Kichekesho%20Kipya Usikose 📕Kitabu cha Mbinu za Kilimo Bora Cha Mboga🌿🍅 Kina kurasa 100 na utaalamu wa mazao zaidi ya 10👉Bofya hapa KuchukuaKizuri

.

ss.gif Faida za mnyonyo na mazao yake

MELKISEDECK-SHINE-LEON.jpg
Melkisedeck Leon Shine

💥"Biashara ya maisha ni kusonga mbele tuu. Maisha hayarudi nyuma wala hayafai kurudisha nyuma. Maisha yanasonga mbele."🔥

👏Baada ya kusoma kuhusu👇;

images-7.jpeg
💡Leo nimekutayarishia💫 makala kuhusu🌠 Faida za mnyonyo na mazao yake👇.

💥Faida za mnyonyo na mazao yake👇

Nyonyo Mbarika (Castor)
Mnyony(KiSwahili) Erand (KiHindi) Kastorka(KiRusi) ni mmea wa jamii ya Mbono Kaburi, kwa
jina la kitaalamu Japtropha

Baadhi ya faida za mnyonyo na mazao yake

Mbali na kuweza kutumia mnyonyo kama uzio hai,njia hii inaweza
kutumika kwa wale wasio na eneo kubwa la shamba ndipo sasa wakapata faida zake kama
ifuatavyo:🔽

Majani ya mnyonyo yanaweza kutumika kama tiba ya ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB), kukanda
(massage) ili kuondoa maumivu na majani haya
yakifungwa kwenye mguu unaouma huleta nafuu hasa kwa maumiviu yanayokuja baada ya kuteguka, pia hutumika kutibu uvimbe kwa wanyama.

Mizizi ya mnyonyo huweza kutumiwa kama dawa
ya mafundo fundo, uvimbe, kuungua, macho ya
manjano, kuumwa koo na magonjwa ya
kuambukiza ya kisonono na kaswende. Ukijaza
maji baridi kwenye kikonyo cha mnyonyo na
kumpa mtu mwenye kwikwi kila baada ya dakika
mbili au tatu hivi, mara nyingi huondoa
usumbufu unaoletwa na kwikwi. Mbegu/Punje/Tunda/Njugu za mnyonyo zikimezwa na maji bilauri moja kila siku kwa muda wa siku tano huweza kutibu maumivu yaliyosababishwa na kuungua. Vile vile, mbegu hizi huweza kusagwa na kisha kuenguliwa mafuta
kwa ajili ya kulainisha mashine na mitambo viwandani. mbegu za mnyonyo kabla ya kukomaa
Mafuta
yatokanayo na
mbegu za nyonyo mfano
Ricinoleic Acid,
Oleic Acid,
Linoleic Acid
nk hutumika
kutibu ugonjwa
wa wa jongo
(rheumatism)unaowakumba watu wengi wanaoishi maeneo ya miinuko na
baridi, pia hutibu ugonjwa wa mifupa ujulikanao kwa jina la kitaalamu kama arthritis na gauti. Mafuta ya mnyonyo pia yanaweza kutumika
kama njia ya kupanga uzazi kwani yana kiasi
fulani cha sumu ya protini ijulikanayo kitaalamu kama ricin ambayo ikitumiwa kwa kiasi kidogo huharibu utungo,huweza pia kutumiwa kama
mafuta ya kupaka ama losheni katika sehemu za
siri ili kuua mbegu za uzazi za kiume wakati wa tendo la kujamiiana. uzazi wa mpango.

Tahadhari:

Mnyonyo ni mti wenye sumu
inayoweza kuua binadamu au
wanyama endapo itatumika kuzidi
kipimo. Mazao yoyote yatokanayo na mnyonyo huhatarisha au/na
kuharibu mimba na hata kuweza
kusababisha kifo cha mjamzito,
hivyo, matumizi yake lazima yawe
ya uangalifu mkubwa. Mafuta ya Ricinoleic acid
yanayopatikana kutokana na mnyonyo vile vile yanaweza kutumika kurekebisha hedhi
(mzunguko wa damu ya mwezi kwa wanawake) ikiwa mzunguko
umechelewa ama kusimama katika
umri usiotarajiwa. Huweza pia
kupunguza maumivu makali
yanayotokea wakati wa hedhi.

