Jinsi ya kupika Baklawa Za Pistachio Na Lozi

By, Melkisedeck Shine.

vichekesho-bomba-vya-siku.png

Jinsi ya kupika Baklawa Za Pistachio Na Lozi

VIAMBAUPISHI

Philo (thin pastry) manda nyembamba - 1 paketi

Siagi - ¼ Kikombe cha chai

Baking powder - 2 Vijiko vya chai

Pistachio/ lozi - 2 vikombe vya chai

Mafuta - ½ Kikombe

VIAMBAUPISHI VYA SHIRA

Sukari - 2 Vikombe vya chai

Maji - 2 ½ Vikombe vya chai

ndimu - ½ kijiko cha chai

JINSI YA KUANDAA

Tafuta treya iliyokuwa sawa na ukubwa wa hizo manda nyembamba (philo) au zikate hizo manda kwa ukubwa wa treya (mraba au mstatili)
Kisha yeyusha siagi changanya na mafuta.
Kisha panga manda moja pakaza mafuta juu yake kisha weka manda nyingine juu yake kisha pakaza mafuta tena weka manda nyingine juu yake, endelea kufanya hivyo mpaka ziwe kama sita au saba kisha nyunyizia pistachio na lozi halafu panga tena manda na mafuta manda na mafuta tena sita au saba kisha nyunyizia tena pistachio na lozi.
Panga namna hivyo mpaka treya ijae inapofika manda ya mwisho kata vipande vya mraba vidogodogo humo humo kwenye treya kisha nyunyizia mafuta yaliyobaki.
Washa moto wa oven 350°F kwa muda wa dakika 20 au hadi rangi ibadilike kidogo (isikauke sana)
Chemsha syrup yako kama shira ya majimaji lakini isiwe nzito sana ikishakuwa tayari mwisho tia ndimu acha ipoe kidogo kisha miminia juu ya treya yote halafu malizia kunyunyizia pistachio na lozi zilizobaki.
Zikishakuwa tayari zipange kwenye sahani tayari kwa kuliwa.

ANGALIZO

Ukishatoa treya kwenye oven wacha ipoe kidogo na syrup yako pia wacha ipoe kidogo kabla hujamimina, ukitia ya motomoto zitalainika.
Manda nyembamba za baklawa zinauzwa tiyari madukani kwenye pakiti.


Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Jinsi ya kupika Baklawa Za Pistachio Na Lozi;

a.gif Jinsi ya kupika Biskuti Nyembamba (Wafer Bar) Za Chokoleti Na Njugu

Wafer Powder/gram wafer (unga wa biskuti uliosagwa wa tayari) - vikombe 2.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kutengeneza biskuti za Matunda Makavu Na Cornflakes

Unga - 4 Vikombe.. endelea kusoma

a.gif Namna ya kutengeneza Visheti Vya Nazi Na Njugu (Sudani)

Unga - 3 mug za chai.. endelea kusoma

a.gif JINSI YA KUANDAA VILEJA

Unga wa mchele - 500g.. endelea kusoma

a.gif Kampeni Ya Wafanye Watabasamu

Let Them Smile Campaign au Kampeni ya Wafanye nao Watabasamu ni kampeni endelevu ya kuhamasisha ushirikiano, umoja na kusaidiana katika jamii kwa watu wa matabaka yote.
Kampeni hii ina lengo la kuamsha na kueneza furaha itokanayo na umoja na mshikamano kwenye jamii kwa njia ya kusaidiana na kushirikiana kimawazo, kwa matendo na kifedha. Ni kweli kwamba furaha ya kweli haiji kwa kujifurahisha mwenyewe bali kwa kufurahishwa… endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Ugali na dagaa

Dagaa (dried anchovies packet 1)
Unga wa ugali (corn meal flour 1/4 kilo) (unaweza kutumia unga wa choice uipendayo)
Nyanya ya kopo (tin tomato 1/2)
Kitunguu maji (onion 1)
Limao (lemon 1/4)
Pilipili mbuzi nzima bila kukata (scotch bonnet pepper1, do not chop)
Chumvi (salt 1/4 ya kijiko cha chai)
Mafuta (vegetable oil)
Hoho (green pepper).. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika Cookies Za Jam Ya Peach Na Raspberry

Unga kikombe 1 ½.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya mboga ya mnavu

Mnavu mkono 1
Kitungu 1
Karoti 2
Maziwa kikombe 1
Mafuta vijiko viubwa 4
Karanga zilizosagwa kikombe 1
Chumvi kiasi ½.. endelea kusoma

vichekesho-bomba-vya-siku.png

.

vichekesho-bomba-vya-siku.png
wadogo.gif
uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.