Jinsi ya kutengeneza Biskuti Za Tangawizi

By, Melkisedeck Shine.

familia-mapenzi-na-mahusiano.png

Jinsi ya kutengeneza Biskuti Za Tangawizi

MAHITAJI

Unga - 2 Vikombe

Cocoa ya unga - 1 Kijiko cha supu

Sukari ya hudhurungi - 1 Kikombe

Siagi - ¾ Kikombe

Yai - 1

Molasses - ¼ Kikombe

Baking soda - 2 vijiko vya chai

Mdalasini wa unga - 1 kijiko cha chai

Tangawizi mbichi - 1 kijiko cha supu

Karafuu ya unga - ½ kijiko cha chai

Chumvi ½ kijiko cha chai

Vanilla ½ kijiko cha chai

MAANDALIZI

Katika bakuli, chunga unga, baking soda, chumvi na cocoa. Weka kando.
Washa oven lipate moto huku unatayarisha biskuti.
Katika bakuli jengine, mimina siagi na sukari upige kwa mashini ya keki hadi mchanganyiko uwe laini kama dakika mbili.
Mimina molasses na yai ndani ya mchanganyiko wa siagi na sukari uchanganye vizuri.
Mimina unga kidogo kidogo huku unachanganya na mwiko hadi unga wote umalizike.
Mimina mdalasini, karafuu na tangawizi, changanya vizuri.
Weka mchanganyiko wako ndani ya friji kama masaa mawili. (Ukipenda unaweza kuhifadhi mchanganyiko wako ndani ya mfuko wa freezer na uoke siku nyengine.)
Tengeneza viduara vidogo vidogo.

Chovya kila kiduara katikati sukari, kisha panga kwenye treya ya kuoka

Rudisha viduara katika friji kama nusu saa.

Oka katika oven 350ºF kwa muda wa dakika 15.

Toa biskuti kwenye oven na uache zipoe kama dakika kumi.
Panga kwenye sahani tayari kuliwa.


Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Jinsi ya kutengeneza Biskuti Za Tangawizi;

a.gif MAPISHI YA LADU

Unga - 6 vikombe.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kutengeneza Biskuti Za Cornflakes

Unga - 1 Kikombe.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kutengeneza Biskuti Za Tende

Unga - 4 Vikombe vya chai
Sukari ya laini (icing sugar) - 1 Kikombe cha chai
Baking powder - 2 Vijiko vya chai
Mayai - 2
Siagi au margarine - 1 Kikombe cha chai
Vanilla -1 Kijiko cha chai
Maziwa ya kuchanganyia - kiasi
Tende iliyotolewa koko - 1 Kikombe
ufuta (sasame) kiasi 1/4 kikombe.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kuandaa Vileja Vya Tambi

Tambi (vermiceli Roasted) Mifuko 2.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kutengeneza Biskuti Za Tende

Unga - 4 Vikombe vya chai
Sukari ya laini (icing sugar) - 1 Kikombe cha chai
Baking powder - 2 Vijiko vya chai
Mayai - 2
Siagi au margarine - 1 Kikombe cha chai
Vanilla -1 Kijiko cha chai
Maziwa ya kuchanganyia - kiasi
Tende iliyotolewa koko - 1 Kikombe
ufuta (sasame) kiasi 1/4 kikombe.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kutengeneza Rock-cakes Za Njugu Na Matunda Makavu

Unga - 4 Vikombe.. endelea kusoma

a.gif MADHARA YA SHISHA

Yafuatayo ni madhara ya shisha;.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika Roast ya biringanya na mayai

Mara nyingi biringanya hutumika kama kiungo cha nyongeza katika mchuzi. Hata hivyo, kiungo hiki kinaweza kupikwa chenyewe na kutoa mchuzi wenye ladha ya kipekee… endelea kusoma

familia-mapenzi-na-mahusiano.png

.

elimu-sayansi-na-tekinolojia.png
UJUMBE-KUOMNBA-KUKUTANA-NA-NDUGU.JPG
picha-kali.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.