Jinsi ya kupika Wali Wa Kichina wa mboga mboga Na Mayai

By, Melkisedeck Shine.

elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

Jinsi ya kupika Wali Wa Kichina wa mboga mboga Na Mayai

Viambaupishi

 1. Mchele (Basmati) - 3 vikombe
 2. Mbogamboga za barafu (karot, njegere, spring beans na mahindi) - 1 kikombe
 3. Kuku Kidari - 1 LB (ratili)
 4. Mayai - 2 mayai
 5. Vitunguu (vikubwa) - 2 au 3 vidogo
 6. Pili pili manga - 1 kijiko cha chai
 7. Paprika - 1 kijiko cha chai
 8. Chumvi - Kiasi
 9. Mafuta - 1/3 kikombe cha chai
 10. Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 kijiko cha supu
 11. Tangawizi - 1 kijiko cha chai
 12. Kidonge cha supu - 1
 13. Soy sauce - 2 vijiko vya supu

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Kuku

Kata kidari cha kuku vipande vidogo vidogo vya kiasi.

Tia mafuta kidogo katika wok (karai ya kichina)

Kisha mtie kuku, thomu, tangawizi, soy sauce, pilipilimanga, paprika chumvi.

Tia mboga za barafu, kidonge cha supu, kaanga kuku na mboga viwive yitu vyote na mchanganyiko ukauke.

Namna Ya Kutayarisha Na kupika Wali

Roweka mchele wa basmati kwa muda wa saa au zaidi.

Halafu chemsha mchele pamoja na chumvi

Wacha uchemke asilimia 70%

Chuja maji na weka kando

Katika sufuria, tia mafuta kidogo tu

Kisha tia mayai mawili ukaange haraka haraka (crumbled egg)

Changanya mchanganyiko wa kuku na mboga

Kisha tia wali changanye vizuri

Rudisha katika moto, funika upikike kidogo hadi uive

Kisha pakua katika sahani na tolea na mayai ya kuchemsha ukipenda.


Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Jinsi ya kupika Wali Wa Kichina wa mboga mboga Na Mayai;

a.gif Mapishi ya Wali Wa Zaafarani Na Kuku Wa Kupaka

Mchele - 3 Vikombe.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya wali mtamu Wa Nazi Kwa Maharage Na Samaki Nguru Wa Kukaanga

Mchele mpunga - 4 Vikombe.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika Biriyani Ya Nyama Ng'ombe

Nyama vipande - 3 LB.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Wali Wa Kichina Wa Kamba Na Kuku

Mchele wa pishori (basmati) - 4.. endelea kusoma

[Msemo wa Leo] 👉Matendo ya mtu

[Jarida la Bure] 👉Kijitabu cha Picha Kali

[Hadithi Nzuri] 👉Stori inayogusa!!

[SMS kwa Umpendaye] 👉Ujumbe wa kimahaba kwa umpendaye sana

a.gif Mambo usiyoyajua kuhusu ugonjwa wa Pumu

Asthma /pumu ni ugonjwa sugu ambao huathiri njia ya hewa ambazo huingiza na kutoa hewa katika mapafu, pia hufanya kuta za ndani ya njia ya hewa kuvimba na hivyo hupunguza kiasi cha hewa kinachoingia na kutoka ktk mapafu, Hali hii husababisha mgonjwa kutoa mlio kama wa filimbi/mluzi wakati wa kupumua, kifua kubana, kushindwa kupumua vizuri na kukohoa sana, watu wa pumu huwa na dalil hizo nyakat za usiku na asubuhi sana pia ugonjwa huu huwaathiri watu wa Rika zote ingawaje Mara nying huwaathiri watoto kwa sababu huanza utoton na hivyo takriban MILION 6 ya watoto wanaumwa pumu na watu takriban 255,000 hufa kila mwaka kwa ugonjwa huu… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya Dengu (Dengue fever)

Ugonjwa wa dengue ni tishio la ugonjwa hatari linaongezeka siku hadi siku. Dengue ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyoenezwa na mbu aitwae aedes… endelea kusoma

a.gif Virutubishi, kazi zake katika mwili na vyanzo vyake

ni viini vilivyoko kwenye chakula ambavyo vinauwezesha mwili kufanya kazi zake, karibu vyakula vyote huwa na kirutubishi zaidi ya kimoja ila hutofautiana kwa kasi na ubora. Kila kirutubishi kina kazi yake mwilini na mara nyingi hutegemeana ili viweze kufanya kazi yake kwa ufanisi. Hakuna chakula kimoja chenye virutubishi vya aina zote isipokuwa maziwa ya mama kwa miezi sita ya mwanzo ya maisha ya mtoto, ni mhimu kula vyakula vya aina mbalimbali ili kuwezesha mwili kupata virutubishi mchanganyiko vinavyohitajika… endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Haliym Ya Nyama Mbuzi -Bokoboko La Pakistan

Nyama ya mbuzi au ng’ombe ya mafupa - 2 LB.. endelea kusoma

picha-kali.png

.

uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png
Marafiki-wa-enzi.GIF
picha-kali.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.