Tafuta

.

👉 Jinsi ya kupika Biskuti Za Tende👇✔

Viamba upishi

Unga 4 Vikombe vya chai

Sukari ya laini (icing sugar) 1 Kikombe cha chai

Baking powder 2 Vijiko vya chai

Mayai 2

Siagi au margarine 1 Kikombe cha chai

Vanilla 1 Kijiko cha chai

Maziwa ya kuchanganyia kiasi

Tende iliyotolewa koko 1 Kikombe

ufuta (sasame) kiasi 1/4 kikombe

Jinsi ya kuandaa na kupika

1. Changanya unga, siagi, baking powder, na sukari katika mashine.

2. Kisha tia mayai, vanilla na halafu maziwa kidogo kidogo hadi mchanganyiko ushikamane.

3. Gawanya madonge mawili na usukume kama chapati, lakini sio nyembamba sana.

4. Tandaza tende robo ya duara na unyunyize ufuta duara zima: kisha kunja hadi mwisho na ukate kate, kisha upange katika trei ya kuvumbika.

5. Vumbika (bake) moto wa 350°F kwa muda wa dakika 20 au hadi vigeuke rangi na viwive.

6. Zikisha iiva ziache zipowe na zitakuwa tayari kuliwa.

Soma%20Zaidi.gif Napendekeza uendelee kusoma kuhusu; Mapishi ya wali wa hoho nyekundu.

🙉🙉🙉Usisahau kushare posti hii kuhusu (Jinsi ya kupika Biskuti Za Tende).👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome💯✔

Ndugu yako yupo hapa anakuulizia Anakupenda sana na amekumiss

👉SOMA ZAIDI HAPA...

Slide1-mabest-skull.PNG

.