Vipimo

Majimbi (Eddoes) kiasi 6 au 7

Nyama ng’ombe Β½ kilos

Tangawizi ilosagwa 1 kijiko cha kulia

Haldi (bizari manjano/turmeric) Β½ kijiko cha chai

Tui zito la nazi vikombe 2

Chumvi kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Safisha nyama kisha weka chumvi, bizari ya manjano, tangawizi mbichi, ukaushe kwanza katika sufuria kwa kukaanga kaanga.
Ikianza kukauka, weka maji funika uchemshe iwive.
Menya majimbi ukate kate na uweke katika sufuria nyengine.
Mimina supu na nyama katika majimbi uchemshe yawive majimbi.
Mwisho weka tui zito la nazi uchanganye vizuri kisha weka katika moto kidogo tu bila kufunika yakiwa tayari.


uliyesoma.gif

πŸ™‰πŸ™‰πŸ™‰Usisahau kushare posti hii kuhusu (Jinsi ya kupika Magimbi Kwa Nyama Ya Ng’ombe).πŸ‘ Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasomeπŸ’―βœ”

🍴 Makala nyingine za Dondoo za Afya & MapishiπŸ‘‡

A.gif

uliyesoma.gif