Dalili za kuharibika kwa Mimba

By, Melkisedeck Shine.

Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha mama mjamzito mimba yake kuharibika. Sababu kuu huwa ni magonjwa kama vile ugonjwa hatari wa malaria, ugonjwa unaotokana na zinaa kama vile kaswende na kisonono na U.T.I, dawa fulani fulani mfano Albendazole, Misoprostol, Metronidazole na kadhalika.

Lakini pia mjamzito akifanya kazi za kutumia nguvu nyingi anaweza kusababisha mimba yake kuharibika. Lakini kuna sababu nyingi ambazo zinasababisha mimba kutoka huweza kuzuilika kwa kwenda kliniki mapema yaani pale tu unapohisi una mimba hata kama ni wiki mbili na kufuata ushauri wa wataalamu.

Ukweli ni kwamba kuna wanawake wengi mimba zao huharibika na wao hushindwa kugundua mapema na matokeo yake anakaa na mtoto mfu hata miezi kadhaa bila kujua.

Zipo dalili ambazo husababisha mimba kuharibika kama tutakavyoona leo hapa. Dalili hizo ni hizi zifuatazo:

1. Kuwa na maumivu makali tumboni.

Ikiwa mjamzito atakuwa ana maumivu makali ya tumbo wakati ni mjamzito hiyo pia ni dalili mbaya. Kwa kawaida maumivu makali ya tumbo hasa kwa mimba kubwa ya miezi zaidi ya mitano au mimba ndogo kama mwezi mmoja, basi kuna uwezekano mkubwa kondo imeanza kujiondoa kwenye kizazi kwa mimba kubwa au mimba ndogo imeshindwa kuendelea kukua na moja kwa moja hiyo inaweza kuwa dalili ya kuwa mimba imeharibika.

2. Mimba kutokukua

Ikiwa mimba itaacha kuongezeka au kukua ni dalili nyingine ya mimba kuharibika. Kila mtu aliye mjamzito anategemea mimba iwe inakua kila siku na iwe kubwa kulingana na umri unavyozidi kwenda mbele, ikiwa mimba iko vilevile kwa miezi kadhaa, yaani haikui au ukubwa wa tumbo haubadiliki ujue kwamba mimba hiyo imeharibika, ili kupata uhakika wahi hospitali kupimwa.

3. Mtoto kuacha kucheza tumboni.

Ikiwa mtoto ataacha kucheza tumboni ni tatizo kubwa kwani kwa kawaida mtoto huanza kucheza akiwa na wiki ya 18 mpaka 20 kwa wanawake ambao hawajawahi kubeba mimba na wiki ya 16 mpaka 20 kwa wanawake ambao wameshawahi kuzaa. Ikitokea mtoto aliye tumboni ameshawahi kucheza lakini ghafla akawa hachezi au muda huo umepitiliza na bado kimya kuna uwezekano mkubwa ikawa mtoto huyo amefia tumboni, hivyo haraka sana wahi hospitali kumuona daktari.

4. Kutokwa na damu nyingi sehemu za siri.

Mjamzito akitokwa na damu nyingi sehemu za siri ni dalili kwamba mimba imeanza kuachia na mlango wa uzazi umeanza kufunguka, na hiyo inaashiria kwamba kuna mambo mawili yameshatokea kwanza inawezekana mtoto ameshafia tumboni au bado hajafa, lakini kama damu imetoka kwa wingi inaashiria kuwa mtoto huyo aliye tumboni atakufa tu.

5. Kutoka na vipande vya vyama sehemu za siri.

Ikiwa mama mjamzito atakuwa akitokwa na vipande vya nyama sehemu za siri ni dalili mbaya sana. Kutokwa na vipande vya nyama sirini ni kuashiria kwamba kuna mtoto ameharibika tumboni. Hali hiyo ya hatari ikitokea mjamzito anatakiwa asafishwe kuondoa masalio yaliyobaki.

