Jinsi ya kupika Biriani Ya Nyama Mbuzi Ya Mtindi Na Zaafaraan

By, Melkisedeck Shine.

afya-mapishi-na-lishe.png

Jinsi ya kupika Biriani Ya Nyama Mbuzi Ya Mtindi Na Zaafaraan

Vipimo - Nyama

Nyama mbuzi - 1 kilo

Kitunguu menya katakata - 1

Nyanya/tungule - 2

Thomu (kitunguu saumu/garlic) saga - 5 chembe

Tangawizi mbichi – kuna/grate au saga - 1 kipande

Pilipili mbichi saga - 2

Bizari ya pilau nzima (cumin seeds) - ½ kikombe cha kahawa

Mdalasini - 1 kijiti

Karafuu nzima - 5 chembe

Gilgilani/dania (coriander seeds) - ½ kikombe cha kahawa

Bizari ya mchuzi - 1 Kijiko cha supi

Chumvi - Kiasi

Mtindi - 1 glass

Hiliki ilopondwa - 2 vijiko vya chai

Vitunguu – menya katakata slices kwa ajili ya kukaanga- 7- 9

Mafuta - Kiasi ya kukaangai vitunguu

Vipimo - Wali

Mchele wa pishori/basmati - 4 glass

Zaafarani roweka katika kikombe cha kahawa - Kiasi

Mafuta - Kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Katika sufuria, changanya nyama pamoja, kitunguu kimoja, tangawizi, thomu, nyanya, na viungo vyake isipokuwa mtindi, hiliki na vitunguu vilobakia.

Tia maji kisha funika ichemke mpaka iwive nyama na ikauke supu.

Tia mtindi na hiliki changanya pamoja.

Weka mafuta katika karai, kaanga vitunguu mpaka viwe rangi ya hudhurungi. Toa uchuje mafuta. Kisha viponde ponde kwa mkono uchanganye na nyama.

Chemsha mchele uive nusu kiini, mwaga maji.

Mimina katika nyama utie zaafarani, funika upike wali hadi uwive.

Epua ukiwa tayari.


USIKOSE HII👉 TIBA KWA KUTUMIA MAJI

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Jinsi ya kupika Biriani Ya Nyama Mbuzi Ya Mtindi Na Zaafaraan;

a.gif Jinsi ya kuandaa Ndizi Mbichi Za Supu Ya Nyama Ng’ombe

Ndizi mbichi - Kisia.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika Biriani ya Nyama Ng'ombe Na Mtindi

Mchele wa biriani - 5 gilasi.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Ndizi mzuzu

Ndizi tamu (plantain) 3-4
Tui la nazi (coconut milk) kikombe 1 cha chai
Sukari (sugar) 1/4 ya kikombe cha chai
Hiliki (Ground cardamon) 1/4 ya kijiko cha chai
Chumvi (salt) 1/4 ya kijiko cha chai.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Tambi za sukari

Tambi (spaghetti 1/2 ya packet)
Mafuta (vegetable oil)
Sukari (sugar 1/2 kikombe cha chai)
Hiliki (cardamon 1/2 kijiko cha chai)
Chumvi (salt 1/2 kijiko cha chai)
Tui la nazi (coconut oil 1 kikombe cha chai)
Maji kiasi.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika mkate wa sembe

Unga sembe glass 1
Unga ngano glass 1
Sukari glass 1 (unaweza kupunguza kidogo)
Maziwa glass 1
Mafuta 1/2 glass
Mayai 4
Iliki iliosagwa 2tbs
Bp 2tbs.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kutengeneza saladi

Tango 1/2
Kitunguu 1/2
Cherry tomato 8
Lettice kiasi
Green olives kidogo
Black olives kidogo
Hoho jekundu 1
Carrot
Giligilani kidogo.. endelea kusoma

a.gif Namna ya kutibu chunusi kwa kutumia asprin

.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia papai

Dawa nyingine madhubuti ya chunusi ni papai. Tunda hili ni moja ya matunda yanayotumika kwa ajili ya urembo hasa kwa wanawake… endelea kusoma

afya-mapishi-na-lishe.png

.

familia-mapenzi-na-mahusiano.png
SALAMU-JIONI98HBS.JPG
elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.