Faida za kula uyoga kiafya

By, Melkisedeck Shine.

Uyoga una vitamini na aina nyingi na madini. Virutubisho vilivyothibitishwa kuwemo kwenye uyoga ni pamoja na Vitamin B2, B3, B5, B6, B Complex pamoja na madini ya Potasiamu na Phosphorus.

Virutubisho hivyo ni muhimu kwenye mwili wa binadamu katika kutoa na kuimarisha kinga ya kupambana na ‘wavamizi’ maradhi.

Aidha, inaelezwa kuwa uyoga ni chanzo kingine kizuri sana cha madini ya chuma (iron) na kopa ambayo yanahusika kwa kiasi kikubwa na uwezeshaji wa usambaza wa hewa ya oksijeni mwilini. Kupatikana kwa madini ya chuma na kopa kwenye uyago ni jambo la kipekee ambalo linafanya mmea huo kuwa tofauti na muhimu.

Uyoga una Utajiri wa Vitamini B

Zikifafanuliwa nguvu za uyoga (Mushrooms) kwa mapana, inaelezwa kuwa Vitamin B2 inayopatikana kwenye uyoga, ni tiba tosha kwa watu wanaosumbuliwa na ugonjwa wa kichwa unaojulikana kama ‘kipanda uso’. Kiasi kidogo cha uyoga utakachokula kitapunguza kasi ya kuumwa kichwa hicho.

Vilevile Vitamin B inasifika kwa uwezo wake wa kuzuia uchovu wa mwili (fatique) na akili hasa wakati wa kazi nyingi. Vitamin B3 husaidia kupunguza kiwango cha mafuta mabaya ya Kolestrol mwilini, wakati Vitamin B6 yenyewe huondoa hatari ya mtu kupatwa na kiharusi au moyo kusimama ghafla (Heart Attack).

Madini ya Zinc katika Uyoga Huimarisha Kinga za Mwili

Kama faida zote za kiafya zilizo orodheshwa hapo juu zinazopatikana kwenye uyoga hazikutosha, basi kuna faida nyingine ambayo inatokana na madini aina ya Zinc yanayopatikana kwa wingi kwenye mboga hii. Zinc ina faida nyingi sana mwilini na miongoni mwa faida hizo ni uimarishaji wa kinga ya mwili (Immune System).

Zinc si muhimu tu kwa uimarishaji wa kinga mwilini, bali pia kwa uponyaji wa haraka wa vidonda mwilini. Vilevile mboga hii inasaidia sana ukuaji mzuri wa seli za mwili, huimarisha kiwango cha sukari mwilini na kukufanya kusikia ladha na harufu ya vyakula na vitu vingine ipasavyo.

Kwa ujumla uyoga ni mboga muhimu na inapaswa kuliwa na kila mtu anayejali afya yake kutokana na faida zinazopatikana humo. Kuanzia leo, jaribu kuweka uyoga katika orodha ya mboga unazonunua kila wiki kwa ajili ya familia yako.

Bila shaka mada hii imekusaidia kuelewa faida za kula uyoga katika kuboresha afya yako. Kama ndiyo basi chukua hatua sasa na uanze kutumia uyoga katika mpango wako wa chakula kwani elimu bila vitendo ni kazi bure.KADI-POLE-MZAZI.JPG

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Faida za kula uyoga kiafya;

a.gif Faida 25 za kutembea kwa Miguu

Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamebadili mfumo wa maisha ya watu pamoja na kuathiri afya zao kwa kiasi kikubwa. Hivi leo watu wanatumia vyombo mbalimbali vya usafiri kwenda karibu kila eneo… endelea kusoma

a.gif Mwanamke kuamka mapeme asubuhi kunapunguza uwezekano wa kupata saratani ya matiti

Kuamka asubuhi na mapema hupunguza uwezekano wa mwanamke kupata saratani ya matiti… endelea kusoma

a.gif Vyakula vya kukusaidia kupunguza uzito

Kuchagua vyakula sahihi kwa mlo wako inaweza kuwa changamoto na tungependa kuamini kwamba kupungua uzito ni jambo tu la kula kalori chache na kufanya mazoezi zaidi . Hata hivyo, si mara zote zoezi hili linakuwa rahisi. Kama ni lengo lako kupunguza uzito, kuchagua chakula gani ule ni muhimu kama kuchagua kiasi gani cha chakula ule… endelea kusoma

a.gif Vyakula 7 vya kuepuka kula ili uwe na afya nzuri

Inasemwa kuwa “wewe ni kile unachokula” kwa kumaanisha kuwa mwonekano wetu na afya ya mwili na akili unajengwa na chakula tunachokula. Madhara ya chakula chetu tunachotumia yako pia katika ngozi. Kuna vyakula vinavyozeesha ngozi kwa haraka na ni budi kuvijua na kuviepuka… endelea kusoma

[Kitendawili Kwako] 👉Ina paa, madirisha na milango

[Kichekesho Kwako] 👉Amri za chuo

KADI-SALAMU-JIONI-MZAZI.JPG

a.gif Namna ya kuondokana na tatizo la kunuka Kikwapa

Harafu ya jasho inakera, kibaya zaidi ni kuwa wewe mwenyewe husikii harufu hiyo ila wale walio karibu yako. Kwa upande mwingine kujaribu kuzuia kutoka jasho ni hatari kwa afya yako na kujaribu kuondoa harufu kwa kutumia pafyumu husababisha madhara mengine ya kiafya na kwa bahati mbaya perfume zina jaribu poteza harufu kwa mda mfupi tu na sio kutokomeza tatizo hilo… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika Biriani Ya Nyama Mbuzi Ya Mtindi Na Zaafaraan

Nyama mbuzi - 1 kilo.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kutengeneza Wali Wa Dengu Kwa Samaki Wa Kukaanga

Mchele wa basmati - 3 Vikombe.. endelea kusoma

a.gif Kampeni ya kutetea watoto yatima

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.
Lengo la kampeni hii ni kuhamasisha watu wote kusaidia kulea na kuwakuza watoto yatima kwa maendeleo bora ya kimwili, kiroho na kijamii kwa manufaa ya watoto wenyewe na kwa manufaa ya watu wote kwa sasa na kwa baadae.
Kampeni hii inaamini kuwa watoto yatima kama walivyo watoto wengine nao ni kama mali ambayo inawekezwa sasa kwa matumizi na maendeleo ya baadae. Japokuwa hawana (wazazi) watu/mtu rasmi wa kuwatunza haimaanishi kuwa hawawezi kuwa watu wa maana baadae… endelea kusoma

[Msemo wa Leo] 👉Uzuri na ubora

[Jarida la Bure] 👉Kijitabu cha Kilimo Bora cha Hoho

[Hadithi Nzuri] 👉Kisa kilichombadilisha mume tabia

[SMS kwa Umpendaye] 👉SMS ya kumtakia sweet wako usiku mwema

Usipitwe na Nafasi za kazi kwa leo

<<Bofya HAPA kujua zaidi>>

.

KADI-MMISI-MZAZI.JPG
UJUMBE-KUOMNBA-KUKUTANA-NA-NDUGU.JPG

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.