Faida za kula ukwaju

By, Melkisedeck Shine.

uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png

Faida za kula ukwaju

Ukwaju ni tunda maarufu sana ambalo hupatikana katika maeneo yenye uoto wa kitropiki. Kwa kingereza hujulikana kama tamarind, na kwa kitaalamu (botanical name) huitwa tamarindus indica, waarabu huita tamru alhind. Katika baadhi ya maeneo hutumiwa kama kiungo katika mboga.

Ukwaju umetunukiwa viambata muhimu na madini ambayo ni muhimu sana kwa mustakabali wa afya zetu. Una viambata kama calcium, vitamin C, copper, phosphorus, madini ya chuma, magniziam, na pyridoxine. Wataalamu wa afya wanasema kila gramu 100 za ukwaju kuna 36%za thiamin, 35% Iron, 23% magnesium ,na 16%phosphoras.
Pia ukwaju una kiwango kikubwa cha tartic acid Ma citric acid

Namna ya kuutumia ukwaju, tengeza juisi nzuri ya ukwaju, tumia kama kiungo katika chakula, unaweza kutafuna majani yake yenye ladha ya chumvichumvu, au kuyakausha majani ya mkwaju kivulini na kuweka katika uji, au supu au juisi ya matunda.

Zifuatazo ni faida zitokanazo na matumizi sahihi ya ukwaju;

Husaidia kuongeza uwezo wa macho kuona (improving eyesight). Matumizi ya ukwaju kwa kula au kutumia kama juisi huondoa matatizo ya macho na kukufanya uwe na macho yenye afya.

Husaidia kwa wenye kisukari, kwa sababu ukwaju unaviambata muhimu kama polyphenols na flavonoids ambavyo ni madhubuti katika kurekebisha sukari mwilini na kupunguza vitambi.

Husaidia kwa wenye shinikizo la damu .unashauriwa kunywa juisi ya ukwaju Mara kwa mara. Kwasababu ukwaju hupunguza kiwango kikubwa cha lehemu mwilini (cholesterol). Pia unakiwango kikubwa cha madini ya potasiam .licha ya hayo ukwaju unafaida ya kusafisha damu.

Huondoa tatizo la nywele kukatika, na kuzipa mng'aro halisi, chemsha ukwaju, kisha tumia maji yake, changanya na vijiko viwili vya bizari, oshea nywele zako. Kisha ziache nusu saa na uzioshe kwa maji ya vuguvugu.

kuboresha mfumo wa mmeng 'enyo na kuondoa gesi, tumia juisi ya ukwaju.

Mengineyo ni kupunguza uzito

Kuboresha ngozi yako


Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Faida za kula ukwaju;

a.gif Namna ya kuondokana na tatizo la kunuka Kikwapa

Harafu ya jasho inakera, kibaya zaidi ni kuwa wewe mwenyewe husikii harufu hiyo ila wale walio karibu yako. Kwa upande mwingine kujaribu kuzuia kutoka jasho ni hatari kwa afya yako na kujaribu kuondoa harufu kwa kutumia pafyumu husababisha madhara mengine ya kiafya na kwa bahati mbaya perfume zina jaribu poteza harufu kwa mda mfupi tu na sio kutokomeza tatizo hilo… endelea kusoma

a.gif Faida 10 za kulala mapema kiafya

Mapera ni matunda yanayo patikana kwa wingi lakini mara nyingi huwa hayapendelewi sana kutokana na ugumu wake wakati wa kuyatafuna pamoja na kuwa na mbegu mbegu nyingi. Hata hivyo matunda haya yana faida kubwa sana kwa afya ya mwili wa mwanadamu… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kujua kama una Mimba: Dalili za kwanza kabisa za Ujauzito

Mwanamke anapopata ujauzito kwa kawaida huwa anaanza kuona dalili ambazo si za kawaida. Na ni wakati huo ambao ni muafaka kwake kuanza kuuchunguza mwili wake… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kuongeza kiasi cha utokaji wa maziwa kwa kina mama wanaonyonyesha na kwa afya ya mtoto

Maziwa ni chakula kikuu cha mtoto punde anapozaliwa. Mama anahitaji kuwa na Maziwa ya kutosha ili mtoto aweze kuwa na afya. Zipo sababu mbalimbali zinazopelekea wakina mama wengi kushindwa kuzalisha maziwa mengi kwa ajili ya kuwanyonyesha watoto zao. Hata hivyo kama wewe ni mama na una tatizo hilo basi unatakiwa kufanya yafuatayio ili utengeneze maziwa kwa wingi;.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika Visheti Vya Kastadi Vya Shepu Ya Kombe

Unga wa ngano 1 Kilo.. endelea kusoma

a.gif Sababu za magonjwa ya figo na jinsi ya kuondokana na janga la magonjwa ya Figo

1.Usichelewe kwenda HAJA. Kutunza mkojo kweye kibofu chako kwa muda mrefu ni wazo baya. Kibofu kikijaa kinaweza kusababisha uharibifu. Mkojo ambao unakaa kwenye kibofu huzidisha bakteria haraka.
Mara mkojo unaporudi nyuma ya njia na Figo, sumu dutu husababisha maambukizi ya figo, pia njia ya mkojo na "nephritis", pamoja na "uremia". Wakati wito asili (unahisi mkojo) fanya hivyo haraka iwezekanavyo… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika Biskuti Za Kuchoveya Chokoleti

Unga 300gm.. endelea kusoma

afya-mapishi-na-lishe.png

.

familia-mapenzi-na-mahusiano.png
KADI-MLO-MWEMA-MZAZI.JPG
picha-kali.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.