Jinsi ya kupika Mseto Kwa Mchuzi Wa Samaki Wa Nazi

By, Melkisedeck Shine.

Vipimo vya mseto

Tanbihi: Kiasi ya vipimo inategemea wingi wa watu, unaweza kupunguza au kuongeza. Hiki ni kiasi cha watu 6 takriban.

Chooko - 3 Vikombe

Mchele - 2 Vikombe

Samli - 2 vijiko Vya supu

Chumvi - kiasi

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

Safisha na kosha chooko utoe taka taka zote.
Osha mchele kisha roweka pamoja na chooko kwa muda wa saa au zaidi.
Pika chooko na mchele ukiongeza maji inapohitajika, tia chumvi, funika pika moto mdogo mdogo huku unakoroga kwa mwiko kila baada ya muda huku unaponda ponda.
Karibu na kuwiva na kupondeka tia samli endelea kupika hadi karibu na kukauka. Epua.

Samaki

Vipande vya samaki (nguru) - 6 – 7 (4LB)

Kitunguu saumu na tangawizi iliyosagwa - 2 vijiko vya supu

Pilipili ya unga nyekundu - 1 kijiko cha supu

Pilipili mbichi iliyosagwa ukipenda - 1 kijiko cha chai

Bizari ya samaki - 1 kijiko cha chai

Chumvi - kiasi

Ndimu - kiasi

Mafuta ya kukaangia - kiasi

Namna Ya Kutaysha Na Kupika

Changanya thomu/tangawizi, pilipili, bizari, chumvi pamoja na ndimu iwe masala nzito.
Paka vipande vya nguru kwa masala hayo weka akolee dakika kumi hivi.
Kaanga vipande vya nguru katika mafuta madogo kwenye kikaango (fyring pan) uweke upande.

Mchuzi Wa Nazi

Vitunguu maji – katakata vidogodogo - 4

Nyanya zilizosagwa (crushed) - 3- 4

Nyanya kopo - 1 kijiko cha chai

Mafuta - 3 vijiko vya supu

Bizari ya mchuzi - 1 kijiko cha chai

Bamia zilizokatwa ndogo ndogo - 2 vikombe

Chumvi - kiasi

Ndimu - 2 vijiko vya supu

Tui la nazi - 3 Vikombe au 800 ml

Namna Ya Kupika

Katika karai au sufuria, tia mafuta ukaange vitunguu hadi vianze kugeuka rangi.
Tia nyanya zilizosagwa, nyanya kopo, uendelee kukaanga, kisha tia bizari, chumvi.
Tia nazi na mwisho tia bamia uache ziwive kidogo tu.
Tia vipande vya samaki vilivyokwisha kaangwa.
Tayari kuliwa na mseto upendavyo.

Vidokezo:

Bizari nzuri kutumia ni ya 'Simba Mbili' inaleta ladha nzuri katika mchuzi.
Ni bora kupika mchuzi kwanza kabla ya mseto kwani mseto ukikaa kwa muda unazidi kukauka.


KADI-POLE-MZAZI.JPG

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Jinsi ya kupika Mseto Kwa Mchuzi Wa Samaki Wa Nazi;

a.gif Mapishi ya Wali Wa Kichina Wa Kuku Na Mboga Mchanganyiko

Mchele wa basmati/pishori - 4 vikombe vikubwa (mugs).. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Wali Wa Nyanya Wa Kukaanga

Mchele basmati, pishori - 3 vikombe.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika Biriani ya Nyama Ng'ombe Na Mtindi

Mchele wa biriani - 5 gilasi.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kuandaa Ndizi Mbichi Za Supu Ya Nyama Ng’ombe

Ndizi mbichi - Kisia.. endelea kusoma

[Kitendawili Kwako] 👉Fimbo yangu nzuri iliotea kwenye miiba

[Fumbo Kwako] 👉Je, glass ina Maji kiasi gani?

KADI-PONGEZI-MZAZI.JPG

a.gif Ugonjwa wa kichomi

Kichomi ni moja ya dalili za ugonjwa moyo. Kupatwa kichomi mara moja moja si vibaya.
Ukipatwa muda mrefu au kila wakti ; basi …chunguza zaidi.
Kichomi husababishwa au kinaweza kuwa… endelea kusoma

a.gif Mapishi mazuri ya Wali Wa Kukaanga Kwa Kidari Cha Kuku

Vipimo vya Wali:.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kutengeneza Biriani Ya Nyama Ya Ng'ombe

Nyama - 2 Ratili (LB).. endelea kusoma

a.gif Soma hii Kabla hujafikiria kula nyama ya nguruwe tena

Hapa huwa kuna mvutano wa kidini sana juu ya nguruwe, Ila Leo napenda kuliweka sawa, kitaalamu kwa mujibu wa MEDICINE (Science)!!.. endelea kusoma

[Msemo wa Leo] 👉Hakuna uwezo Bila fursa.

[Jarida la Bure] 👉Kijitabu cha Kilimo Bora cha Hoho

[SMS kwa Umpendaye] 👉SMS nzuri ya kumtumia mume wako

Usipitwe na Nafasi za kazi kwa leo

<<Bofya HAPA kujua zaidi>>

.

utotoni.gif
ml.gif

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.