Faida za ulaji wa Peasi

By, Melkisedeck Shine.

afya-mapishi-na-lishe.png

Faida za ulaji wa Peasi

Peasi ni tunda ambalo limekuwa halithaminiwi licha ya kuwa na faida lukuki katika mwili wa binadamu. Tunda hilo ambalo kwa umbo linafanana na tufaa (apple), lina faida nyingi kwa binadamu iwapo atalitumia mara kwa mara.

Tunda hili limekuwa adimu kutokana na kutostawi katika maeneo mengi hivyo watu wengi hawalifahamu na hata walionapo hawalitilii maanani kama ilivyo kwa matunda mengine kama vile ndizi, embe, papai na mengine.
Tunda hili lina faida mbalimbali katika mwili wa binadamu kama vile kukausha jasho la kwapa kwa wale wenye kutokwa na jasho jingi endapo litaliwa mara kwa mara.
Pia tunda hilo ambalo hulimwa sana katika Mkoa wa Tanga husaidia kupunguza mwasho wa koo na juisi yake ni nzuri skwa kuua mba, hutibu kibofu cha mkojo na uti wa mgongo.
Vilevile tunda hili lina Vitamin A na B ambazo husaidia kuepukana na upofu, pia husaidia kuongeza hamu ya kula na kuboresha mfumo wa fahamu.
Wakati mwingine tunda la peasi husafisha mishipa ya moyo na kutibu mafua ya ndege na husaidia mmeng’enyo wa chakula ufanyike vizuri.
Tunda la Peasi husaidia kuongeza kinga za mwili, kuupa mwili nguvu, hupunguza shinikizo la damu, kuzuia mafuta kuganda mwilini (cholestrol), huzuia magonjwa ya saratani, kiungulia pamoja kupunguza homa.
Pia tunda hili likitumika baada ya chakula cha usiku au baada ya kupata kifungua kinywa huweza kuleta matokeo mazuri.


Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Faida za ulaji wa Peasi;

a.gif Dalili za kuharibika kwa Mimba

Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha mama mjamzito mimba yake kuharibika. Sababu kuu huwa ni magonjwa kama vile ugonjwa hatari wa malaria, ugonjwa unaotokana na zinaa kama vile kaswende na kisonono na U.T.I, dawa fulani fulani mfano Albendazole, Misoprostol, Metronidazole na kadhalika… endelea kusoma

a.gif Sababu, dalili na jinsi ya kujikinga na tatizo la kiungulia kwa wanawake wajawazito

Hii ni hali inayowakumba mama wajawazito walio wengi. Inaweza kutokea kipindi chochote cha ujauzito ila mara nyingi hutokea katika umri wa mimba kuanzia miezi mitatu… endelea kusoma

a.gif Faida za kula mayai asubuhi

Mayai ni kitu kilichozoeleka na kinachopatikana kwa gharama nafuu. Kutokana na kuzoeleka huku watu wengi wamekuwa wakipuuza umuhimu au nafasi ya mayai katika afya zao. Pengine kupuuza huku kunatokana na mazoea au ukosefu wa elimu juu ya faida zinazopatikana kutokana na ulaji wa mayai… endelea kusoma

a.gif Namna ya kuongeza nguvu za kiume bila kutumia dawa

Upungufu wa nguvu za kiume umekua tatizo kubwa sana kwa wanaume wengi. Tatizo hili limewakumba wanaume wengi walio katika ndoa na hata wale ambao bado hawajaoa. Watu wengi wamekuwa wakisumbuka kutafuta utatuzi kwani tatizo hili huwafanya kuwa na wasiwasi wa maisha. Ndoa nyingi zimevunjika na mahusiano kuharibika kwa sababu ya tatizo hili… endelea kusoma

a.gif Njia za kuongeza wingi wa mbegu za kiume

Chakula unachokula kina mchango mkubwa katika kutibu tatizo hili. Vyakula vingi vya kisasa havina uwezo wa kuongeza uwingi wa mbegu… endelea kusoma

a.gif Dondoo muhimu za afya

Tafadhali soma na uwapelekee wengine… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika Biskuti Ya Keki Kavu kwa kizungu Shortcake

Unga 2 Magi (vikombe vya chai).. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia Uwatu (Fenugreek)

Uwatu ni dawa nyingine ya asili inayotumika kutibu chunusi. Uwatu unaondoa sumu na maambukizi mbalimbali… endelea kusoma

picha-kali.png

.

afya-mapishi-na-lishe.png
UJUMBE-MSAMAHA-35JHF32.JPG
familia-mapenzi-na-mahusiano.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.