magonjwa mengine mengi kama presha na kisukari.

Kama unasumbuliwa na tatizo la kukosa choo au unamfahamu mtu mwenye shida hii basi mshilikishe na ajaribu kufuta maelekezo kama yalivyotolewa hapa ili kuweza kutibu tatizo la kukosa choo kwa kupangilia vyakula tu unavyokula kila siku.KADI-SALAMU-MCHANA-JION.JPG

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Jinsi ya kutibu tatizo la kukosa choo bila kutumia dawa;

a.gif Mambo ya msingi kufahamu kuhusu uotaji wa meno kwa mtoto

Mtoto wako atakapofikisha miezi sita, ataanza kuota meno. Watoto wengi wanapotaka kuota meno humwaga mate sana na hutaka kutafunatafuna vitu. Wakati mwingine watoto hutapika au kuhara wakiota meno… endelea kusoma

a.gif Vyakula 7 vya kuepuka kula ili uwe na afya nzuri

Inasemwa kuwa “wewe ni kile unachokula” kwa kumaanisha kuwa mwonekano wetu na afya ya mwili na akili unajengwa na chakula tunachokula. Madhara ya chakula chetu tunachotumia yako pia katika ngozi. Kuna vyakula vinavyozeesha ngozi kwa haraka na ni budi kuvijua na kuviepuka… endelea kusoma

a.gif Madhara ya kubana mkojo muda mrefu

Utakubaliana na mimi kwamba, kitendo cha mtu kubanwa na haja ndogo siyo kitu cha hiyari kwamba sasa mtu anaamua ngoja nibanwe na mkojo, hili ni jambo la asili na ni matokeo ya vyakula, matunda au vinywaji tunavyotumia. Kwa lugha nyingine tumekuwa tukiita kuwa ni wito wa asili au nature’s call… endelea kusoma

a.gif Faida 6 za kula karoti kiafya

Asilimia kubwa tunapenda kutumia karoti katika kuunga katika mboga ya nyama na si kuila karoti kama karoti. wataalamu wanashauri ili uwe na afya bora unatakiwa ule karoti sita kwa wiki au moja kwa siku. Unaweza kula karoti ya kuchemshaa,juisi au mbichi… endelea kusoma

[Kitendawili Kwako] 👉Mwenyewe hana uti wa mgongo

[Chemsha Bongo Kwako] 👉Je, hii familia ina watoto wangapi?

KADI-MZAZI-ASUBUHI.JPG

a.gif Jinsi ya kupika Vileja

VIPIMO.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Ugali na dagaa

Dagaa (dried anchovies packet 1)
Unga wa ugali (corn meal flour 1/4 kilo) (unaweza kutumia unga wa choice uipendayo)
Nyanya ya kopo (tin tomato 1/2)
Kitunguu maji (onion 1)
Limao (lemon 1/4)
Pilipili mbuzi nzima bila kukata (scotch bonnet pepper1, do not chop)
Chumvi (salt 1/4 ya kijiko cha chai)
Mafuta (vegetable oil)
Hoho (green pepper).. endelea kusoma

a.gif Vitu vinavyoweza kusababisha tatizo la mbegu chache na ugumba kwa ujumla kwa wanaume

Vifaa vingi vya kisasa vya kieletroniki vinasababisha kushuka kwa wingi na ubora wa mbegu kwa wanaume wengi miaka ya sasa kwani mionzi yake hupelekea joto lisilohitajika katika mifuko ya mbegu za kiume. Vifaa hivi ni pamoja na simu na Kompyuta… endelea kusoma

a.gif Madhara ya kunywa pombe wakati wa ujauzito

Kuacha Matumizi ya pombe wakati wa ujauzito ni moja ya njia ya kuzuia kupata matatizo ya kuzaliwa nayo na udhaifu kwa mtoto. Pia kuna matatizo kadhaa yanaweza kutokea kwa kichaga kutokana na matumizi ya pombe wakati wa ujauzito… endelea kusoma

[Picha Nzuri] 👉Huyu ndiyo fundi wa admini

[Msemo wa Leo] 👉Kushindwa jambo sio Makosa

[Jarida la Bure] 👉Mapishi ya wali wa karoti na nyama

Usipitwe na Nafasi za kazi kwa leo

<<Bofya HAPA kujua zaidi>>

.

utotoni.gif
rafiki.gif

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.