6. Kupotea kwa dalili za ujauzito.

Kupotea kwa dalili za ujauzito ni tatizo lingine baya kwa mama mjamzito. Mara kwa mara mwanamke akiwa na ujauzito anakuwa na dalili nyingi kama vile kuwa na kichefuchefu, kukosa hamu ya kula baadhi ya vyakula, kutapika, kulamba vitu vichachu kama vile limao, ndimu, wengine hula udogo na wengi hubadilika sana tabia, hivyo basi dalili zote hizo za mimba zikisimama ghafla basi ujue mimba imeharibika.KADI-MMISI-MZAZI.JPG

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Dalili za kuharibika kwa Mimba;

a.gif Sababu, dalili na jinsi ya kujikinga na tatizo la kiungulia kwa wanawake wajawazito

Hii ni hali inayowakumba mama wajawazito walio wengi. Inaweza kutokea kipindi chochote cha ujauzito ila mara nyingi hutokea katika umri wa mimba kuanzia miezi mitatu… endelea kusoma

a.gif Sababu ya tatizo la Tumbo kujaa gesi na jinsi ya kujitibu

Tatizo la tumbo kujaa gesi husababishwa na kumeza chakula pamoja na gesi inayotolewa katika vyakula mbalimbali tunavokula ambayo hujaa tumboni na kwenye utumbo mdogo. Hali hii husababisha tumbo kujaa au kuvimba na mtu hutoa gesi hiyo kwa njia ya ushuzi na kubeua… endelea kusoma

a.gif Faida za ulaji wa Peasi

Peasi ni tunda ambalo limekuwa halithaminiwi licha ya kuwa na faida lukuki katika mwili wa binadamu. Tunda hilo ambalo kwa umbo linafanana na tufaa (apple), lina faida nyingi kwa binadamu iwapo atalitumia mara kwa mara… endelea kusoma

a.gif Faida za kula mayai asubuhi

Mayai ni kitu kilichozoeleka na kinachopatikana kwa gharama nafuu. Kutokana na kuzoeleka huku watu wengi wamekuwa wakipuuza umuhimu au nafasi ya mayai katika afya zao. Pengine kupuuza huku kunatokana na mazoea au ukosefu wa elimu juu ya faida zinazopatikana kutokana na ulaji wa mayai… endelea kusoma

[Kitendawili Kwako] 👉Chakutisha lakini hakikuui

[Fumbo Kwako] 👉Je, hawa walizikwa wapi?

[Chemsha Bongo Kwako] 👉Je, hii familia ina watoto wangapi?

[Kichekesho Kwako] 👉Kuwa na Binti aliyeacha shule

nn.gif

a.gif Jinsi ya kufanya ili upate mtoto wa kike au wa kiume

Katika urutubishaji yai la mwanamke linabeba chromosome X yani XX. Na mbegu ya mwanaume inabeba chromosome XY. Chromosome X kutoka kwa mwanamke ikikutana na Y kutoka kwa mwanaume mtoto wa kiume hupatikana. Chromosome X kutoka kwa mwanamke ikikutana na X kutoka kwa mwanaume mtoto wa kike hupatikana.. endelea kusoma

a.gif Magonjwa hatari 10 yanayotibika kwa kutumia mbegu za Maboga

Mbegu za maboga zina protini na madini ya kutosha na ya mhimu zaidi mwilini kama madini ya zinki, kopa, maginizia, manganizi na chuma, mbegu za maboga ni tamu na zinaweza kutafunwa nyakati zozote na mahali popote hasa kwa wapenda kutafuna-tafuna kama mimi. Tafiti mbalimbali zimethibitisha pasipo na shaka kuwa mbegu za maboga zina faida nyingi kiafya na zina uwezo wa kukuepusha na magonjwa hatari zaidi ya 10 yafuatayo:.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya tambi za mayai

  1. Tambi ½ paketi
  2. Vitunguu maji 2 vikubwa
  3. Karoti 1
  4. Hoho 1
  5. Vitunguu swaumu(kata vipande vidogo) kijiko 1 cha chakula
  6. Carry powder kijiko 1 cha chai
  7. Njegere zilizochemshwa ½ kikombe
  8. Mafuta kwa kiasi upendacho
  9. Mayai 2
  10. Chumvi kwa ladha upendayo.. endelea kusoma

a.gif Njia za kuongeza wingi wa mbegu za kiume

Chakula unachokula kina mchango mkubwa katika kutibu tatizo hili. Vyakula vingi vya kisasa havina uwezo wa kuongeza uwingi wa mbegu… endelea kusoma

[Msemo wa Leo] 👉Mfu wa Mawazo

[Jarida la Bure] 👉Jinsi ya kupika Biskuti za Njugu

[Hadithi Nzuri] 👉Kisa cha baba mzee na mwanae

FURSA..! Kuna nafasi za kazi 100.

Au soma zaidi hapa

.

nn.gif
Slide3-mliopoteana.GIF

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.