AckySHINE Afya na Mapishi Β» Jinsi ya kutengeneza Visheti Vyeupe Na Vya Kaukau

Tafuta

πŸ‘‰ Jinsi ya kutengeneza Visheti Vyeupe Na Vya KaukauπŸ‘‡βœ”

VIAMBAUPISHI

Unga - 4 Vikombe vya chai

Siagi - 1 Kikombe cha chai

Hiliki Β½ Kijiko cha chai

VIAMBAUPISHI:SHIRA

Sukari - 2 Vikombe vya chai

Maji - 1 Kikombe cha chai

Vanilla Β½ Kijiko cha chai

(cocoa ukipenda kugawa visheti aina mbili) 2 Vijiko vya chai.

JINSI YA KUTENGENEZA

Tia unga kwenye bakuli pamoja na siagi na hiliki.
Changanya vizuri isiwe na madonge.
Tia maji baridi vikombe viwili kasoro vya chai changanya ukiona bado ongeza maji kidogo, iwe kama chapati usikande uchanganye tu.
Halafu utakata sampuli unayopenda mwenyewe.
Unaweka karai ya mafuta yakisha kupata moto unaanza kuchoma moto usiwe mkali sana, kiasi, baadae unaweza kuongeza moto na vikaange hadi viwe rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta. .
Ukipenda gawa visheti sehemu mbili, na shira pia igawe sehemu mbili
Changanya nusu ya visheti kwa shira nyeupe.
Nusu ya shira nyingine ibandike tena motoni na tia cocoa vijiko viwili vidogo vya chai.
Inapochanganyika cocoa vizuri changanya nusu ya visheti ulivyogawa kupata visheti vya shira ya cocoa.

πŸ™‰πŸ™‰πŸ™‰Usisahau kushare posti hii kuhusu (Jinsi ya kutengeneza Visheti Vyeupe Na Vya Kaukau).πŸ‘ Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasomeπŸ’―βœ”

Marafiki-wa-enzi.GIF

Expert available for Hire

Jinsi ya Kutana na Ndugu mliopotezana Anaweza akawa na yeye anakutafuta .
Soma%20Zaidi.gif