AckySHINE Afya na Mapishi Β» Jinsi ya kutengeneza Biskuti Za Tende

Tafuta

πŸ‘‰ Jinsi ya kutengeneza Biskuti Za TendeπŸ‘‡βœ”

MAHITAJI

Unga - 4 Vikombe vya chai
Sukari ya laini (icing sugar) - 1 Kikombe cha chai
Baking powder - 2 Vijiko vya chai
Mayai - 2
Siagi au margarine - 1 Kikombe cha chai
Vanilla -1 Kijiko cha chai
Maziwa ya kuchanganyia - kiasi
Tende iliyotolewa koko - 1 Kikombe
ufuta (sasame) kiasi 1/4 kikombe

MAANDALIZI

Changanya unga, siagi, baking powder, na sukari katika mashine.
Kisha tia mayai, vanilla na halafu maziwa kidogo kidogo hadi mchanganyiko ushikamane.
Gawanya madonge mawili na usukume kama chapati, lakini sio nyembamba sana.
Tandaza tende robo ya duara na unyunyize ufuta duara zima: kisha kunja hadi mwisho na ukate kate, kisha upange katika trei ya kuvumbika.
Vumbika (bake) moto wa 350Β°F kwa muda wa dakika 20 au hadi vigeuke rangi na viwive.
Zikisha iiva ziache zipowe na zitakuwa tayari kuliwa.

πŸ™‰πŸ™‰πŸ™‰Usisahau kushare posti hii kuhusu (Jinsi ya kutengeneza Biskuti Za Tende).πŸ‘ Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasomeπŸ’―βœ”

Hapa unaweza kutafuta ndugu zako mliopotezana Wanakutafuta kwenye mtandao

πŸ‘‰Jua Zaidi...


"Katika maisha, kinga kuu ya magonjwa na majanga yote ni kujikatalia au kujinyima."

wadogo.gif

Expert available for Hire