Mahitaji

Muhogo - 3

Tui La Nazi - 2 vikombe

Chumvi - kiasi

Pilipili mbichi - 2

Mafuta - 1 kijiko moja

Kitunguu maji - 1 kidogo

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Chambua muhogo ukatekate au tumia iliyo tayari.
Chemsha muhogo katika sufuria kwa maji kidogo na chumvi, funika uive muhogo.
Karibu na kukauka maji tia tui, kitunguu maji ulichokatakata na pilipili mbichi.
Unaupika moto mdogo mdogo hadi ukauke tayari kuliwa na samaki au kitoweo chochote kingine


Slide3-mliopoteana.GIF

πŸ™‰πŸ™‰πŸ™‰Usisahau kushare posti hii kuhusu (Jinsi ya kutengeneza Muhogo Wa Nazi Na Samaki Wa Kukaanga).πŸ‘ Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasomeπŸ’―βœ”

🍴 Makala nyingine za Dondoo za Afya & MapishiπŸ‘‡

A.gif

KUKUTANA-MPENZI-FG94T.JPG