Jinsi ya kuandaa Pilau ya sosi ya soya, nyama na mboga

By, Melkisedeck Shine.

familia-mapenzi-na-mahusiano.png

Jinsi ya kuandaa Pilau ya sosi ya soya, nyama na mboga

Mahitaji

Nyama isiyokuwa na mifupa - 1 ½ Lb(ratili)
Mchele wa Basmati (rowanisha) - 3 Magi
Vitunguu maji - 2
Mchanganyiko wa mboga za barafu - 1 Magi
(karoti, mahindi, njegere)
Pilipili Mbichi - 3
Pilipili mboga kijani na nyekundu - 1
Pilipili manga - ½ kijiko cha chai
Chumvi - Kiasi
Sosi ya soya (soy sauce) - 5 Vijiko vya supu
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa - 1 Kijiko cha supu
Mchanganyiko wa bizari (garam masala) - 1 Kijiko cha supu
Kotmiri iliyokatwa - ½ Kikombe
Mafuta ya kukaangia - Kiasi

Namna Ya Kutaarisha

Ndani ya sufuria, tia mafuta yakipata moto kaanga vitunguu mpaka ziwe rangi ya hudhurungi.
Kisha tia nyama iliyokatwa vipande vidogo vidogo pamoja na maji ya kiasi na viungo vyote isipokuwa mchele, mboga zote na kotmiri. chemsha mpaka nyama iwive na maji yakauke.
Halafu changanya na mboga na iwache kwa muda wa dakika kumi kisha tia kotmiri na umimine kwenye bakuli au treya ya oveni na uweke kando.
Chemsha mchele na chumvi uwive kama kawaida ya kupika wali wa kuchuja, kisha umwagie juu ya ile treya ya nyama.
Nyunyizia mafuta na sosi ya soya na ipike katika oveni moto wa 350° kwa muda wa dakika 20 hivi.
Ukishawiva, uchanganye ukiwa tayari kwa kuliwa


Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Jinsi ya kuandaa Pilau ya sosi ya soya, nyama na mboga;

a.gif Mapishi ya Haliym Ya Nyama Mbuzi -Bokoboko La Pakistan

Nyama ya mbuzi au ng’ombe ya mafupa - 2 LB.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kuandaa Muhogo, Samaki Wa Kuchoma Na Bamia

Mihongo 3 - 4.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika Viazi Vya Nazi Kwa Nyama

Viazi - 3lb.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kutengeneza Muhogo Wa Nazi Na Samaki Wa Kukaanga

Muhogo - 3.. endelea kusoma

[Msemo wa Leo] 👉Umbali na upendo

[Jarida la Bure] 👉Jarida la kilimo bora cha HOHO

a.gif Mapishi ya Mlenda wa bamia na nyanya chungu

Bamia (okra) 20
Nyanya chungu (garden eggs) 5
Magadi soda (Bicabonate soda) 1/4 ya kijiko cha chai
Nyanya (fresh tomato) 1
Chumvi (salt) kidogo
Pilipili 1/4.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika Juisi Ya Mabungo

Mahitaji.. endelea kusoma

a.gif Dondoo muhimu kwa Afya yako unapostuka usiku

Kumekuwepo na tatizo la vifo vya ghafla sana tena kwa watu ambao wana afya njema na hii inatokana na kuamka ghafla usiku ambapo ubongo hukisa damu ya kutosha… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika wali wa Tuna (samaki/jodari)

Tuna (samaki/jodari) - 2 Vikopo.. endelea kusoma

vichekesho-bomba-vya-siku.png

.

vichekesho-bomba-vya-siku.png
mtu.gif
uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.