Mafuta ya mnyonyo yanayojulikana
kitaalamu kama Undecylenic Acid
huweza kutumika kutibu magonjwa
mbalimbali ya ngozi na vidonda
vinavyosababishwa na bakteria ama ukungu(fungus). mbegu za mnyonyo baada ya kukomaa

Akina mama wanaonyonyesha pia wanaweza kutumia mafuta
baridi ya mnyonyo (kiasi kidogo ili kuepuka madhara ya mafuta hayo kwa mtotokumbuka
hapo awali nimeandika kuwa mafuta haya
yakitumiwa kwa kiwango kikubwa ni sumu ) kuongeza wingi na mtiririko rahisi wa maziwa.

Nywele nzuri, safi, nadhifu na zisizokatika pia
ngozi imara inapatikana kutokana na matumizi ya mafuta ya mnyonyo.Mafuta ya mnyonyo pia ni
dawa nzuri ya kufungua tumbo la uyabisi(kuvimbiwa).

Mnyonyo unaweza pia kuwafaa watu wanaoishi na VVU (Virusi Vya UKIMWI) kwani mafuta yake ni sumu ya kuua vimelea vya
magonjwa kama vile bakteria na ukungu(fungus).

Njia:

Kupakaza: Chukua kipande cha nguo ama
kitambaa, kisha kiloweke kwenye mafuta ya
mnyonyo ndipo ufunge katika kiwiko ama
eneo lenye maumivu ama kidonda.Vinginevyo
chukua kiasi cha mafuta na kupaka eneo linalohusika mfano, penye kidonda, kuugua
ama pakaza kichwani au juu ya tumbo wakati
wa maumivu ya hedhi nk. Unaweza kuacha kwa muda wa saa moja kabla ya kunawa ili uipe ngozi muda wa kunyonya kiasi cha
mafuta. Unaweza kujifunga kitambaa hicho
tumboni ama mgongoni kama kibwebwe na kuendelea na shughuli za kawaida.

Kunywa: Chemsha mbegu chache za mnyonyo
pamoja na maji na maziwa kisha unywe kiasi kidogo kadiri ya nusu hadi bilauri moja ya ujazo wa mili lita mia mbili na arobaini.

Kusafisha utumbo: Kunywa mafuta ya mnyonyo vijiko viwili vikubwa vya chakula asubuhi, kisha pumzika kwa saa mbili ndipo unywe maji glasi mbili na endelea kunywa maji glasi moja kila baada ya saa moja.

👊Usikubali kupitwa na Jarida la kilimo bora cha vitunguu maji na vitunguu twaumu (swaumu). Linatoa elimu ya kulima vitunguu . 👉Bofya hapa Kuchukua👈

so.gifLadha ya bia😁😁😁

MELKISEDECK-LEON.jpg

📝Nitumie Maoni💭 yako Kuhusu Faida za mnyonyo na mazao yake hapa👇

Jina
Mahali
Mfano Mkoa, wilaya n.k
Email
Itatumika kukujibu
Maoni yako
images-13.jpeg

🐼 Endelea kusoma kuhusu;-🙉

.

MELKISEDECK-SUA.jpg
C.gif "Uwezo wa kuwa makini katika jambo bila kuyumbishwa na kitu chochote ni ishara kuu ya mtu mwenye akili na mwenye mafanikio."

.

Kichekesho%20Kipya Usikose Jarida la Kilimo Bora cha Matikiti Linafundisha ulimaji wa matikiti 👉Bofya hapa KuchukuaKizuri

.

.

📷 Picha Bomba👇

P.gif
V5.gif

.

.

Kichekesho%20Kipya Usikose 📕Kitabu cha Mbinu za Kilimo Bora Cha Mboga🌿🍅 Kina kurasa 100 na utaalamu wa mazao zaidi ya 10.
👉Bofya hapa KuchukuaKizuri

.

Kichekesho%20Kipya Usikose 📕Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE👧👗👠 Kinamwelezea🔎Mwanamke🔍 kinagaubaga✔.
👉Bofya hapa KuchukuaKizuri

.

.

.

IMG_20170703_130508.jpg

Habari msomaji wangu…?
"Ni matumaini yangu kuwa wewe ni miongoni mwa wasomaji wangu wa kila siku wa blog hii, kama sivyo unakaribishwa kuungana na wasomaji wangu wanaotembelea Blog hii kila siku."

images-22.jpeg

Jina langu ni Melkisedeck Leon Shine Mwendeshaji wa blog hii.

Usisite kuniandikia maoni,mapendekezo au maswali hapa

Jina
Mahali ulipo
Mfano Mkoa, Wilaya n.k
Email
Itatumika kukujibu
Maoni yako

KUHUSU BLOG HII | MAWASILIANO | ABOUT AUTHOR | LEGAL GUIDELINES