Tafuta

.

👉 Jinsi ya kupika Mboga Za Majani Makavu (Aina Yoyote)👇✔

Viamba upishi

Mboga za majani makavu ¼ kg
Mafuta vijiko vikubwa 3-4
Karanga zilizosagwa kikombe ½
Maziwa au tui la nazi kikombe 1
Kitunguu 1
Nyanya 2
Chumvi (kama kuna ulazima)
Maji baridi

Hatua

• Loweka mboga za majani makavu na maji kwa dakika 10-15.
• Osha , mboga na katakata nyanya na vitunguu.
• Kangaa, pukusua na saga karanga zilainike.
• Kanga kitunguu, weka nyanya, koroga zilainike.
• Ongeza mboga zilizolowekwa na maji yake kwenye rojo, koroga na funikia mpaka maji yakaukie na ive. Punguza moto.
• Koroga karanga zilizosagwa na maji, ongeza kwenye mboga ukikoroga kwa dakika 5.
• Onja chumvi, pakua kama kitoweo.
Uwezekano
Weka nyanya kidogo.
Tumia tui la nazi au krimu badala ya maziwa.
Weka nyama au dagaa au Mayai badala ya Karanga.

Soma%20Zaidi.gif Napendekeza uendelee kusoma kuhusu; Jinsi ya kupika kisamvu bila nazi.

🙉🙉🙉Usisahau kushare posti hii kuhusu (Jinsi ya kupika Mboga Za Majani Makavu (Aina Yoyote)).👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome💯✔

Jiunge na Kampeni ya utunzaji wa miti na misitu Lengo ni kuhamasisha watu kupanda na kutunza miti na misitu kwa manufaa yao ya sasa na kwa manufaa ya vizazi vijavyo

👉JUA ZAIDI...

New-Microsoft-PowerPoint-Presentation-2.gif

.