Faida ya kunywa maji yenye limao au ndimu kila siku

By, Melkisedeck Shine.

elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

Faida ya kunywa maji yenye limao au ndimu kila siku

Watalam mbalimbali wa afya wanasema ya kwamba kwa kila siku ni vyema unywe maji ya ndimu ili uweze kujitibu magonjwa yafuatayo;

Unachotakiwa kufanya ni;
Weka maji yenye joto kidogo (vuguvugu) katika glasi au kikombe , kata limao au ndimu vipande viwili na kamua kipande kimoja tu ndani ya glasi yenye maji.

Kunywa na uanze siku mpya. Ni vizuri ukafanya hivi dakika 30 kabla ya kula chochote kingine kwa faida zaidi.

Anza leo kwa kunywa maji yenye ndimu kila siku asubuhi na uone mabadiliko ndani ya mwili wako. Mshirikishe mwenzio ili naye afaidike.

1. Huchochea Mmeng’enyo wa Chakula Tumboni

Maji yenye ndimu husaidia chakula kusagika vizuri na haraka katika mfumo wa chakula. Japo limao lina asidi(acid) lakini likiwa tumboni huwa alkali (alkaline) na kufanya mazingira mazuri kwa usagaji wa chakula.

Pia maji ya uvuguvugu husaidia kusawazisha utumbo uliojikunja na kutoa mawimbi tumboni na kufanya chakula kusukumwa vizuri.

2. Huboresha Kinga za Mwili

Vitamini C na potasiumu iliyomo kwa wingi katika limao inasaidia katika utengenezaji wa seli za kinga katika mwili.

3. Husaidia Kinga Dhidi ya Saratani

Vitamini C ni antioksidant (antioxidant) ambayo inasaidia kuondoa free radicalsmwilini ambazo zimetambulika kusababisha saratani (cancer).

Usafishaji wa Mwili na DamuLimao husaidia kusafisha damu kwa kuondoa uchafu. Limao pia husafisha figo ,ini na mfumo wa chakula.

4. Kurekebisha Sukari katika Mwili

Limao husaidia kuweka kiasi cha sukari tumboni na katika mwili kuwa katika kiasi stahili.
Hii inawasaidia sana wagonjwa wa kisukari katika ulaji wao.

5. Dawa ya Kikohozi na Mafua

Limao ikitiwa katika maji ya uvuguvugu na asali husaidia sana katika kutibu mafua na kikohozi kwa njia ya asili.

6. Inasaidia Urekebishaji wa Ngozi na Kupona Makovu

Limao inasaidia kufanya ngozi isizeeke. Kama unataka kubaki kijana basi limao litakusaidia. Tabia za vitamin C za kusafisha uchafu zinasababisha kufanya ngozi kuwa na afya na kutozeeka haraka.

7. Husaidia Kupungua Uzito

Limao hupunguza hamu ya kula. Na inajulikana kuwa sababu kubwa ya watu kuwa na uzito mkubwa ni kula chakula kingi au kula mara kwa mara. Limao litakufanya ujisikie kushiba muda mrefu hivyo kusaidia wale amabao wanataka kupungua uzito.

8. Kuondoa Harufu ya Mdomo

Limao husaidia kuua bakteria wabaya mdomoni ambao husababisha harufu mbaya.


Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Faida ya kunywa maji yenye limao au ndimu kila siku;

a.gif Dalili za homa ya dengu (Dengue fever)

Dengue ni moja kati ya homa kali inayodhoofisha na kuambatana na maumivu makali. Kwa sasa hakuna kinga ya homa ya dengue, njia pekee ya kuepuka ugonjwa huu ni kuzuia kuumwa na mbu anayesambaza homa ya dengue… endelea kusoma

a.gif Tatizo la kutoka majimaji kwenye matiti

Tatizo hili husimama lenyewe kama ugonjwa ingawa pia inaweza kuwa ni dalili kama mwanamke ni mjamzito, ananyonyesha au ametoa mimba au ameharibikiwa na mimba. Kusimama kwake kama ugonjwa ni pale yanapotoka wakati mwanamke hana historia ya dalili hizo hapo juu… endelea kusoma

a.gif Madhara ya kunywa pombe wakati wa ujauzito

Kuacha Matumizi ya pombe wakati wa ujauzito ni moja ya njia ya kuzuia kupata matatizo ya kuzaliwa nayo na udhaifu kwa mtoto. Pia kuna matatizo kadhaa yanaweza kutokea kwa kichaga kutokana na matumizi ya pombe wakati wa ujauzito… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kufanya ili upate mtoto wa kike au wa kiume

Katika urutubishaji yai la mwanamke linabeba chromosome X yani XX. Na mbegu ya mwanaume inabeba chromosome XY. Chromosome X kutoka kwa mwanamke ikikutana na Y kutoka kwa mwanaume mtoto wa kiume hupatikana. Chromosome X kutoka kwa mwanamke ikikutana na X kutoka kwa mwanaume mtoto wa kike hupatikana.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kutengeneza Mkate wa mayai

Slice za mkate 6
Mayai 3
Chumvi
Olive oil.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Mandazi

Unga wa ngano (nusu kilo)
Sukari (Kikombe 1 cha chai)
Chumvi (nusu kijiko cha chai)
Hamira (kijiko kimoja cha chai)
Yai (1)
Maziwa ya unga (vijiko 2 vya chakula)
Butter (kijiko 1 cha chakula)
Hiliki (kijiko1 cha chai)
Maji ya uvuguvugu ya kukandia
Mafuta ya kuchomea.. endelea kusoma

a.gif Utajuaje kama una upungufu wa maji mwilini? Dalili ni hizi

Upungufu wa maji ni pale mwili unapopoteza kiasi kingi cha maji kwa njia mbalimbali, ikiwemo jasho na mkojo, mwili hupungukiwa maji na hivyo mtu huyo huambiwa ana upungufu wa maji. Tunaelezwa kuwa karibu theluthi mbili ya miili yetu imejaa maji… endelea kusoma

a.gif Madhara ya kutumia dawa za kuzuia mimba wakati wa hatari

Watu wengi hasa vijana watakuwa wanafahamu dawa ambazo hutumiwa sana kuzuia ujauzito pale ambapo wapenzi wamejamiiana ndani ya siku za hatari. Ninazungumzia dawa za kuzuia mimba sio dawa za kupanga uzazi. Dawa hizi zipo za aina nyingi ambazo zitozitaja hapa siku ya leo. Endapo wawili hawa wanakuwa hawapo tayari kupata mtoto, na wanaona kwamba siku walizojamiiana zitapelekea mwanamke huyo kutunga mimba, basi anaweza kutumia dawa hizi ambazo zinaharibu mazingira au uwezekano wa mimba kutungwa… endelea kusoma

picha-kali.png

.

picha-kali.png
KADI-PONGEZI-MZAZI.JPG
vichekesho-bomba-vya-siku.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.