Dondoo Muhimu kuhusu ugonjwa wa kisukari

Mpendwa Msomaji, baada ya kukuandalia makala inayopendwa kuhusu; Virutubishi, kazi zake katika mwili na vyanzo vyake, sasa nimekuandalia makala hii kuhusu;

Dondoo Muhimu kuhusu ugonjwa wa kisukari.

Unaalikwa pia kusoma kuhusu; Mapishi ya Ugali Kwa Mchuzi Wa Samaki Wa Kuchoma.

Dondoo Muhimu kuhusu ugonjwa wa kisukari

By, Melkisedeck Shine.

Wapendwa, napenda kushirikiana na nyinyi kujuzana hili nililolisikia kupitia channel ten leo asubuhi kuhusu ugonjwa wa kisukari.
Wataalam waliokua wakitoa mada walikua Prof Endrew Swai na Dr Mohamed Juma.
Kwa ufupi wamesisitiza sana kufanya mazoezi kwa takriban nusu saa kwa siku na ambayo mtu anatoa jasho na moyo kumwenda mbio. Hiyo ni kwa ajili ya kusaidia misuli ya miguu,tumbo kifua, mgongo na mikono kutumia kiasi cha sukari kinachozalishwa mwilini.
Kadhalika wamesisitiza sana kula vyakula visivyokobolewa,ikiwamo kula dona badala ya sembe,ulezi,mtama na matunda.
Watu wapunguze na ikiwezekana kuacha kunywa vimiminika vyenye sukari,ikiwamo juice,soda pombe na vinginevyo. Na hiyo nikwasababu vinywaji hivyo havikai tumboni na badala yake huenda moja kwa moja kwenye utumbo mwembamba na kulazimisha kongosho linalozalisha kemikali ya insulin kufanya kazi kwa kiwango cha juu kuliko ilivyo kawaida.
Vyakula visivyokobolewa vinafaida sana kwani vinachukua muda wa kutosha kutoka kwenye tumbo na kwenda kwenye utumbo mwembamba na hatimaye kuvunjwavunjwa kwa ajili ya kutumika mwilini. Kadhalika makapi yatokanayo na hivyo vyakula hutuzuia kupata kansa ya utumbo. La ajabu wametoa takwimu za kutisha kwani ulaya kwasababu wanakula vyakula vilivyokobolewa wanapata kansa ya utumbo kuliko nchi au bara la afrika,
na kansa hiyo ni ya nne kwa kusababisha vifo barani ulaya na amerika.
Tafadhalini tujihadharini kwani mada ilikua ndefu na nzuri sana kwa mustakabali wetu na afya zetu.
1.Mazoezi ni muhimu
2.Vyakula viwe na uasilia wake
3.Mtu aliye na mwenza wake afanye tendo la ndoa kwa kadiri inavyowezekana kwani ni sehemu ya mazoezi
4. Tubadili mifumo ya maisha yetu,kukaa tu bila kuishughulisha miili yetu.
Atakayeona anataka kupata elimu zaidi hao madaktari niliowataja wapo hospitali ya muhimbili kitengo cha tiba ya kisukari.
Ufahamu juu ya afya yako binafsi …nimeikuta sehemu 👆👆👆👆👆👆

Usisahau kushare makala hii uliyoisoma kuhusu; Dondoo Muhimu kuhusu ugonjwa wa kisukari. Share Facebook, Twitter bila kusahau WhatsApp.

Makala hii kuhusu, Dondoo Muhimu kuhusu ugonjwa wa kisukari, imeonekana kupendwa na wasomaji wengi. Makala nyingine zinazopendwa ni kama hizi zifuatazo;

• Jinsi ya kutengeneza Fagi Ya Kumumunyuka Mdomoni, endelea kusoma...

• Jinsi ya kuandaa Muhogo, Samaki Wa Kuchoma Na Bamia, endelea kusoma...

• Mapishi ya Maharage, endelea kusoma...

• Ugonjwa wa kichomi, endelea kusoma...

• Mapishi ya Wali Wa Kukaanga Kwa Kidari Cha Kuku (Chicken Breast) Wa Kukausha, endelea kusoma...

• Jinsi ya kupika Wali Wa Karoti Na Nyama, endelea kusoma...

• Jinsi ya kupika Pilau Ya Nafaka Na Nyama Ya Kusaga, endelea kusoma...

• Jinsi ya kupika Pilau Ya Samaki WaTuna Na Mboga, endelea kusoma...

• Jinsi ya kupika Pilau Ya Nyama Ya Ng'ombe Na Nyanya, endelea kusoma...

• Jinsi ya kupika Wali Wa Sosi Ya Tuna, endelea kusoma...

Unaweza kusoma makala mpya nzuri kila unapotembelea website hii wakati wowote. Baada ya kusoma makala hii kuhusu; Dondoo Muhimu kuhusu ugonjwa wa kisukari, sasa endelea kusoma makala hizi nyingine nzuri nilizokuandalia;

FURSA.PNG

Fursa Ya Kazi Na Ajira Yenye Malipo Mazuri

Au soma zaidi hapa

.

Slide3-mliopoteana.GIF
mtu.gif